Madeni Special thread: Changamoto gani unakutana nazo wakati wa kudai na kudaiwa?

Mi nadhani huyu ndugu amekueleza kuwa alipitia changamoto hakuitegemea
Japo sio justification hio ya kutokulipa
Maneno yako pia duh hatariii una maneno ya shombo


Hayo maneno ni ya kawaida sana mkuu, kuna watu wana maneno makali sana bado hujakutana nayo nadhani....

Ila ukiwa muwazi inakujengea imani kwa watu, huyu jamaa angenijulisha tangu mwanzo jambo lililomkuta, mimi ningemtoa akilini kumdai hadi pale hali yake ikitengamaa ndio anilipe.

Sio vizuri kumuambia mtu siku fulani nitakupa, halafu ikifika hiyo siku ukikumbushwa unazingua
 
Orodha ya taasisi zinazo nidai
HESLB: 12,568,400/=
BENKI YA CRDB (SALARY ADVANCE) 75,000/=
TPB BANK: 1,000,000/=
NBC BANK: 1,200,000//=
BOA: 1,000,000/=
ABC BANC: 4,367,390/=
TIGO NIWEZESHE: 48,000 (WAMENISAMEHE MAANA NATUMIA TIGOPESA FRESH TU)
AIRTEL MONEY: 35,000/= (NIMETUPA LINE)
BRANCH 18900/= WANANITUMIA VITISHO
TALA: 22,000/= WALINITISHAGA MPAKA WAMEFILISIKA.

Bado naamini nakopesheka, mimi ni tajiri mno, nisingekuwa tajiri wasinge nikopesha. NATEMBEA KIFUA MBERE!

HAKUNA RAIA WAKAWAIDA ANAYE NIDAI UKIONDOA ILE 60,000/= NINAYODAIWA NA WASHKAJI NA MWEZI HUU NITAPUNGUZA 35,000/=

Sent using Jamii Forums mobile app
Hahaha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Orodha ya taasisi zinazo nidai
HESLB: 12,568,400/=
BENKI YA CRDB (SALARY ADVANCE) 75,000/=
TPB BANK: 1,000,000/=
NBC BANK: 1,200,000//=
BOA: 1,000,000/=
ABC BANC: 4,367,390/=
TIGO NIWEZESHE: 48,000 (WAMENISAMEHE MAANA NATUMIA TIGOPESA FRESH TU)
AIRTEL MONEY: 35,000/= (NIMETUPA LINE)
BRANCH 18900/= WANANITUMIA VITISHO
TALA: 22,000/= WALINITISHAGA MPAKA WAMEFILISIKA.

Bado naamini nakopesheka, mimi ni tajiri mno, nisingekuwa tajiri wasinge nikopesha. NATEMBEA KIFUA MBERE!

HAKUNA RAIA WAKAWAIDA ANAYE NIDAI UKIONDOA ILE 60,000/= NINAYODAIWA NA WASHKAJI NA MWEZI HUU NITAPUNGUZA 35,000/=

Sent using Jamii Forums mobile app

aiseee


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
HABARI WANAJAMVI.

Ni matumaini yangu kuwa mko salama. Tujielekeze kwenye mada husika. Katika maisha yetu ni kitu cha kawaida kudaiwa aidha fedha, vitu n.k au Kudai. Madeni ni kitu cha kawaida lakini kimepelekea watu kugombana hata mahusiano kuvunjika au kufa kabisa sababu ya madeni..

Uzi huu nimeuleta rasmi Ili watu wafunguke changamoto wanazokutana nazo katika kudai na kudaiwa, Funguka unadaiwa kiasi gani au unadai kiasi gani kwa watu mbalimbali naunafanya nini kumaliza madeni yako au unafanyaje kudai madeni huku ukiendelea na uhusiano mzuri na wadeni wako?

Upande wangu. Kuna rafiki alikuja ofisini kwangu akaomba nimkopeshe laptops 6 used kwa ajili ya kiofisi chake kipya gharama yake ilikuwa Tsh 3,000,0000/= yaani 500k@ laptop. Akatoa advance 500K. Namdai 2.5M. Huu ni mwezi wa 6 sasa ananizungusha. Na alivyo wa ajabu kwa sasa kila siku asubuhi amekuwa mwaminifu sana hunitumia mafungu ya Biblia yenye mrengo wa namna Mungu anavyotupenda na tunavyopaswa kuwasamehe wengine. Sasa sijui ndo nishadhulumiwa?.

KARIBU FUNGUKA CHANGAMOTO ZAKO ZA MADENI NA NAMNA GANI TUSAIDIANE HAPA.

Sent using Jamii Forums mobile app

Nimecheka kama mazuri 🤣🤣🤣🤣🤣 eti vifungu vya bible daah unajua kuna kitu mtu anaweza akasema ukajua tu kilipo tokea, yan kwa maelezo yako hizi ni sound za watu wa dar 🤣🤣🤣🤣🤣🤣, ukitaka kwenda kumfanyia ambush kakuwah na vifungu vya bible 🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Ukichilia mbali deni la bodi ya mikopo, nina deni la 1.8m ambayo bado sijaanza kulipa,
Rafiki yangu aliniita na kunipatia/kunikopesha hiyo pesa ili tuu nihamie katika kibanda changu, baada ya kuona muda wa kodi umekaribia akashauri nichukue hiyo pesa ili nisilipe tena kodi, alishauri nitalipa kidogo kidogo pale ninapoweza " nikajisemea dunia hii watu wema bado wapo "
Napambana ili mwezi huu Disemba nianze kulipa deni la watu, najua hana nyingi lakini alitoa kwa moyo wake wote,
Mungu ni mwema siku zote

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Zaidi ya milioni 150. Afu sina hata 1000 mfukoni

Sent using Jamii Forums mobile app

we jamaa nlikuwa nadaiwa 20 nikapambana mpaka nikailipa kwa mbinde sasa ivi naona nna ahueni yan napumua kabisa nakaa bar naagiza six pack ya budwizer 🤣🤣🤣🤣, deni lisikie tu kwa mtu aisee, alafu ela yenyewe nlienda kufanya kilimo hela ikazama shambani kudadeki...


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Mie nina mpangaji wangu, ni baba mwenye familia yake, sasa hapo kwenye nyumba yangu alimpangishia mchepuko wake, nina mdai kodi ya miezi sita, sababu ananiambia hali ngumu!
Nikamuuliza kama unajua una hali ngumu kwanini ujiingize kwenye kupangisha mchepuko?
Jibu lake: "sasa hapo naona mama unaingilia faragha yangu..."
Nawaza kumtimua kwa kweli!
Nipangishe mie nahitaji chumba
 
Back
Top Bottom