Made in Tanzania

Rev.Kishoka,
"je ni lini nitaweza kutumia kila kitu pale Ikulu na hata kununua madukani bidhaa zinazosema "made in Tanzania"?
Siku utakapolazimisha wahusika wote kufanya hivyo pasipo kuwaomba. Toa amri na hakikisha kinafanyika..
Sidhani kama kuna sababu ya kuuliza hawa WATU ambao kwanza hawafahamu umuhimu wa maagizo yako. Kama nilivyosema bado tunaishi ktk dunia ya stone age kiasi kwamba nadiriki kusema tofauti baina ya hao wasomi na yule Moran Masai au Wabarber ni kutokana na kuelewa matumizi ya vitu vya nje.

Kwa hiyo kazi kubwa unayotakiwa kufanya ni kuleta mkakati ukiwa na kifimbo mkononi kama cha mwalimu. Toa agizo na hakikisha linafuatwa na kila mhusika, kwani utawala wa nchi zetu unahitaji Udikteta, mabavu na amri moja. Nitashauri tu kwamba lugha na uungwana ulotumia hapo juu haufai kabisa na hauwezi kufanya kazi.

Wapo wengi ambao hawakufahamu kwa nini mwalimu alichapa watu bakora, kwa nini alikuwa dikteta hivyo siku baada ya siku ktk kiti chako cha Ikulu, utakuja elewa wazi kwamba Mdanganyika ni kama Punda haendi pasipo bakora..Ikiwa Loliondo na Bulyankulu zimechukuliwa kwa mabavu na bado wananchi wengi (wasomi) hawafahamu ubaya wake, itakuwa vipi waelewe uzuri wa mchango huu..
 
Tatizo kubwa ni kuwa kati ya viongozi tunaowapata, ni wachache sana wanafikiria kuhusu Tanzania... wengi wanajifikiria wenyewe na iwapo wataamua kujifikirisha zaidi watawafikiria ndugu zao
 
Back
Top Bottom