ONYO: Abood Bus waonye Madereva wako, Mwendokasi unaua abiria wasio na hatia

Faana

JF-Expert Member
Dec 12, 2011
31,829
33,221
Nipo kwenye Abood Bus T 818 DXJ linalotoka Dar - Morogoro, dakika chache zilizopita tumenusurika ajali kugongana uso kwa uso na lorry karibu na Imperial Sec School Chalinze kisa ni dereva wa Abood kuwa kwenye mwendo mkali na kuovertake lorry lenye namba T662 DEM sehemu isiyoruhusu wakati mbele kuna lorry jingine linakuja.

Dereva wa lorry la kushoto akajitahidi kutoa nje ili tupite lakini haikusaidia ikabidi dereva wa lorry la mbele afunge breki za ghafla kunusuru hali.

Dereva wa Abood alipopenya akafika mbele na kumvizia dereva wa lorry lililotunusuru na kumsogezea bus ili atoke nje ya barabara.

Dereva wa lorry T662 DEM ametoa taarifa Polisi Mdaula na dereva wa bus amezuiwa kuendelea na safari baada ya askari kupata ushahidi kutoka kwa abiria juu ya kilichotokea.

Abood una mabasi mazuri yenye viwango, lakini jitahidi ku-mentor your drivers
 
KIkiwekwa kiwango cha elimu utasikia kwani cheti ndio kinaendesha gari?

Akipata ajali aseme mmiliki anatoa kafara mara nimeona mishale barabarani.(ingawaje yawezatokea )
 
Nipo kwenye Abood Bus T 818 DXJ linalotoka Dar - Morogoro, dakika chache zilizopita tumenusurika ajali kugongana uso kwa uso...
Siku ukifa kwa huo mwendo ndio utaelewa wajibu wako..

Avoid hapandi hayo mabasi wewe Kama abiria ukiona deteva speed muonye huo humo ndani..

Mwisho huwa Kuna namba za trafiki zimebandikwa waandikie Polisi.
 
Ajabu mlalamikaji ni Yule yule! Mi nahisi alipigwa na kitu kizito na bwana dere kwenye mapenz, sasa analipizia kijanja
Huyu dereva alishalalamikiwa March 13, 2022
Nipo kwenye Abood Bus T 818 DXJ linalotoka Dar - Morogoro, dakika chache zilizopita tumenusurika ajali kugongana uso kwa uso na lorry...
Soma vizuri nani amepost nini kisha ipime akili yako
 
Back
Top Bottom