Madaktari wauaji Mt. Meru Hospital arusha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Madaktari wauaji Mt. Meru Hospital arusha

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by MVUMBUZI, May 4, 2011.

 1. MVUMBUZI

  MVUMBUZI JF-Expert Member

  #1
  May 4, 2011
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 4,970
  Likes Received: 664
  Trophy Points: 280
  Baadhi ya madaktari na Manesi katika hospitali ya Mt .Meru Arusha wamethibitika kufanya kile ambacho watu wengi wamekuwa wakikilalamikia licha ya wao kuendelea kukana uovu huo. Imedhihirika kwamba baadhi ya madaktari wamekuwa wakitumia taaluma yao vibaya kwa kuharakisha vifo vya wagonjwa badala ya kuwapa huduma itakayo wawezesha kuongeza angalau siku kadhaa za kuishi na kufurahiwa na watoto, wake, waume, wazazi na hata ndugu zao.

  Uchunguzi uliofanywa siku tatu mfululizo katika wodi namba 6 ya wanaume umeshuhudia madaktari vijana wakishawishiwa na manesi wazoefu wa kuua (a.k.a watoa roho za watu) ili kuwanyima baadhi ya wagonjwa drip makusudi ili zibaki za kuuza kwa kisingizio kwamba ugonjwa wake hauwezi tibika na kwamba drip haimsadii chochote. Hali hii ilijidhihirisha pale mgonjwa mmoja aliyekuwa na tatizo la kumeza chakula alipoletwa na ndugu zake ili angalau apate drip ya Glucose zimwongezee nguvu huku wakitafuta utaratibu wa kumpeleka KCMC. Siku alipoletwa ndugu hawa waliwapa Manesi Shilingi 2000 na ndugu yao akawekewa drip tatu. Siku iliyofuata manesi hawakupewa hela kwa hiyo wakamwekea drip moja tu kwa masaa 24 ilihali wakijua kabisa mgonjwa huyu alikuwa anategemea drip kama chakula.
  Tatizo la mgonjwa lilikuwa ni chakula tu kwani alikuwa anaongea vizuri na kutembea mwenyewe bila shida yoyote. Nesi mmoja aliyekuwa zamu siku ya Jumanne saa sita na nusu mchana tarehe 3/5/2011 katika wodi 6 ya wanaume na Dk aitwaye Israeli Kasago wakaenda mbali na kumpa discharge kuliko wampe drip ambazo siyo mali yao bali zimegharamiwa na fedha za walipa kodi kwa ajili ya kuwasaidia watanzania.

  Mgonjwa alipoomba kuwekewa drip ili ake angalau apate nguvu kidogo yule nesi akamkataza Dr. Israeli Kasago na alipoulizwa kwa nini anafanya hivyo akasema huyu mgonjwa amechanganyikiwa. Niliposikia hivyo nilitaka kumzaba kofi au ngumi ila hekima ikanizuia.
  Wasifu wa huyu Nesi aliyekuwa zamu siku ya tarehe 3/5/2011 saa sita na nusu mchana hadi saa 7:20 ni Mnene mweupe aliyekuwa amevalia white . Sikufanikiwa kupata jina lake ila niliambiwa ni mmachame feki kwani wamachame ninavyowafahamu hawana roho mbaya hivyo.

  Ndugu zake wakamwomba angalau mgonjwa apewe drip wakati wanajipanga kifedha kumhamishia KCMC lakini huyu Dr. Akamsikiliza zaidi huyu Nesi muuaji badala ya kutumia taaluma yake na hivyo kwa makusudi wakam-discharge mgonjwa akafie mbali. Katika siku hiyo hiyo wagonjwa wengine watatu ambao pia hali zao zilikuwa mbaya wakaandikiwa discharge waondoke wodini kwa sababu tu Manesi hawapati chochote kutoka kwao.

  Katika hali kama hii sichelei kusema kwamba Wataalam hawa waliosoma kwa kodi za wagonjwa haohao na watanzania kwa ujumla balala ya kutumia taaluma yao kutetea uhai wa watanzania wamekuwa wakiharakisha mauti yao.
  Hii ni dhambi na ninajua vyama vyao vitawatetea ila ukweli utabakia kuwa ukweli kwa ninayooandika hapa nimeyashuhudia mimi mwenyewe na nathubutu kuwaita hawa “madaktari wauaji kwani kwa siku tatu za uchunguzi mambo waliokuwa wakiwafanyia wagonjwa yamethitisha kwamba ndiyo tabia yao.”.
   
 2. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #2
  May 4, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,798
  Likes Received: 157
  Trophy Points: 160
  Mahospitali yote ya Serikali na baadhi ya watu binafsi yameoza!
   
 3. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #3
  May 4, 2011
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280
  Duh pole sana lakini heading yako imekaa mkao mbaya unaweza kuirekebisha kidogo.
  Mt Meru Hospital wapo madaktari wazuri na wauungwana sana Dr Nkya,Dr Lyimo,Dr Makiago na wengine wengi sana.Kipindi cha nyuma alikuwepo marehemu Dr Mollel na Dr Solo hawa madaktari kila wakati walikuwa wamelewa hawakujali majukumu ya kazi zao kabisa laiti wangekuwa wameajiriwa kwenye taasisi za dini wangeshatimuliwa kazi siku nyingi.

  Mkuu Dr I Kasongo simfahamu vizuri ngoja nitaulizia habari zake lakini nashangaa Dr kupokea amri ya Nesi/Sister imekaa mkaa wa ajabu.
   
 4. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #4
  May 4, 2011
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
  dr Solo nilikuwa namfahamu sana, kuachilia mbali ulevi wake mbona kama alikuwa makini sana na kazi yake, ictoshe na docs wengi ni walevi...
   
 5. MVUMBUZI

  MVUMBUZI JF-Expert Member

  #5
  May 4, 2011
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 4,970
  Likes Received: 664
  Trophy Points: 280

  Mkuu sibadilishi heading na huy daktari ninaye msema anavaa miwani na ukitaka kumjua hebu fuatilia aliyekuwa zamu katika hiyo ward kwa masaa niliyotaja
   
 6. Uda

  Uda JF-Expert Member

  #6
  May 4, 2011
  Joined: Nov 27, 2010
  Messages: 730
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Hapa umewahukumu madaktari wote wa mt meru.i think kuna madaktari wanaofanya kazi yao vizuri.umeyapeleka malalamiko yako kwa incharge wa hospital?
  Hatuwezi kutoa maamuzi kwa ushahidi wa pande moja.
   
 7. Narubongo

  Narubongo JF-Expert Member

  #7
  May 4, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,922
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 135
  mimi niliandikiwa sindano hosptali ya wilaya bagamoyo, nikapanga msululu zamu yangu ilipofika nikazama ndani niliwakuta manurse 3, akanambia nichojoe nikafanya alichosema, kamata meza (masikini hata kitanda chumba cha sindano hakuna), nikakamata halafu akanambia "hapa hospitali hatuna sindanoo zimeisha lakini mimi ninazo za kwangu moja sh 300, lakini kama utapenda" jamani jamani jamani..
   
 8. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #8
  May 4, 2011
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,111
  Likes Received: 3,031
  Trophy Points: 280
  hebu wakwetu nifunue akili kidogo hapa.......doctor Solo ni marehemu?
   
 9. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #9
  May 4, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Mkuu sioni kama umetumia busara kumuita dr.israel kasago muuaji!nina hakika huwezi kuthibitisha hizo accusation zako la sivyo ungeenda mahakamani.unafahamu madhara ya kumuwekea mtu drip za glucose kwa saa 24??nadhani ulikuwa na jazba kama inavyojidhihirisha kwenye thread yako,ungepunguza hasira na kuongea na huyu dr.angekuelewesha kwa nini alikataa kumuwekea drip na kumdischarge.ina maana hiyo wd 6 ilikuwa na mgonjwa wako tu?wangapi wameuawa na hawa madaktari wa mt meru?
  Msipende kutumia uchache, unyonge,upole,maadili na umasikini wa madaktari au manesi kuwakandamiza.kama hajakutendea haki kuna njia muafaka za kufuata na sio kumchafua!naona utafurahi sana wananchi wakimtafuta huyu dr.israel na kumpiga mawe hadi kufa(naona hili ndio lengo lako)

  watanzania wengi tunaenda kwenye hospitali za serikali tukiwa na fikra(hisia) za kupata huduma mbovu kitu ambacho ni kinyume na wengi tunavyohisi.
   
 10. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #10
  May 4, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  alifariki mwaka jana i think november
   
 11. MVUMBUZI

  MVUMBUZI JF-Expert Member

  #11
  May 4, 2011
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 4,970
  Likes Received: 664
  Trophy Points: 280
  Ndugu hata kama huwezi fanya maamuzi kwa ushahidi wa upande mmoja huo ndio ukweli na mimi sikwenda kwa incharge kwa sababu madaktari wana tabia ya kulindana mno. Unakumbuka tukio la Muhimbili la mtu kufanyiwa upasuaji wa kichwa badala ya mguu na mwingine upasuaji wa mguu badala ya kichwa. Huu uzembe ulikuwa obvious na uliwashtua watanzania kiasi cha ku-question competence ya madaktari wetu lakini bado kulindana kulikuwa kwa hali ya juu mno.
   
 12. Sigma

  Sigma JF-Expert Member

  #12
  May 4, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 5,015
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  ujasiriamali kwa urefu wa kamba
   
 13. MVUMBUZI

  MVUMBUZI JF-Expert Member

  #13
  May 4, 2011
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 4,970
  Likes Received: 664
  Trophy Points: 280
  Mimi nami nafanya kazi kama yeye na huwezi fika ofisini kwangu ukanikuta nafanya ubabaishaji alioufanya kuandika discharge masaa 2 na kisha akaifungia ndani ya faili mpaka wenye mgonjwa waliokuwa tayari wamesubiri muda mrefu walipomwona hawamwoni wakamwita nesi aliyekuwa anatoa dawa na alipokwenda right away akaileta huku Dr. Israeli Kasago akiwa ameishia zake bila kujali kwamba wenye mgonjwa walikuwa wamekwisha subiri discharge kuanzia saa sita na nusu.
   
 14. MVUMBUZI

  MVUMBUZI JF-Expert Member

  #14
  May 4, 2011
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 4,970
  Likes Received: 664
  Trophy Points: 280

  Hakuna suala la hisia hapa ni tukio la ukweli na ambalo nimeshuhudia . cha kushangaza Dr. Mzima anaambiwa na Nesi/Sister asimpe mgonjwa drip hala anamsikiliza "what an incompetent doctor".
  Tatizo Manesi na baadhi ya Madokta wana dharau sana kwa wagonjwa na ndugu zao na imekuwa vigumu wagonjwa ku- react kwani hawana alternative na Nurses wanatumia opportunity hiyo kuwa mistreat binadamu wenzao kwa kuwataka wafe kabla ya muda wao.
   
 15. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #15
  May 4, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Alihamishiwa mapokezi baada ya Menejimenti kuona kuwa amekuwa mzigo kwa hospitali, na hakuacha hiyo tabia, nadhani baadaye akapata frustrations zilizopelekea kupoteza maisha!
   
 16. MVUMBUZI

  MVUMBUZI JF-Expert Member

  #16
  May 4, 2011
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 4,970
  Likes Received: 664
  Trophy Points: 280
  Mimi nami nafanya kazi kama yeye na huwezi fika ofisini kwangu ukanikuta nafanya ubabaishaji alioufanya kuandika discharge masaa 2 na kisha akaifungia ndani ya faili mpaka wenye mgonjwa waliokuwa tayari wamesubiri muda mrefu walipomwona hawamwoni wakamwita nesi aliyekuwa anatoa dawa na alipokwenda right away akaileta huku Dr. Israeli Kasago akiwa ameishia zake bila kujali kwamba wenye mgonjwa walikuwa wamekwisha subiri discharge kuanzia saa sita na nusu.
   
 17. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #17
  May 4, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Kumbuka pia tukio la MWANANYAMALA HOSPITALI mwaka huu miezi ya February, kulipatikana vichanga kama 10 vikiwa vimezikwa kwenye shimo 1, lakini hadi leo hakuna adhabu rasmi iliyotolewa kwa wahusika!
   
 18. Rweye

  Rweye JF-Expert Member

  #18
  May 4, 2011
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 15,025
  Likes Received: 3,051
  Trophy Points: 280
  Tushibishane,mbona hzo cases ni nyingi sana siku hizi,mfano mwingine ni wale manesi pale Teure (Mwanza) dhidi ya akina mama wajawazito,wanakuwa harrased sana,wanauliwa watoto wao,fuatilia mwaka jana/juzi utaona tu,ama nenda kwenye media wanazo recorded cases,huyu anasema eti uende kwa maofisa wa hospitali husika,nacheka sana! Tanzania kuna haki? nauliza tena,Tanzania kuna haki? ama huyu yeye anayo hyo haki ambayo hata mahakamani haiko,anayo????
   
 19. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #19
  May 4, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Mkuu, pole sana kwa yaliyokukuteni!
  Binafsi imenisikitisha sana.
  Jumapili nilimpeleka mgonjwa aliyekuwa amevunjika mguu hapo.
  Nikalipia 15,000 mapokezi kama gharama za kufungua faili na kulazwa..Cha ajabu daktari mmoja akaja akanivuta shati na kunipeleka kwa nesi mmoja sehemu ya faragha, akaniambia mbele ya nesi huyo kuwa nitoe elfu 5 za kumdungia sindano ya maumivu mgonjwa wangu, la sivyo sindano hiyo(diclofenac inj.) isingepatikana...nikacheka na kumpigia simu Dr ninayemfahamu, mambo yakaenda fasta!
  Wasiojua taratibu na wasio na ndugu wanaumizwa sana hospitali ile!
  Sidhani kama Mganga Mkuu Dr Toure anajua kinachoendelea hospitalini hapo, maana muda mwingi yuko Ofisini, Warsha, Kongamano, symposium, workshop, na kwenye LandCruiser la DFP(Hisani ya Merikani)...
   
 20. MVUMBUZI

  MVUMBUZI JF-Expert Member

  #20
  May 4, 2011
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 4,970
  Likes Received: 664
  Trophy Points: 280

  Ni kweli PJ nashangaa kuna mtu humu anadhubuti kutetea wauaji. Naandika haya si kwa jazba bali kwa uchungu na imenibidi nipunguze makali ya maneno kwani kwa mambo niliyoyaona wagonjwa wakifanyiwa ni dhahiri itafikia hatua wagonjwa au ndugu wa wagonjwa wata -react kwa kuwa- target individual Nurse au Doctor.

  Hakuna justification yoyote ya mtu kutumia taaluma yako kinyume na maadili ya kazi yake hasa ukizingatia kwamba ndio taaluma chache ambazo upohitimu unakula kiapo cha kulinda uhai na siri za mgonjwa. Iweje sasa mnageuka monster wa kuharakisha vifo vyao kwa uroho wa hela chache kama shilingi 2000 tu.
   
Loading...