Madee amedai angekuwa ameathirika na matumizi ya Madawa ya kulevya, angewataja wanaomuuzia

explicity

JF-Expert Member
Oct 9, 2015
207
140
Msanii wa muziki kutoka Tip Top Connection Madee Ali amesema kama angekuwa anatumia Madawa ya kulevya na tayari ameshaathirika basi angewataja wale wanaomuuzia ili kuisaidia serikali kutokomeza matumizi ya madawa ya kulevya
20ab70de9c3412528e779aa023724745.jpg
Akizungumza katika kipindi cha Enewz cha East Africa Television, Madee amesema serikali inaweza kutokomeza biashara ya Madawa ya kulevya kama ikiwatumia wale walioathirika.
“Ningekuwa mimi natumia Madawa ya kulevya na tayari yameshaanza kuniathiri si utaulizwa imekuwaje kuwaje, nani amekufundisha hizi mambo, umeanza wapi umenunua kwa nani, ina maana nitaanza kumtaja yule ambaye ameniuzia, na ambaye ameniuzia mimi kikete, yeye atamtaja bosi wake, bosi wake atamtaja yule bosi wake mkubwa kwa hiyo ile cheni yote itakuja mpaka itamfikia yule kigogo anayeingiza kutoka nje”, alisema Madee
Pia Madee alisema ingawa wasanii wana nafasi yao katika kupambana na biashara ya Madawa ya kulevya, lakini serikali ndio chombo ambacho kinaweza kupambana na biashara hiyo na inatokomea kabisa. Credit bongo5.com
 
Umeelewa vibaya mkuu nilikua nauliza pia.
Poa mkuu, ila jamii sasa inatakiwa ibadilike na kuanza kutaka sheria iwe kali zaidi ili na hao wanaovuta wajumuishwe kwenye hukumu yaani wavutaji au watumiaji nao wawe wahalifu
 
Back
Top Bottom