Made in Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Made in Tanzania

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Rev. Kishoka, Nov 29, 2009.

 1. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #1
  Nov 29, 2009
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Nawaza ni mwaka 2011 na nipo pale Ikulu, Rais Rev. Kishoka, natafakari cha kufanya ili kusisimua uzalishaji wa ndani na naita mkutano na Wafanyabiashara kupitia TCCIA, Wizara ya Biashara, Chama cha Wakulima TFA, Wizara ya kilimo, uvuvi na mifugo na watu wa TBS, Chakula Bora na Waziri Mkuu.

  Tukiwa tunakunywa maji ya matunda ya Maaza na kufinyanga vipande vya nyama vilivyonunuliwa shoprite na mkusanyiko huo kuhudumiwa na Movenpick, nawauliza wote walioko,

  "je ni lini nitaweza kutumia kila kitu pale Ikulu na hata kununua madukani bidhaa zinazosema "made in Tanzania"?

  Wakiwa bado wanatafakari, nitawarushia kombora jipya na kutoa amri ya upole kuwa ikifika mwaka 2013, nataka nione kuwa kila kona kuna bidhaa zilizotengenezwa Tanzania na kuzalishwa Tanzania! Zaidi natoa amri kwa mtu wa Ikulu, Luhanjo wangu kuwa kuanzia siku hiyo, ni marufuku kwa Ikulu kutumia bidhaa kutoka nje, ikiwa bidhaa hizo zinazalishwa Tanzania na tunauwezo wa kuzitengeneza (manufacture) zitumike.

  Nitawageukia Wafanyabiashara, Wakulima na Mawaziri wa wizara husika na kuwauliza, wanahitaji nini kutoka kwangu na Serikali yangu ili mkate, siagi, maziwa, matunda, asali, chai, soda, bia, mvinyo, mayai, nyama, mchele, mahindi na aina yeyote ya Chakula kinachopikwa na kutumika Ikulu ni mali ya Tanzania kutoka kwa Mkulima wa Kitanzania na kusindikwa kwa ubora wa kimataifa na kampuni ya Kitanzania?

  Nitaendelea na kuwauliza Wafanyabiashara wenye viwanda, ni lini Ikulu itaanza kutumia karatasi zinazozalishwa Tanzania kwa kutumia miti ya Tanzania? ni lini penseli, kalamu na samani za ofisini na nyumba za Ikulu zitakuwa zote ni mali ya Tanzania kuanzia malighafi mpaka zao la mwisho?

  Je itakuwa ni makosa kutoa amri na agizo kama hilo na kuwataka wanieleze wanataka nini kutoka kwangu ili mimi kama Rais wa Tanzania na Raia wa Tanzania waanze kujivunia matunda ya mazao yetu na si kufikiria mara mbili mbili tukienda Shoprite ambako asilimia 97% ya bidhaa ni kutoka nje ya nchi?

  Hivi kutakuwa na ubaya gani ikiwa VOIL na Tanbond ikawa ndio chaguo la Mtanzania badala ya Blue Band na Korie?

  Je ni dhambi kuona kuwa nyama na vyakula vinazalishwa Tanzania kwa ubora kama ule wa zile nyama za Farmers Choice kutoka kenya au zile nyama za Afrika Kusini?

  Je ni dhambi kuona kuwa tunaanza kutengeneza samani nzuri kwa kutumia mafundi wetu na viwanda vyetu badala ya kuagiza kutoka Dubai?

  Je nitakuwa nimekosea kutoa hamasisho kama hilo kwa Wafanyabiashara ili kuzindua upya shughuli za Uzalishaji mali wa nchi yetu kitu ambacho kitatoa ubora wa bidhaa zetu na zaidi kutoa ajira kwa Watanzania na kuachana na uagizaji wa bidhaa na vyakula ambavyo tuna uwezo mkubwa wa kuzalisha wenyewe na hivyo tuache kuomba mikopo au kutumia fedha zetu za kigeni kununulia vitu ambavyo tunavyo hapa hapa nchini?
   
 2. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #2
  Nov 29, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  ni wazo zuri sana mkuu. Ukiangalia nchi zingine wana tumia kadri ya uwezo wao vitu vilivyo tengenezwa kwao. Kwa mfano msafara wa raisi wa Marekani au Ujerumani hauwezi kuona gari la kigeni. That's how it should be.

  Tatizo ni kwamba hatu hamasishi wajasiria mali Tanzania. kila siku ni kelele za kilimo kwanza. Karne hii nchi uchumi wenu una tegemea kilimo? Tena cha hali ya chini? Najua kwa sasa kuna bidhaa kama magari ambazo tuna weza kutengeneza wenyewe ila vipo vitu ambavyo tunaweza na vingi vyao usha vitaja hapo juu.
   
 3. P

  Papa Sam Senior Member

  #3
  Nov 29, 2009
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 102
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mawazo ya kimapinduzi, hakuna watekelezaji, nnchi yenye rais anaefat bembea Jamica, nnchi yenye kiongozi anaeamini kua bila misaada ya kifedha toka maghalibi hawezi kuleta maendeleo yoyote, tuna raisi anayehusudu vya watu kuliko wakati mwingine wowote
   
 4. N

  Njimba Nsalilwe JF-Expert Member

  #4
  Nov 29, 2009
  Joined: Mar 23, 2008
  Messages: 251
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  President Kishoka,

  Made in Tanzani? Good dream but ....

  Hiyo ni ndoto nzuri sana, tatizo watu wote utakao zungukwa nao walishapoteza uzalendo wa nchi hii. So for them "made in Tanzania" what for?

  Wangekuwa nao mengi tunayo yaona leo yasingetokea chini yao.

  Inaaminika ufisadi wote unaofanya nchini unapangwa na wazalendo wenyewe; Eg. EPA, na madudu mengine mengi.

  Hebu fikiria mafisadi wa EPA wangejuaje kama kuna hela bila Bilali kusema? Huu ni mfano mdogo tu.

  Ukitaka, itabidi uanze kumuondoa Luhanjo na wenzake uje na timu nyingine mpya, vinginevyo utakuwa umeshindwa kabla ya term yako ya kwanza kuisha.

  Njimba
   
 5. Tumain

  Tumain JF-Expert Member

  #5
  Nov 29, 2009
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 3,158
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  unagombea kwa kutumia fedha kutoka wapi? ukipitisha kapu lako lazima utabeba mafisadi watakaohitaji malipo..challenge no 1

  Saddam alitaka kufanya made in Iraq..aling'olewa na wenye dunia? challenge no 2

  wasomi wako wa kutengeneza makaratasi, etc made in tanzania..watachonga deals kama za epa, na richmond wataku-fyonza mpaka uje kuwashtukia mwaka wa nne- challenge no 3.

  need to address hizo challenge kwanza..utafikaje hapo?, external challenge? na internal operational problems kazi kwako.
   
 6. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #6
  Nov 30, 2009
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Kwa nini tunaweka mbele hujuma na fikra kuwa tutahujumiwa na si kujiuliza kama tuna uwezo wa kufanya ambalo Rais Kishoka analiagiza?
   
 7. M

  Mkandara Verified User

  #7
  Nov 30, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Rev. Kishoka,
  Kwanza kumbuka maneno yangu... WATU na MAZINGIRA kisha weka mikakati inayolingana nao kwani haya ni mawazo mazuri sana kama ya mwalimu lakini watu wenyewe (Limbukenis) na ktk Mazingira (stone age) wakitaka changes huvamia chochote mbele yao.

  Acha mbali IKULU, mitaani leo hii kuku wa kienyeji hana market kuliko kuku wa kidhungu (kizungu) pamoja na kwamba ufugaji wake ni mgumu kupindukia. Heineken inanyweka kuliko beer ya nyumbani..Mkenya au Mpopo anaitwa Foreigner na sifa kwa mwanamme au mwanamke wa Kitanzania kuwa karibu naye. Khanga ya Maleysia ina thaminika kuliko ya Tanzania..Modified food against Organic ili mradi tupo ktk mpito wa Ulimbukeni ni kazi kubwa sana kujaribu kuyabadilisha Mazingira yetu wakati hatuna vifaa ama elimu inayolingana na rasilimali tulokuwa nazo.
  Kisha basi ajabu ni kwamba hao tunaowaiga iwe Waingereza au Marekani, hawajui dunia nyingine zaidi ya nchi zao wenyewe labda ktk vitu ambavyo hawavizalishi na kwa sababu maalum.
  Kifupi huyo waziri, Wafanyabiashara, na wakulima wataondoka wamechanganyikiwa kabisaaa. Mali toka nje itapigwa marufuku na uzalishaji utarudi chini zaidi kwa sababu kila mmoja wao hana elimu wala fikra za kulima isipokuwa Kulimwa..
   
 8. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #8
  Nov 30, 2009
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145

  Rev.Kishoka ukiona mawazo haya yanatawaka basi ujue watu wamesha kataa tamaa na hawajitambui ndiyo maana wanakuja na mawazo mgando
   
 9. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #9
  Nov 30, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Kishoka,
  Uwezo wa kufanya hayo yote uliyoyataja Tanzania tunao. Kinachokisekana ni nia. Kuna wakati enzi za Mkapa rafiki yangu mmoja alikuwa na kiwanda chake cha maziwa na uwezo wa kusupply Dar. Lakini mahoteli kuanzia Sheraton yalikuwa yakileta maziwa kutoka Afrika kusini na kwa sababu walikuwa wamepewa likizo ya kodi basi waliweza kuyaingiza yale maziwa bila ushuru. Rafiki yangu akahenya mpaka akapata appointment Ikulu. Akawaambia kinachoua soko la ndani ni hizi bidhaa zinazoingizwa kutoka nje bila kutozwa kodi. Ikulu wakageuka viziwi. Uwezo tulikuwa nao lakini nia ilikuwa ni kuleta vitu vya Kaburu.
   
 10. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #10
  Nov 30, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Kwa bahati mbaya inaonekana kuwa nchini Tanzania watu wenye mawazo ya kwako huwa hawafiki mbali, na bahati mbaya zaidi ni kuwa wanapuuzwa. Siasa za Tanzania zinahitaji chuki,fitna,blackmail na udanganyifu kuingia madarakani, na ukiingia madarakani unatakiwa uchote kwanza mpaka uchoke ndio uifikirie nchi yako.

  Ndio maana watu kama Mrema wenye uzalendo na Tanzania leo wako hoi, na mafisadi wanapeta tu.
   
 11. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #11
  Nov 30, 2009
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Mkandara,

  Naelewa ni watu na Mazingira ndio maana pamoja na kutoa agizo, nimewauliza wanahitaji nini kutoka kwangu na Serikali yangu ili wafanikishe Agizo hilo. Maana sitataka kusikia tuunde tume au kisingizio kwa nini tumeshindwa!

  Jasusi,

  Uwezo tunao, Sababu tunayo, Nia ni lazima tuiamshe na kuileta na si kukubali kuwa wachache walio wavivu au wahujumu waingilie safari ya kuleta maendeleo. Naelewa fika kuna wapinga maendeleo na wahujumu wa ndani na nje ya nchi, ni wajibu wetu kusimama kidete na kushinda majaribu.

  Bongolander,

  Inabidi tuanze kuzalisha jamii mpya ya Watanzania ambao hawayumbishwi na inda au ujinga na upumbavu uliotuzalishia uozo tulio nao!
   
 12. Triplets

  Triplets JF-Expert Member

  #12
  Nov 30, 2009
  Joined: Sep 27, 2007
  Messages: 1,103
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  yote hayo uliyopendekeza hapo juu yanawezekana kabisa Mr. President mtarajiwa Kishoka.
  ila itabidi yafanyike kiamri amri na kibabe kibabe, hata kuingia hapo ikulu itabidi upindue nchi kwanza..
   
 13. JuaKali

  JuaKali JF-Expert Member

  #13
  Nov 30, 2009
  Joined: Nov 14, 2007
  Messages: 785
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Hayo ni wamazo duni saaana, na tukiendelea kufikiria hivyo mwaka 2050 utatukuta hivi hivi tukipiga porojo.
   
 14. Z

  Zhule JF-Expert Member

  #14
  Nov 30, 2009
  Joined: May 22, 2008
  Messages: 354
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Made in Tanzania ilizikwa na Mzee ruksa.Aliona akuna haja kuangaika kufikiri namna ya kutengeneza wakati wenzetu wanavyo.Mkapa akamalizia kuziuza basi.Mzee kikwete ameridhika hana time anabembea uko jamaika.Shida kweli kweli
   
 15. Mwalimu

  Mwalimu JF-Expert Member

  #15
  Nov 30, 2009
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 1,475
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Hawa Shoprite Kenya hawapo...wamepigwa chini
   
 16. h

  housta Senior Member

  #16
  Nov 30, 2009
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 160
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Mkuu heshima zako,

  Ninaamini kuwa kukubali kuwa conservative au liberal ni chaguo la mtu.Kukubali hizo "Special Interest" groups pia ni chaguo la mtu.Sikubaliani kuwa ukitaka kuwa kiongozi wa nchi lazima upate baraka za "Special Interest" groups.Nchi bado ina wazalendo wachache na ndio hao hao watakatoa mwamko na kukazaliwa wenye mwammko wengine,that is how it goes.Kuna watu naamini wanatamani sana kulianzisha lakini wanaogopa wasije wakawa ni wenyewe.Inahitaji a "VOICE" and you will see what will happen.Am not saying this to disrespect what you have said BUT I BELIEVE kukiwa na mwamko,EVERYTHING IS POSSIBLE.Watu waache uoga.Of course kila kitu kina gharama yake lakini tutafika kule tunapotaka kwenda.

  Nawasilisha.
   
 17. Tangawizi

  Tangawizi JF-Expert Member

  #17
  Nov 30, 2009
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 2,835
  Likes Received: 927
  Trophy Points: 280
  Sio tu hatuwapi hamasa wazalishaji wa ndani, bali pia tunawawekea mazingira ya magumu ya kuweza kufanikisha biashara zao, unless wamekuja na the so called wawekezaji wa nje. Kama kuna kitu kinatusumbua ni hili la kuamua bila kujari athari zake kwamba hatuwezi kufanya lolote bila uwekezaji wa nje.
  Na hii kelele ya kilimo kwanza unaweza shangaa ikageuka wimbo wa taarabu huko mbele ya safari. Very unfortunately hatuko serious about ourselves and what we do.
   
 18. W

  WildCard JF-Expert Member

  #18
  Nov 30, 2009
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Na viwanda vya kutengeneza vitu vyetu wenyewe bado vipo. Ni kuvipatia mtaji tu na kuviweka mbali na WANASIASA wetu. Tuige kidogo sheria kali za CHINA (naamini hili Rev. unaliweza kama mabandiko yako humu ndio wewe!). Hebu tukumbuke kanga na vitenge vya Urafiki, Mwatex, Mutex. Juisi na mikate ya NMC, nyama ya Kongwa, kuku na mayai ya ilyokuwa NAPOCO,......
   
 19. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #19
  Nov 30, 2009
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,582
  Likes Received: 3,882
  Trophy Points: 280

  Inawezekana kabisa mh.rais.

  Kwa sababu kama bila aibu tuliweza kukaa uchi mbele ya mataifa mengine nadhani kuvaa nguo itakuwa ni chapchap.Hata kama wanaokuzunguka hawatafurahia, ila watoto wao watafurahia!
   
 20. Injinia

  Injinia JF-Expert Member

  #20
  Nov 30, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 850
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Nina rafiki yangu mKenya nilikuwa nae Moshi mjini wakati fulani tukaingia dukani kununua vitu vya nyumbani, yeye naye anaishi Moshi. Nilipomueleza kuwa mimi sinunui kitu ya Kenya unless extremely necessary, na yeye akasema vivyo hivyo kuwa hanunui chochote made in TZ, hata toilet paper!! Ananunua vya Kenya tu. Hiyo inaonesha jinsi gani soko la TZ limefurika bidhaa za Kenya, kiasi kwamba raia wa Kenya anaweza kusurvive Tanzania bila kutumia bidhaa ya Tanzania!!

  Mimi sikumbuki mara ya mwisho niliyotumia, kwa mfano vienna/sausage za Farmer's Choice, tangu viwanda vya Tanzania viweze kuzalisha bidhaa hizi ( Healthy Choice, na kile kiwanda cha Morogoro, sikumbuki jina)
   
Loading...