Madeni Special thread: Changamoto gani unakutana nazo wakati wa kudai na kudaiwa?

swahiba Senior

JF-Expert Member
Nov 12, 2016
2,479
3,613
HABARI WANAJAMVI.

Ni matumaini yangu kuwa mko salama. Tujielekeze kwenye mada husika. Katika maisha yetu ni kitu cha kawaida kudaiwa aidha fedha, vitu n.k au Kudai. Madeni ni kitu cha kawaida lakini kimepelekea watu kugombana hata mahusiano kuvunjika au kufa kabisa sababu ya madeni..

Uzi huu nimeuleta rasmi Ili watu wafunguke changamoto wanazokutana nazo katika kudai na kudaiwa, Funguka unadaiwa kiasi gani au unadai kiasi gani kwa watu mbalimbali naunafanya nini kumaliza madeni yako au unafanyaje kudai madeni huku ukiendelea na uhusiano mzuri na wadeni wako?

Upande wangu. Kuna rafiki alikuja ofisini kwangu akaomba nimkopeshe laptops 6 used kwa ajili ya kiofisi chake kipya gharama yake ilikuwa Tsh 3,000,000/= yaani 500k@ laptop. Akatoa advance 500K. Namdai 2.5M. Huu ni mwezi wa 6 sasa ananizungusha. Na alivyo wa ajabu kwa sasa kila siku asubuhi amekuwa mwaminifu sana hunitumia mafungu ya Biblia yenye mrengo wa namna Mungu anavyotupenda na tunavyopaswa kuwasamehe wengine. Sasa sijui ndo nishadhulumiwa?.

KARIBU FUNGUKA CHANGAMOTO ZAKO ZA MADENI NA NAMNA GANI TUSAIDIANE HAPA.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mie nina mpangaji wangu, ni baba mwenye familia yake, sasa hapo kwenye nyumba yangu alimpangishia mchepuko wake, nina mdai kodi ya miezi sita, sababu ananiambia hali ngumu!
Nikamuuliza kama unajua una hali ngumu kwanini ujiingize kwenye kupangisha mchepuko?
Jibu lake: "sasa hapo naona mama unaingilia faragha yangu..."
Nawaza kumtimua kwa kweli!
 
IMG_7333.JPG

Akija na mstari wa Biblia na wewe mpelekee huo
 
Back
Top Bottom