Made in Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Made in Tanzania

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by ThinkPad, Aug 13, 2009.

 1. ThinkPad

  ThinkPad JF-Expert Member

  #1
  Aug 13, 2009
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 1,851
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Hii inatufundisha nini haswa?
  Katika matokeo ya Form 4 yaliotoka miezi michache iliyopita Mwanafunzi kutoka shule ya Kata Aibuka kidedea aongoza hesabu Tanzania nzima, ni kutoka katika Wilaya ya Tarime shule ya Secondary Nkende ipo njiani ukiwa unaelekea Sirari ipo nje ya mji wa tarime inapakana na Mlima wa Chambili (aliyekuwa mbunge wa tarime).

  Ningependa serikari iweke kila mahitaji ya wanafunzi ili waweze kufanya vizuri zaidi,
  Naamini nkende hakuna umeme wala hawana Labaratory kwa ajili ya practical je! ni wanafunzi wangapi wenye uwezo ktk hizi shule za kata lkn wanakosa Miundombinu ya kusoma kwa vitendo?

  Wananchi tusidharau shule za kata hata kama zipo kijijini kama ilivyo hii Nkende,

  Wizara iwemakini katika kuangalia shule zote kwa usawa maana kama hizi shule zikikosa maabala labda tungepata mtaalamu lkn kutoka na miundombinu mtu anaashindwa kufanya masomo ya sayansi anakimbilia masomo ya Siasa ambayo hayaitaji maabala na hivyo tunapoteza vichwa muhimu ktk taifa letu.

  Na Wizara husika inashindwa kumpa moyo na kutoa changamoto ili watu wasikimbilie St, Seminary n.k , Lakini naamini tutafika tu na sisi tutakuwa juu miakahiyo tukiona Computer,simu, Printer n.k vimeandikwa MADE IN TANZANIA

  Wizara husika isimamie haya mambo ya Elimu maana bila elimu hatutatoka jamani kwani hatuoni mfano kwa wenzetu!!!!!

  Nawakilisha.
   
  Last edited: Aug 13, 2009
 2. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #2
  Aug 13, 2009
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,159
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Mkuu hiyo ya shule ya kata kutoa best student ni 1 kati ya 1,000,000! Cha msingi kama ulivyosema, ni serikali kuhakikisha mazingira ya huko shule za bush yanaboreshwa!
   
 3. ThinkPad

  ThinkPad JF-Expert Member

  #3
  Aug 13, 2009
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 1,851
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Next.........,
  Yaani huku Tz kuna vichwa balaa nadhani hata huko Sikonge nishasikia kuna jamaa walipasua mpaka ,

  Na walimu pia ni isue maana kweli kabisa wakipewa mishahara minono kweli jamani tutaona vitu kibao vimeandikwa made in Tanzania
   
 4. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #4
  Aug 13, 2009
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,159
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Ha!ha!ha!ha! naona mkuu ulitaka unipeleke Sikonge......sipo huko kaka! Kule bush ya kwetu wananchi wenyewe huwa wanafanya harmbee kuboresha mazingira ya shule pamoja na ya walimu so mambo si mabaya kivile mkuu!

  Bt all in all kuna vichwa vingi sana TZ vinapotea coz ya kukosa mazingira bora ya kuviendeleza!
   
 5. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #5
  Aug 13, 2009
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  ThinkPad,

  Wee unaongelea mwaka gani? Mwaka Jaji Mfwalila yuko Sekondari nini?

  Wakati huo hata Sekondari haikuwepo Sikonge.

  Hii sifa yako imekaa kimashakamashaka. Nahisi kama unasema Sikonge pia walitumia NYENZO aka phantom aka kunyonyesha mtoto.
   
 6. ThinkPad

  ThinkPad JF-Expert Member

  #6
  Aug 15, 2009
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 1,851
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Sikonge kumbe na kwenu hali mbaya?,
  Sasa tufanyeje kama dunia nzima hakuna nchi ambayo imefanikiwa bila watu wake kwenda shule.
  Jana nimesikia kwenye magazeti kwamba Serikali itajenga maabala kwa kila shule sijui wataanza lini.

  Kushakucha watu ndo wanakumbuka shuka tutakuwa tukiongoza kutoka mwisho maana elimu imegeuzwa biashara hapa kwetu kama tu huduma ya afya eti dawa ya malaria 12000 wakati watu wangesoma na kuwekewa mazingira staili wangeweza kufyatua hizo dawa .We need changes now ...
   
Loading...