Madaktari wetu someni Alama za NYAKATI | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Madaktari wetu someni Alama za NYAKATI

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by yusufummaka, Jul 13, 2012.

 1. y

  yusufummaka Member

  #1
  Jul 13, 2012
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 30
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tume huru ziundwe kuchunguza nani kateka na kunyasanyasa Dr. Ulimboka hilo halina ubishi. Lakini pia tume huru iundwe kuchunguza madhara yaliyosababishwa na mgomo wa madaktari tangu walipoacha kuona wagonjwa OPD na Mawodini ili tujue uhusika wa kila daktati katika madhara yaliyowapata wananchi (yaani gharama, maumivu, complications, deaths, na usumbuvu) wakati wa mgomo.

  Ili kuzui migomo hii isitokee mara kwa mara ndugu na jamaa walioathirika wafungue kesi mahakamani kudai fidia toka kwa madaktari husika, serikali na mifuko ya bima za afya kwa kukosa matibabu siku za mgomo.

  Uzalishaji wa madaktari nchini hivi sasa umeongezeka kila mwaka hasa baada ya kuongezeka kwa vyuo vinavyotoa taaluma hii (MUHAS, KCMC, IMTU, KIU, HKMU, BUGANDO), hii inasababisha isiwe vigumu serikali kuwafukuza madakatari 200 wanaowatelekeza wagonjwa mahospitalini, madaktari wasiomheshimu waziri wao wa afya, waziri wao mkuu na hata amri ya mahakama. madaktari wa aina hii wamepoteza sifa na heshima ya kuitwa madakatari ndani ya jamii. Hata huko nje ya nchi pia kuna matatizo, hivyo kusema mtakwenda kufanya kazi huko ni upuuzi mtupu. Mawazo finyu yatakufanya uone kuwa huko nje ya nchi wanaruhusu madaktari wanaoacha kutibu wagonjwa kwa kudai posho zaidi. Nchi ina matatizo mengi sana kila secta sio CT scan na vitanda hospitalini pekee, pia tunakumbwa na njaa kila mara, baadhi ya sehemu hazina maji, umeme, barabara, nyumba za walimu. Ona wale polisi wanaokaa katika jengo la msimbazi police lilivyo chafu, mahakama hazina vitendea kazi, magereza mahabusu wamerundikana, n.k. Mnaposema mnagoma ili kuboresha mazingira ya kutolea huduma ni utoto mtupu. Maslahi yenu hayawataji hata wenzenu mnaoshirikiana nao katika kutoa tiba kama wafamasia, wauguzi, maabara, mortuary, cleaners, mionzi, n.k, hivi hao maisha yao ni mazuri kuliko ya kwenu? Au mna agenda nyingine?

  Mwezi wa nane wizara itapokea kakribani vijana 1000 wanaohitimu masomo ya udaktari kwenye vyuo vyetu nchini na kuanza mafunzo ya internship. Hivyo, zama zile zakujiona miungu watu ndani ya jamii zitakwisha. Tuungane tujenge Tanzania yenye neema kwa wafanyakazi na watu wote, sio neema kwa madaktari tu. Unapogoma wewe mfirikirie baba na mama yako, dada, babu, bibi, mpwa na shangazi wanapokwenda kwenye zahanati ya kijiji na kukuta watumishi wamegoma kudai maslahi. Mtalaanika, acheni maandamano yasio na kichwa wala miguu. Enzi zetu pia tulikuwa tunagoma lakini tulikuwa hatuachi wagonjwa, ila tulikuwa tunagoma kuelekea Ikulu tukiwatangunguliza mbele madakatari wenye busara kama prof. Shaba na wengine ili kuonana na waziri mkuu ama Rais kudai maslahi yetu.

  Serikali ichukue hatua kali dhidi ya vitendo hivi
   
 2. N

  Nakwetu Member

  #2
  Jul 13, 2012
  Joined: Apr 27, 2009
  Messages: 73
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni kweli nchi yetu ina mahitaji kibao. Pia ni ukweli nchi yetu ina UTAJIRI mwingi kiasi watu wa nje (Wahisani wanauliza kwa nini Tanzania ni maskini?) Nadhani jibu unalikumbuka " HATA MIMI SIJUI")
  Kila mfanyakazi atatetea HAKI yake mwenyewe, manesi, wafamasia n.k. Pili pamoja na shida zote Kwanini serikali haioni shida kuwalipa WABUNGE shs 10,000,000/= (Millioni kumi) kwa mwezi? Kwanini hawaoni shida ya kusafiri asubuhi na jioni na watu kama 50 kila safari? Kwa nini hawafanyi juhudi yeyote kukusanya kodi ipasavyo? Kodi za wafanyakazi ndio zinaendesha nchi.
  Je nikae KIMYA sababu wewe uko kimya?
  Serikali inazalisha madaktari wasiozidi 400 kwa mwaka, na sio Madaktari bigwa ni INTENS. Nao wakibobea Watagoma tu maana watajua haya yote. Mtafukuza kwa miaka kama 3 mfululizo ndio mtajua kuzalisha sio kazi, kazi kutunza.
   
 3. Avanti

  Avanti JF-Expert Member

  #3
  Jul 13, 2012
  Joined: Aug 24, 2010
  Messages: 1,209
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Umesema kweli kabisa, sisi wanasheria zamani tulikuwa deal lakini sasa tunauza sura tu, hatuna hata soko, kampuni za uwakili nazo zinaenda hadi wilayani, kazi kweli kweli!
   
 4. mwenyenchi

  mwenyenchi JF-Expert Member

  #4
  Jul 13, 2012
  Joined: Nov 10, 2011
  Messages: 655
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  inaonekana hujui unalosema,hakuna mwananchi mwenye haki ya kumdai dokta kwa kifo cha ndugu yake,bali waishtaki serekali, ni wajibu wa serekali kuhakikisha mwananchi wake anapata huduma bora za afya ,dokta kama mtu mwingine yeyote anahaki ya kutumia taaluma YAKE NA UZOEFU WAKE KUOKOA MAISHA YA WATU, LAKINI SI KWAKUMLAZIMISHA LAZIMA KUWE NA MAKUBALIANO KATI YA MWAJIRI (serekali) na dokta(mwajiriwa), kama unafikiri utamfukuza huyu umlete mwingine bila kuboresha vifaa na mazingira ya kazi basi hata huyo atakaye kuja hawezi kukuokoa bila dawa ,gloves, vipimo nk, so fikiria kabla hujaongea vitu vya ajabu
   
 5. Ndumbayeye

  Ndumbayeye JF-Expert Member

  #5
  Jul 13, 2012
  Joined: Jan 31, 2009
  Messages: 4,813
  Likes Received: 1,057
  Trophy Points: 280

  wenzenu kina ndungulile si wako kule wafateni kama ubunge unaona ni rahisi, mmegoma kwa sababu wabunge wanapata ,10,000,000?
   
 6. Ozzie

  Ozzie JF-Expert Member

  #6
  Jul 13, 2012
  Joined: Oct 9, 2007
  Messages: 3,234
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 135
  Heri mimi nisiyesema kuonesha ujinga wangu.
   
 7. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #7
  Jul 13, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Madaktari wa siku hizi umri mdogo naona wanakuwa wana akili kama wanafunzi wa vyuo vikuu bora waongezewe miaka ya kusoma hapo Muhimbili . Wanakuwa kama wale wanafunzi wa vyuoni ambao huitisha migomo isiyo na tija halafu wakisharudishwa makwao wakikaa wakiitwa tena viongozi wanatimuliwa wanafyata mikia. Fikirini kabla ya kutenda nyie madaktari maslahi.
   
 8. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #8
  Jul 13, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Ndumbayeye,

  Bora uwaambie hawa madaktari wachumia tumbo. Hamna aliyewakataza na wao kwenda kugombania ubunge mmbona Kangwalangwala yupo kule na ni daktari mwenzao? Wajipange upya madai yao ni rubbish tupu!
   
 9. Gwalihenzi

  Gwalihenzi JF-Expert Member

  #9
  Jul 13, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 5,117
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  Mawazo mgando kama haya ni hatari sana katika jamii, yaani badala ya kuwakabiri watawala wezi, mafisadi na wasio na upeo mkubwa wa kutatua matatizo ya nchi, wewe unamwaga pumba zako hapa kuwalaumu watu wanaodai haki zao za msingi. Kwa uelewa wako finyu unalidhika na matatizo yaliyosababishwa na wala rusha na mafisadi na kutaka waonewe huruma!! kafie mbali jinga la kujipendekeza wewe!
   
 10. Isalia

  Isalia JF-Expert Member

  #10
  Jul 13, 2012
  Joined: Nov 3, 2011
  Messages: 950
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 45
  Kama ningekuwa na uwezo madaktari wote walio goma wangeenda jela kwa ujinga wanaoufanya vipi umwache mgonjwa kitandani afe kisa maslahi na kuboreshewa mazingira ya kufanya kazi je unajuwa thamani ya uhai wa mtu tuache ushabiki wasiasa za kijinga hata kama ufisadi upo lakini bado haijawa kigezo bora hata na yeye alivyopata maumivu ya kuumwa ingawa sio jambo zuri alilofanyiwa. "HIVI NANI KALAZIMISHWA KUFANYA KAZI YA UDAKTARI"
   
 11. G

  Gilly Member

  #11
  Jul 13, 2012
  Joined: Aug 6, 2009
  Messages: 87
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Uko sahihi Mkuu. Nakumbuka mara moja mlimgomea Nyerere mambo ya National Service. Mlibeba bango kwamba akina Nyerere wanajilipa mishahara mikubwa na wanakomba Hazina. Nyerere alikubaliana nanyi kwamba huenda ni kweli na akaanza palepale kujikata yeye mwenyewe mshahara wake 6% kuchangia walimu (labda ndiko alikotokea) na mchango huo uliendelea hadi alipostaafu. Licha ya uamuzi huo, aliwatimua na baadaye akawarudisha. Hebu niambie sasa mambo yakoje? Ni ubabe kwa kwenda mbele! Ninachotaka kukueleza Mkuu ni kwamba huwezi kutumia mbinu za Nyerere za kuzima mgomo na huku huwezi kufanya kama Nyerere alivyofanya. Ya kukata mshahara wake kwanza! Kama Mkulu angekata mshahara wake kwa 10% halafu akaacha kusafirisafiri na kutulia nyumbani nani angedai nyongeza ya mshahara na marupurupu? Thubutu! Hata wawekezaji wasingefika kuwekeza nasi tungesalimika kunyonywa!
   
 12. a

  asakuta same JF-Expert Member

  #12
  Jul 13, 2012
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 15,065
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 0
  ndugu una mawazo na fikra mgando ,kama ni mtu mzima basi ni kituko a.k.a hovyo.huo mkataba wa kisheria kati ya daktari na mgonjwa unatoka wapi mpaka mgonjwa amfungulie kesi daktari kwa kumnyima huduma .ni jukumu la kikatiba la serikali kutoa hudoma bora za afya kwa wananchi wake.halafu unasema kuwafukuza madaktari 200 haitakuwa ngumu ,marekani(ratio yake ni daktari mmoja kwa wagonjwa chini ya 1000) yenyewe iliyopiga maendeleo leo hii haijajitosheleza kwa madktari sembuse sisi tanzania9ratio ni daktari 1 kwa wagonjwa zaidi ya 30000), achilia mbali Gharama walizotumia kuwasomeshea.sifa na heshima ya kuitwa daktari kwenye jamii yetu ni kutibu wagonjwa bila vifaa tiba ,vitendea kazi,madawa ,mazingira mazuri? au sifa ni daktari kutibu huku akiwa na njaa? nje ya nchi ni kweli kuna matatizo na changamoto zake ila huwezi ukalinganisha na hapa Tanzania ndiyo maana kuna idadi kubwa sana ya madaktari kutoka Tanzania wamesambaa nchi mbalimbali hapa Duniani zikiwemo nyinginezo nyingi tu hapa Afrika tena kusini mwa jangwa la sahara......kwenda nje kimaslahi siyo upuuzi mtupu kwani kiukweli huku kunamazingira bora ,vifaa tiba na maslahi bora zaidi tena mbali sana na tanzania ila inakuwa upuuzi kwa kukimbia changamoto zilizopo hapa nyumbani ,kwanini wasibakie hapa hapa kuishinikiza serikali kuboresha sekta ya afya kwa njia mbalimbali ikiwemo mgomo kama sasa hivi wanavyofanya.
  kuwemo kwa matatizo mengi kwenye nchi hii haiwezi kuwa hoja ya msingi kwa wao madaktari kudai haki zao na kuboreshwa kwa sekta ya afya. Matatizo mengi ya nchi hii ni kwasababu ya uongozi dhaifu ,rushwa iliyopitiliza ,bunge legelege ,upuuzi wa chama tawala ,zao la ufisadi uliopitiliza ,kudharaulika kwa ushauri wa wataalamu kwasababu ya ubinafsi wa viongozi wachache ,kukosekana kwa fikra huru miongoni mwa watanzania ,uoga na ubinafsi wa wasomi na mambo mengine mengi kama hayo.kwa uozo huo sioni ni kwanini madaktari wasipiganie wanachokiamini(hawawezi kutibu km waganga wa kienyeji kwa wewe kuhalalisha ukosefu wa vipimo na vifaa vya muhimu mahospitalini).
  hao wahitimu 1000 wa udaktari unaowategemea mwezi wa nane unaweza kuwainisha hapa ni kutoka chuo gani?Tanzani mpaka sasa na utitiri wote wa vyuo bado hatuna uwezo wa kutoa wahitimu wa MD 1000 kwa mwaka.
  kuhusu enzi zenu mlizokuwa mnagoma kwa namna yenu madaktari wa sasa hawawezi kutumia mbinu zile zile ,kutoka kwenye fikra zile zile halafu utegemee matokeo tofauti. These are new Methods from new minds and people for new generation and new results kwa akili zilizochoka kuongozwa na akili ndogo zenye fikra zile zile mgando.zama hizi ni zama za akili kubwa kuongoza ndogo na siyo vinginevyo ,kwahiyo endelea kupotosha wasiona uwezo wa kuchambua mambo.
   
 13. m

  mbwembwekali Member

  #13
  Jul 13, 2012
  Joined: Jul 4, 2012
  Messages: 22
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  poyoyo mwingine huyoooo! yaani wewe uende ukanunue wese la kuchakachuliwa BP petrol station halafu umfungulie mashtaka mfanyakazi anayekujazia wese? kweli huelewi jinsi ambavyo sekta ya afya ilivyo, wala dhamana ya afya ya mtanzania iko kwa nani kikatiba, ila naomba nikupe uhakika kuwa HAIKO KWA MADAKTARI! ndio maana ukijaribu kufungua kesi leo kuhusu ukosefu wa huduma za afya kesi haitaenda popote, kwa sababu utajikuta kumbe unaishtaki serikali! Na ndio maana hata kwenye mgomo wa February Naibu waziri wa afya alipoulizwa bungeni watu wangapi wamefariki kutikana na mgomo akapiga bla bla, mpaka leo hatujui ukweli kamili!
  vijana wote wanaosomea udaktari wako benet na movement zote zinazoendelea na madaktari, na wawakilishi wa huhudhuria na kuchangia katika vikao vyote vinavyofanyika, na mpaka sasa wanaunga mkono move inayofanywa na madaktari, kwani hakuna daktari yeyote, awe mwanafunzi ama daktari aliyefidhu mafunzo, asiyetaka kuboresha sekta ya afya. hao wanafunzi wanaenda kufanya kazi kwenye mazingira hayo hayo, na wanayafahamu fika, kwa sababu ndipo wanapofundishiwa udaktari, mahospitalini humo humo!
  KWA KIFUPI U R FULL OF ****!!!!!!!
  N.B. kama uzalishaji wa madaktari nchii ni 1000 kila mwaka inakuwaje seriali ina madaktari 1700 tu (wakiwemo na maspecialist)??? au ndio tunawazalishia watu wa nchi za nje? TAFAKARI, CHUKUA HATUA!!!!! USIWE ZUZU LA KUTUMWA TUMWA TUUUU!!!!
   
 14. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #14
  Jul 13, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Kuna mpango mkubwa wa kujenga chuo kikuu cha Muhimbili MUHAS kama chuo cha kujitegemea. Kikiisha tutakuwa tunamwaga tu madaktari wengine watazunguka soli zinaisha.
   
 15. m

  mbwembwekali Member

  #15
  Jul 13, 2012
  Joined: Jul 4, 2012
  Messages: 22
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ndio maana huna uwezo huo nyangau weeee! na kama hutaki kuwalazimisha si wachunie tu, mbona unamind wakigoma? si huwalazimishi kufanya kazi ya udaktari bwana?
   
 16. a

  asakuta same JF-Expert Member

  #16
  Jul 13, 2012
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 15,065
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 0
  huyo mgonjwa unayelalamika daktari amemuacha afe kwa mgomo ,madaktari kila siku wanawashuhudia wakifa kwa ukosefu wa dawa muhimu na vifaa tiba na ndiyo maana wamechoka. kama mgonjwa anataka oxygen kwahiyo daktari asipogoma atakuwa pale kumulizia oksijeni?
  wakeup mkuu ,au unatibiwa Appolo nn wewe? au daktari atamfunga vipi mgonjwa POP bila kuona X-ray ya mgonjwa.udaktari siyo uganga wa kienyeji upige ramli vipimo vya msingi na vifaa tiba vya msingi ni lazima viwepo ili mtu atumie taaluma yake kuokoa maisha.
   
 17. m

  mbwembwekali Member

  #17
  Jul 13, 2012
  Joined: Jul 4, 2012
  Messages: 22
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  tehe tehe tehe! hawa tu 1700 hamuwezi kuwalipa wala kuwajengea mazingira bora ya kazi, wala kuwapa vitendea kazi na madawa ya kuwapa wagonjwa! itakua kama baba anayezalisha mitoto miiingiiii halafu anaitafutia leseni za magari wakati gari alilo nalo halina usukani wala matairi, halafu liko kwenye kilima linarudi kinyume nyume!
   
 18. Sigma

  Sigma JF-Expert Member

  #18
  Jul 13, 2012
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 5,014
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Vijana 1000 wanahitimu udaktari....
  Mwache kutumia vijambio ndivyosivyo!
   
 19. m

  mbwembwekali Member

  #19
  Jul 13, 2012
  Joined: Jul 4, 2012
  Messages: 22
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  unaongelea watu waliosoma vyuo vikuu UTADHANI WEWE UNA ELIMU YA CHUO! MAFORM FOUR LEAVER BWANA!!!!
   
 20. N

  NG'ONGOVE Senior Member

  #20
  Jul 13, 2012
  Joined: Apr 28, 2012
  Messages: 151
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0


  NKwa wewe hakuna asubuhi. kweli ni bora uendelee kuota hizo ndoto
   
Loading...