Madereva wa zamani Abood Bus Service

fdizzle

JF-Expert Member
Jul 29, 2015
1,891
2,367
Wakuu tuachane na mambo ya siasa kidogo maana zinaumiza kichwa tu
Miaka ya 2000 mwanzoni Abood Bus Service Dar mpaka Moro alitoa toleo jipya la mabasi aina ya Scania yenye bodi za Marcopolo Andare Class.
Kabla ya hapo alikuwa na yale mabasi ya kizamani kuna zile mbili zilikuwa injini nyuma yaani gari inakusogelea kimya kimya husikii sauti ila ikikupita sasa hizo kelele zake hatari.
Kilichopelekea mpaka Abood kuleta basi mpya ni ushindani alioupata toka kwa Hood Ambae alileta Marcopolo Torino.
Baada ya Abood kuleta hizo basi zake,kuna madereva walikuwa wanatembeza zile mashine hatari sana.Mimi niliwakariri wanne wote hao nilipanda basi zao Dar mpaka Moro mantumia masaa mawili na nusu tu.
Wa kwanza alikuwa bonge.Huyu mzee ni mnene hatari Kama Pepe Kalle hivi.Huyu nilipanda basi natokea Moro kwenda Dar.Aisee pamoja na unene wake alikuwa anatembeza mashine hatari.
Mara ya pili tulikuwa na Cresta enzi hizo ndio Kama Athlete za Crown dah huyu jamaa alikuwa mbele yetu tulianza kufukuzana nae kuanzia Mdaula mpaka tunakaribia mizani ya Mikese yeye mbele tu jamaa yetu kila akinyoosha goti wapi basi lipo speed ile mbaya. Mpaka tunampita na kumcheck Ni yeye na barakashia yake kichwani. Sijui Kama kwa sasa bado anaendelea na Abood.
Wa pili kulikuwa na bitozi flani hivi huyu jamaa alikuwa anatembeza scania hatari. Nakumbuka kuna siku tulitoka Msamvu saa saba tunawahi mechi ya kombe la ng'ombe Urafiki(jamaa yangu alikuwa mchezaji) inaanza saa kumi jioni kufika Msamvu tukakuta Hood Inatoka jamaa yangu akaniambia twende Abood.
Kufika Abood tukapanda Safari ikaanza.Dah ile mashine ilitemebezwa ile kukaribia ruvu darajani tukaona mashine inakamuliwa ile mbaya ikabidi tukaze macho mbele kwa mbali tukaona tai kajitawanya nyuma ya basi (hii ni chata ya Hood) yaani ile basi iliyotuacha Msamvu tukaikuta inakaribia Mlandizi.
Yule dereva Wa Hood akakaza nae tukapita Mlandizi Hood mbio mbio Hood mbele Abood nyuma.
Mbele kidogo tukaipita Hood.
Huwezi amini tisa na nusu tupo Ubungo Terminal na basi lilikuwa linasubiriwa lishushe abiria lipakie kurudi tena Moro.
Watatu huyu alikuwa na ndevu za kibeberu kaziacha kidevuni huyu jamaa alikuwa hatari Sana
Siku moja nipo msamvu pale aliilaza gari kwa zile konakona za msamvu mpaka nikahisi anaangusha gari.
Wa nne alikuwa Kibabu fulani hivi ukimuona Kama mzee fulani hivi. Huyu nilimkubali alikimbizana na Ottawa inatoka Songea kuanzia Mikese mpaka mdaula akaja kuipita kwa spidi ya ajabu.
Old is gold
Uzi tayari!!!
 
Uyo dereva bonge wa Abood alikuwa anaitwa Hamis, alishakufaga Kwa presha
 
Dah
So sad
Aliwahi kushuka pale maili moja kwenda kwenye kibanda cha traffic watu walipiga mayowe utafikiri wameona nini
Dah Ila nimejisikia vibaya kusikia amekufa ingawa alikuwa mnene sana
 
ishapita miaka zaidi ya mitano tangia afariki
 
Dah
So sad
Aliwahi kushuka pale maili moja kwenda kwenye kibanda cha traffic watu walipiga mayowe utafikiri wameona nini
Dah Ila nimejisikia vibaya kusikia amekufa ingawa alikuwa mnene sana
Maisha ni kama maigizo kuna wakati mwingine unaambiwa mtu kafa unaona kama utani tu lakini ndio hivyo
 
Dah kweli mkuu
Ila uyo jamaa ni bonge la mtu halafu alikuwa anatembeza zile scania hatari
 
Wakuu tuachane na mambo ya siasa kidogo maana zinaumiza kichwa tu
Miaka ya 2000 mwanzoni Abood Bus Service Dar mpaka Moro alitoa toleo jipya la mabasi aina ya Scania yenye bodi za Marcopolo Andare Class.
Kabla ya hapo alikuwa na yale mabasi ya kizamani kuna zile mbili zilikuwa injini nyuma yaani gari inakusogelea kimya kimya husikii sauti ila ikikupita sasa hizo kelele zake hatari.
Kilichopelekea mpaka Abood kuleta basi mpya ni ushindani alioupata toka kwa Hood Ambae alileta Marcopolo Torino.
Baada ya Abood kuleta hizo basi zake,kuna madereva walikuwa wanatembeza zile mashine hatari sana.Mimi niliwakariri wanne wote hao nilipanda basi zao Dar mpaka Moro mantumia masaa mawili na nusu tu.
Wa kwanza alikuwa bonge.Huyu mzee ni mnene hatari Kama Pepe Kalle hivi.Huyu nilipanda basi natokea Moro kwenda Dar.Aisee pamoja na unene wake alikuwa anatembeza mashine hatari.
Mara ya pili tulikuwa na Cresta enzi hizo ndio Kama Athlete za Crown dah huyu jamaa alikuwa mbele yetu tulianza kufukuzana nae kuanzia Mdaula mpaka tunakaribia mizani ya Mikese yeye mbele tu jamaa yetu kila akinyoosha goti wapi basi lipo speed ile mbaya. Mpaka tunampita na kumcheck Ni yeye na barakashia yake kichwani. Sijui Kama kwa sasa bado anaendelea na Abood.
Wa pili kulikuwa na bitozi flani hivi huyu jamaa alikuwa anatembeza scania hatari. Nakumbuka kuna siku tulitoka Msamvu saa saba tunawahi mechi ya kombe la ng'ombe Urafiki(jamaa yangu alikuwa mchezaji) inaanza saa kumi jioni kufika Msamvu tukakuta Hood Inatoka jamaa yangu akaniambia twende Abood.
Kufika Abood tukapanda Safari ikaanza.Dah ile mashine ilitemebezwa ile kukaribia ruvu darajani tukaona mashine inakamuliwa ile mbaya ikabidi tukaze macho mbele kwa mbali tukaona tai kajitawanya nyuma ya basi (hii ni chata ya Hood) yaani ile basi iliyotuacha Msamvu tukaikuta inakaribia Mlandizi.
Yule dereva Wa Hood akakaza nae tukapita Mlandizi Hood mbio mbio Hood mbele Abood nyuma.
Mbele kidogo tukaipita Hood.
Huwezi amini tisa na nusu tupo Ubungo Terminal na basi lilikuwa linasubiriwa lishushe abiria lipakie kurudi tena Moro.
Watatu huyu alikuwa na ndevu za kibeberu kaziacha kidevuni huyu jamaa alikuwa hatari Sana
Siku moja nipo msamvu pale aliilaza gari kwa zile konakona za msamvu mpaka nikahisi anaangusha gari.
Wa nne alikuwa Kibabu fulani hivi ukimuona Kama mzee fulani hivi. Huyu nilimkubali alikimbizana na Ottawa inatoka Songea kuanzia Mikese mpaka mdaula akaja kuipita kwa spidi ya ajabu.
Old is gold
Uzi tayari!!!
Namiss bongo aisee japo jiwe kai fak-up

Magonjwa Mtambuka
 
Hivi mabasi ya Hood bado yapo?
Yapo mawili ambayo yanafanya safari zake Arusha to Mbeya..hii kampuni ilikua baada ya Mzee Hood kupishana kidogo na watoto wake Tiff na Fesal baba mtu alitaka aachane na biashara ya mabasi awekeze kwenye majengo na biashara zingine kwani pia ukiachana na hilo ana hisa Azania group..alikua anadai kina Tiffu na Fesal Hood walikua wanaiendesha kihasara kampuni..kina Tiffu walikua tayari wameshaweka oda zije gari fulani kali kinoma siku naonyeshwa picha za hayo mabasi yaliyodizainiwa Italy nilipiga saluti lakini ndo hivyo dili likafa baada ya mzee kukataa kutoa mpunga basi mabasi na kampuni ndo ikapotea namna hiyo
 
Hood za Tunduma-Dar miaka ile nimepanda sana SAA 10 kqmili jioni uko Mbeya toka Dar ilikuwepo Hekima na Sabco full ushindani ving'amuzi na tochi zilikuwa chache sana na mizani haikuwa mingi kama sikuhizi. Mkifika Moro nusu saa gari inachekiwa ndo mnaondoka

Back
Top Bottom