Madaraka ya kulevya na intelijensia ya kishenzi

Madaraka ya kulevya na intelijensia ya kishenzi

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
361,124
Reaction score
831,803
Pamoja na kwamba marehemu hana haki lakini damu ya mtu haiendi bure! Karma is bitch.... And this bush has a story to tell....!!!!

F.jpg


Chris Musando RIP kafa kifo cha mateso makubwa, Mtaalam mwandamizi wa mambo ya ICT kwenye tume ya uchaguzi Kenya
Ni mmojawapo wa watu wachache sana nchini Kenya aliyekuwa anajua servers za tume ya uchaguzi Kenya zilipo

Siku chache zilizopita aliteuliwa KUKAIMU nafasi nyeti ya usimamizi kitengo cha ICT kwenye tume ya uchaguzi Kenya, mtangulizi wake alilazimishwa kwenda likizo ya mwezi mmoja. Alikubali uteuzi lakini pengine uzalendo kwa nchi yake ulimfanya asikubaliane na matakwa ya kundi fulani (kundi la madaraka ya kulevya)

Alianza kupokea vitisho siku chache baada ya uteuzi, alichukua hatua stahiki kwa kuripoti kituo kikuu cha polisi na akapewa ulinzi maalum wa askari wasiopungua sita wenye silaha na magari mawili (chase cars)

Mara ya mwisho alionekana ijumaa jioni akitoka kazini na ujumbe waje wa mwisho (hausemwi) aliutuma usiku wa manane kuamkia jumamosi kwenda kwa rafiki yake! Mwili wake ulikuja kuokotwa nje ya jiji la Nairobi vichakani ukiwa na majeraha mgongoni kichwani usoni tumboni na mkono mmoja ukiwa umevunjwa kabisa... Dalili za kifo cha mateso sana...

Pamoja naye alikuwa na mwanamke ambaye hajatambulika(most likely alitumika kama chambo). Kwa maslahi ya wachache Chris ameacha mjane na yatima, amewaacha ndugu jamaa na marafiki, ameondoka na elimu na utaalam wake mkubwa, maisha yake yamekatishwa kwa ajili ya uroho wa wachache
Sikuwahi kukufahamu kabla lakini nimeumia....

Intelijensia ya kufuatilia wazalendo kisha kuwatesa na hatimaye kuwamaliza ni intelijensia ya hovyo kabisa.... JIRANI KACHEMKA MBAYA

cris.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bosi wake alipewa likizo ya lazima ,halafu yeye akapewa jukumu la bosi wake kisha naye kauwawa siku chache baadaye. Mbona muuaji yuko wazi kabisa? Wauaji wa huyu jamaa ni wale waliohusika na kumpa bosi wake likizo ya lazima. Kwa mtazamo mpana hawa watu walikuwa wanataka kuwatumia hawa wataalamu kuchakachua uchaguzi, inaonekana huyu bosi aligoma wakaona isiwe tabu ngoja tumlazimishe aende likizo halafu tumuweke huyu mwanzake huenda akakubaliana na sisi, jamaa naye baada ya kupewa akakataa kushawishiwa kibaya zaidi wamemlazimisha kwenda likizo ya kudumu. Ndg yetu huyu inaonekana alikuwa mzalendo na mbishi kweli kuwapa hawa jamaa ushirikiano. Usidhani alikatwa mkono akiwa marehemu hapana , huyu jamaa kila jeraha alilipata akiwa hai tena akiwa na fahamu zote. No mateso makali yaliyotokana na kutokuwa tayari kutoa siri fulani. Hapa kuna mikono ya wazi kabisa ya wenye uwezo wa kulazisha watu kwenda likizo.

Kanikumbusha jinsi ndg Zisti wa NEC yetu alivyotolewa kwenye idara yake ya ICT wiki kabla ya uchaguzi. Sijui kwanini wenye kuhamisha na kutoa likizo hawafanyi haya mapema.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Siasa kitu kibaya sana. Ndio maana wengne tunashukur kwa kila jambo liwe baya au zuri ili mradi mkono unaenda kinywani..

Hii ipo tangu enzi na enzi hata kabla hujazaliwa ..
Tangu enzi za akina Davi G
 
Back
Top Bottom