The Evil Genius
JF-Expert Member
- Mar 21, 2014
- 6,147
- 20,085
Madalali matapeli wa kupatana hawatanisahau.
Walitangaza nyumba kupitia kupatana, nikawatafta kesho yake wakanipeleka kwenye nyumba, wakaifungua nikaikagua kisha wakatengeneza mwenye nyumba feki nikamlipa kisha narudi kesho nakuta habari tofauti.
Kwanza najua utapeli wa aina hiyo upo ila kwa mazingira yale sikutilia mashaka kabisa jinsi walikua wamejipanga.
Baada ya kukuta mambo sio yenyewe nikawapigia sim hawakupokea, nikampigia aliejifanya mwenye nyumba hakupokea sim, nikajua nishaingizwa mjini.
Ila kitu nimewafanya watahadithiana wenyewe maana nimewafanyia umafia hawajawahi kuona, kwanza niliwaacha sikuwafta tena, miezi kadhaa wakajisahau, kwa ufupi ile chain yote iko polisi wiki sasa na kipigo kizito juu.
Tahadhari. Ukiwa na shida ya nyumba ukaona tangazo la dalali mahala popote ukimpigia sim alafu kabla hujaonana nae akakuunganisha na dalali mwingine kwa sababu yoyote ile basi achana na huyo dalali.
Pili, usilipe hela mtaani, yani mfano nyumba iko kimara alafu mwenye nyumba akakwambia mkutane Temeke, achana nao hao ni matapeli.
Tatu, hakikisha mkataba mnasainishana kwa mwenyekiti wa serikali za mtaa, mwenyekiti awe kama shahidi wako namba moja.
Huyu hapa ni dalali mmoja tapeli maarufu, kila siku anabadili majina kupatana, ila namba ni ile ile. Angalia hiyo namba kisha kua nao makini. Yeye alifanikiwa kutoroka ila bado anatafutwa, wenzake wako ndani. Ila bado naona anaweka matangazo kupatana. Ameishajulikana hadi nyumbani kwake ila kwa sasa hatuna shida nae maana wenzake tuko nao mahala salama. Kuweni makini na hiyo namba.