MADEREVA- Jifunzeni kutumia Indicator

Mparee2

JF-Expert Member
Sep 2, 2012
2,580
4,262
Kwa mawazo yangu zaidi ya asilimia 70% ya madereva hawajui kutumia indicator ifaavyo;
Binafsi nimekuwa barabarani muda mwingi na toyo yangu asubuhi na jioni nikienda kibaruani, ukweli ni kuwa kero kubwa ninayo pata ni matumizi yasiyo sahihi ya indicator
Madereva wengi wa magari ya binafsi ambayo ndio mengi na daladala, hawatumii indicator kama inavyo faa...

Wengi wanaonesha indicator wakati wamesha anza kukata au pengine chini ya meta kumi kabla ya kukata!!!! na wengine ndio kabisa hawawashi.

Nimekuwa napata kero sana kiasi kuwa gari la mbele likipunguza mwendo, hata kama naona mbele yake kupo sawa inabidi na mimi nipunguze mwendo pengine kusimama kabisa hadi nijue anataka kufanya nini...KERO!!!!

Chukulia tu mfano wewe umefuatana na gari mwendo wa kawaida tu 80km/h halafu mtu anapunguza mwendo, wakati una anza kumpita (overtake) na yeye ana elekea upande huohuo (overatake)???

Kumbuka indicator ni kwa manufaa ya watu wote wanao tumia barabara (wenye vyombo vingine na watembea kwa miguu).

WANAO FUNDISHA MADEREVA NAOMBA MSISITIZE MATUMIZI SAHIHI YA INDIKETA (INDICATOR) KWANI AJALI NYINGI ZA KUKWANGUANA ZITAPUNGUA. Pia waendesha pikipiki wengi wamekuwa vilema na pengine kupoteza maisha kwa sababu ya matumizi yasiyo sahihi ya waendesha magari...
Najua wengi hawazitetei Pikipiki ila KAMA WEWE NI DEREVA AU DEREVA MTARAJIWA; TIMIZA WAJIBU WAKO....

Nawakilisha!!!!
 
Haswaaa mkuu umenena...hata mimi pia natumia sana pikipiki kwa shughuli zangu za kila siku (si bodaboda) na hizi kero ndo nnazokutana nazo kila siku ya Mungu..tena kuna wale wanatabia wakiona pikipiki ndo wanaizarau kabisa..yaani anakuona kabisa mbele yako kuna gari na kwa hali halisi huwezi overtake afu yeye anakuja nyuma yako anaanza kukupigia honi..sasa niende wapi? afu kama haitoshi anaanza yeye ku overtake then akifika katikati yako anaona sasa hawezi kuovertake anakubana pembeni badala ya yeye kupunguza mwendo kurudi alipokuwa...sasa wewe ndo mtumiaji wa barabara peke yako?

Afu na kuna wale "wakeraji" wengine ambao ikishaingia jioni tu basi wao taa ni FULL mda wote..hajali anapita maeneo gani na hata ukimuonyeshea ishara ashushe taa zake chini ye wala hana hata mpango...hivi kila mtu akiwasha taa Full itakuaje humu mijini?

Mi nadhani Traffic police nao wabadilike sasa, badala ya kukagua leseni, bima na ushuru tu sasa wawe wanaangalia na vitu kama hivi pia..taa, indicator na vitu vingine vya utendaji wa gari...
 
Katika miji niliyotembea Makambako ni balaa,madereva wakazi wa kule kati ya 50 wanaotumia indicator ni watano.
 
Back
Top Bottom