Choosen Branch
Member
- Sep 4, 2024
- 51
- 36
Moja kwa moja kwenye mada.
Siku kadhaa zilizopita nilifanya safari kati Dodoma na Sumbawanga, nilitumia usafiri wa Bus la Kampuni ya AN Classic.
Pamoja na kwamba route hiyo AN Classic ndiyo Bus pekee linalofanya safari zake kupitia Itigi, Tabora na Mpanda imekuwa ni changamoto kwa kukumbana na huduma zisizoridhisha kabisa kutoka kwa Kondakta ya Kampuni hiyo.
Changamoto nilizozibaini kipindi cha safari
1. Kauli zisizoridhisha kutoka kwa Kondakta.
2. Bus kusimama simama vituo vingi ambavyo vingine halikustahili kusimama, hii ilisababisha safari ionekane ni ndefu sana na hata kuchelewa kufika kule mtu unapokwenda.
3. Bus halina Dustbin, kondakta hatimizi wajibu kuangalia mazingira ya usafi ndani ya Bus lake.
4. Bus kupakia abiria kupita uwezo wake, hasa lilipofika Mpanda, abiria zaidi ya kumi na tano walisimama.
5. Hali ya Bus nayo si ya kuridhisha sana kwani kuna wakati lilisimama kufanyiwa matengenezo.
Ushauri
1. Mmiliki wa Kampuni pamoja na Askari wa Usalama barabarani watupie macho ya karibu kwa Bus hili, hususani kwenye suala la kupakia abiria kupitiliza inapofika jioni hii ni hatari kwa usalama wa abiria. Nilipofuatilia nilibaini abiria waliopandia Mpanda waliaminishwa Bus litakapofika kila mtu atapata Seat yake ili hali Mawakala wa kukatisha ticket wakijua si abiria wote wanaoshuka Bus likifika Mpanda.
2. Pamoja na kwamba AN Classic ndiye mtoa huduma pekee kwa sasa katika route hii , lakini asijisahau kwa kutoa huduma mbovu bado abiria wanayo haki ya kupata huduma bora kabisa kama zilivyo route nyingine hapa nchini.
C. B