diana chumbikino
JF-Expert Member
- May 29, 2018
- 428
- 368
SERIKALI imetoa onyo kwa madalali na waendesha minada wote nchini, wanaoendesha shughuli hizo bila ya kuwa na leseni, kuwa kuanzia sasa atakayebainika hatua kali zitachuliwa dhidi yake. Madalali hao ni wa nyumba, viwanja, mahakama, usafiri na magari na kampuni zinazoendesha minada.
Pamoja na hayo, serikali imeagiza Ofisi ya Uhakiki wa Mali za Serikali, kukagua mali zote za serikali, zilizotaifishwa na zinazohitaji kufanyiwa minada, ili zinazohitaji kuuzwa ziuzwe na zinazohitaji kuingizwa mfumo ziingizwe, badala ya kuachwa na kuharibika. Hayo yamebainishwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Doto James wakati akizindua Mfumo wa Kieletroniki wa Utoaji wa Leseni za Udalali na Uendeshaji Minada, Dar es Salaam jana.
Alisema kwa muda mrefu sekta ya udalali na uendeshaji minada, imekuwa ikidharauliwa na wakati mwingine kuonekana ya kihuni kutokana na kuwa na wavamizi na makanjanja wengi, wanaoishushia hadhi sekta hiyo. “Nasema wazi hapa leo, udalali ni ajira kama zilivyo ajira nyingine na inatambulika kisheria. Ingawa Sheria ya Udalali ya mwaka 1928 ni ya zamani na imepitwa na wakati, iko kwenye mchakato wa kufanyiwa marekebisho ili iendane na wakati wa sasa,” alisema James.
Alisema haiwezekani kazi hiyo ya udalali, ikaachwa na kuishia kuonekana ya kitapeli kutokana na uwepo wa watu wengi wanaoiendesha wasiofuata sheria. “Sasa tutaangaza jicho kali zaidi hapa. Ujumbe wangu wa leo, tutakuwa wakali kuliko kawaida, yeyote tutakayembaini anafanya shughuli ya udalali na minada bila leseni, kitakachofuata si huruma, ni kushughulika na yeye tu,” alisisitiza.
Akielezea mfumo huo mpya wa utoaji leseni, alisema inawarahisishia madalali na waendesha minada, kuomba leseni kwa njia ya mtandao na kuzipata katika mikoa waliyopo, tofauti na zamani ambapo madalali na waendesha minada hao nchi nzima, walilazimika kwenda Dodoma kuomba vibali hivyo.
Alisema pia mfumo huo, umeunganishwa na Mfumo wa Serikali wa Malipo (GePG), ambapo muombaji atatakiwa kulipa ada ya leseni hizo, ambayo kwa mwaka ni Sh 150,000 kupitia mtandao na kisha kupatiwa taratibu za namna ya kupata leseni yake kupitia Ofisi ya Uhakiki Mali ya Mkoa husika.
Alisema baada ya kuzinduliwa mfumo huo kuanzia jana, maombi yote ya leseni za udalali na uendeshaji minada, yawasilishwe kupitia tovuti ya Wizara ya Fedha na Mipango ya www.mof.go.tz. Alitoa rai kwa taasisi za umma na sekta binafsi zinazohitaji huduma za udalali na minada, kutumia waendesha huduma hizo waliosajiliwa.
Soma
MJADALA: Nini kifanyike kuwadhibiti madalali wa nyumba, vyumba, mashamba, gari n.k?
Habari wakuu, Kama kichwa cha mada kinavyojieleza hapo juu, kumekuwa na changamoto kubwa katika suala zima la kupanga na kununua nyumba, mashamba, magari na kadhalika. Hawa watu wanaojulikana kama madalali au 'mtu wa kati' wamekuwa wakifanya maisha kuwa magumu kila siku yaani ni kero kwa...
www.jamiiforums.com
Madalali wa nyumba,viwanja wasajiliwe
Biashara ya udalali wa kuuza/kununua nyumba,viwanja nk inafanyika kienyeji na kiholela na watu wasio na usajili wowote. Serikali haiwafahamu. Hivyo hawalipi kodi. Biashara hii ya hovyo haiwapi usalama wa kisheria wananchi(legal protection). Aidha, hao madalali wasiojulikana kisheria...
www.jamiiforums.com