MADARAJA YA MABASI YALIYOPANGWA NA SUMATRA NA VIGEZO VYAKE

mikumiyetu

JF-Expert Member
Aug 16, 2016
1,311
944
MADARAJA YA MABASI YALIYOPANGWA NA SUMATRA NA VIGEZO VYAKE( baadhi tu vigezo, si vyote). 1.ORDINARY BUS (DARAJA LA KAWAIDA)
1.seats mbili upande mmoja na tatu upande mwingine
2.hakuna A/C
3.Hakuna huduma ya choo
4.Hakuna huduma ya vitafunwa na vinywaji laini
5.Hakuna mpangilio mzuri wa muda wa kuondoka na kufika
6.Hakuna mapazia
7.TV chini ya tatu

2.SEMI-LUXURY BUS (DARAJA LA KATI)
1.Mpangilio wa seats ni wa mbili kwa mbili
2.Ndani lazima kuwe kuna A/C
3.Huduma ya vinywaji laini na vitafunwa
4.Mpangilio na ufuatiliaji wa muda wa kuondoka na kufika
5.Mapazia safi katika madirisha
6.TV kuanzia NNE na kuendelea
7.Wahudumu nadhifu

3.LUXURY BUS (DARAJA LA KWANZA)
1.Mpangilio wa seats ni mbili kwa mbili au moja kwa mbili
2.Lazima kuwe na A/C
3.Huduma za vinywaji laini na vitafunwa muda wote
4.Uzingatiaji wa muda wa kufika na kuondoka
5.Mapazia safi muda na wakati wote wa safari
6.TV zaidi ya tano / kila seat
7.Mwendo mzuri na wa kistaarabu.
8.Wahudumu nadhifu muda wote wa safari
9.Huduma ya choo ndani ya basi pia bafu ikiwezekana.
10.Seats za kulala na nafasi ya kutosha kunyoosha miguu.
11.Huduma za ziada au binafsi ( basi kusimama njiani kwaajiri ya kufurahia hali ya hewa ya nje na mazingira mf.kitonga n.k)
#HUDUMABORA_SAFIRISALAMA
f9ee87ca31afd9a3936ad09f91fc4d32.jpg
 
Kuna mabasi yameandikwa semi luxury lakini ni malori.
Ndani seat zimebanwa, Hakuna AC wala soft drinks Yaani ni safari tu ya kukufikisha unakoenda.
Sumatra, sio kila basi LA yutong au zhongtong ni high class.
Kuna wengine Sawa tu na scania za zamani.
Hawa jamaa wanahitaji kufanya ukaguzi mpya WA mabasi
 
Tahmeed hao ndo wanaonekana kuwa makini na kazi yao achana na kimtikoooooo ,yaani bora upande daraja utawahi kufika ila sio hayo mabati.
 
Hakuna kitu hapo Mabasi yote yana fanana tu, nazani watu wanavutiwa na TV na kugawawai Soda.
Tatizo la haya mabasi ni moja
Siti zimebananishwa mno yaani ukitaka ku ejoy panda likiwa tupu hapo uta enjoy kwa kukunjua kiti. Ila kama liko full basi tarajia wa nyuma yako kukuambia unambana.
Hili ni kwa mabasi yote kuanzia Dar expres, Tahmeed Kilimanjaro na zinginezo.

Customer care ya hayo mabasi yanayo itwa kuxury nayo ni shida tupu hakuna Customer care ya maana.

Jaribuni kuangalia Magari ya Kenya mfano, Modern coast sit zake zimeachana sana sawa na wakina Taqwa na Spider, hawa jamaa Taqwa na Spider wanacho shindiwa ni hayo mambo yavyoo ila una enjoy sana safari make viti vinakunjuka kabisa.
 
Kuna mabasi yameandikwa semi luxury lakini ni malori.
Ndani seat zimebanwa, Hakuna AC wala soft drinks Yaani ni safari tu ya kukufikisha unakoenda.
Sumatra, sio kila basi LA yutong au zhongtong ni high class.
Kuna wengine Sawa tu na scania za zamani.
Hawa jamaa wanahitaji kufanya ukaguzi mpya WA mabasi
Hahahaaaaaa mbona Lori,bora umenisemea
 
Haya mabasi ni shida hasa wakiwa vituo vya njian na wana uroho wa pesa za ziada siti ya watu wawili mnajikuta mmekaa watu watatu hasa siti za nyuma ni mateso tupu.
 
Kwahyo daraja la kwanza wahudumu hawana ulazima wa kuwa nadhifu?,kweli maisha hayako fea
 
Kisbo wanagawa viroba kwa abiria

Yale mabasi yana injini za treni....yakifunguka dereva anaweza hata kupitiliza na kutokea mogadishu
 
Back
Top Bottom