Madaktari wapigwa stop kufanya kazi private | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Madaktari wapigwa stop kufanya kazi private

Discussion in 'JF Doctor' started by KUNANI PALE TGA, Jun 29, 2010.

 1. KUNANI PALE TGA

  KUNANI PALE TGA Senior Member

  #1
  Jun 29, 2010
  Joined: Feb 6, 2009
  Messages: 137
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  habari wakuu
  kumekucha,serikali imekuja na mpya nyingine,kuanzia sasa daktari wa serikali hamna ruhusa kufanya kazi private,unless uwe na kibali maalum.what is going on in this country?sasa mishahara ya madaktari yenyewe ni sawa na mfagiaji wa TRA,sasa kweli hapa tutaishi?kama wanataka hivyo mbona wasboreshe maslahi ya madaktari wa serikali,ili wasiende private?hii ndiyo kasi zaidi ya kuwafanya madaktari wawe maskini zaidi.na mwisho wote watakimbia nchi,tutibiwe na waganga wa kienyeji.
  oh god,bless this country,what and where and when did we go wrong that we have to suffer this life soo much?bora tu ulete tsunami tufe wote,ili yaishe,hii nchi haikaliki.
   
 2. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #2
  Jun 29, 2010
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Source Please hatutaki majungu
   
 3. Kibunago

  Kibunago JF-Expert Member

  #3
  Jun 29, 2010
  Joined: Jan 11, 2008
  Messages: 288
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  TGA ebu weka hapa huo waraka wa utumishi husika ndipo tujadili hili.

  Unajua uamuzi kama huo hauwezi kuishia tu hapo itabidi uwahusu na Walimu, Wahandisi, Wauguzi, Mabwana shamba, Wafamasia nk

  Ni jambo moja suala linapoanza kujadiliwa katika Wizara, Bungeni na hata katika vikao vingine vya kijamii na ni jambo jingine kabisa linapopitishwa na kutolewa waraka wa serikali!
   
 4. Askofu

  Askofu JF-Expert Member

  #4
  Jun 29, 2010
  Joined: Feb 14, 2009
  Messages: 1,668
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 133
  :clap2:
   
 5. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #5
  Jun 29, 2010
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Ndio maana tukaomba source muungwana na huo waraka kwasababu kama wakizuia MaDr wasifanye kazi katika private sectors na pia tunaomba wabunge wasifanye biashara pamoja na viongozi wa serikali, vilevile wale maprofessa wanaoenda kufundisha private university wapigwe marufuku, na vilevile wale akina John muhasibu (yaani wahasibu) wasifanye kazi za auditing katika private organisations otherwise ni kuwaonea madaktari kwa kutaka kujitafutia riziki.
   
 6. Nyunyu

  Nyunyu JF-Expert Member

  #6
  Jun 29, 2010
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 4,370
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  lete source mkuu!!!
   
 7. Nyunyu

  Nyunyu JF-Expert Member

  #7
  Jun 29, 2010
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 4,370
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Kweli mkuu!!! I second.

  Hii avatar yako mpya angalau angalau, ile iliyo pita ilikuwa na rangi mbaya sana!!!
   
 8. p

  p53 JF-Expert Member

  #8
  Jun 29, 2010
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 613
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Ku practice medicine bongo ni njaa tu na mwishowe ni kupokea virushwa vya buku mbili mbili.Labda ufanye siasa kama kina Sarungi lakini vinginevyo kuwa MD bongo ni maumivu tu.Wakati wenzetu ma MDs ni millionaires,sisi ma MD wanashindwa mshahara na wapiga deki wa TRA.Bongo MD ashindwa ku afford hata ka gari ka kijapan ka m5.Ndiyo maana wengi wanakimbia nchi.
   
 9. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #9
  Jun 29, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Mkuu, njoo u-practice bongo!!! CCD zinalipa sana mazee... hahahaaaa

  eniwei, waraka/agizo hautekelezeki!!!!
   
 10. p

  p53 JF-Expert Member

  #10
  Jun 29, 2010
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 613
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Mkuu De novo,mimi nimesomea sayansi ya mazingira,lakini kama ningekuwa MD ningeshakimbia bongo,manake nina mshkaji wangu yeye ni MD yuko muhimbili na ndiye anayenipa nyeti.
  Hiyo CCD ni mupya mzee,ndiyo nini tena hiyo?Kama huwezi weka public,niPM ili nimtonye na mshkaji nae labda itamlipa!
   
 11. MchunguZI

  MchunguZI JF-Expert Member

  #11
  Jun 29, 2010
  Joined: Jun 14, 2008
  Messages: 3,623
  Likes Received: 590
  Trophy Points: 280

  Ilikuwa ni hatua nzuri kuwaruhusu doctors kutafuta kipato cha ziada private lakini hata wao wanaharibu na kutumia ruhusa hiyo vibaya. Daktari anakuwa muhimbili asubuhi kama sehemu ya kutafuta wateja na baada ya saa moja anatoweka.

  Muhimbili akitafutwa haonekani. Tena mwingine ni profesa lakini kila siku yuko kwenye kibanda hapo kisutu anakiita dispensari akikusanya pesa za kuandika prescription. Nini maana ya ajira sasa?

  Lakini uamuzi huu ufutwe kwa wafanyakazi wote. sasa hivi tuna waalimu wako ktk ajira ya serikali lakini masaa yote wako private school!

  Huko vyuo Vikuu kuna waalimu wako ktk ratiba ya vyuo zaidi ya vitatu. Hapo kuna ubora?
   
 12. Q

  Qadhi JF-Expert Member

  #12
  Jun 29, 2010
  Joined: Oct 27, 2009
  Messages: 235
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  CCD=Chakula Cha Dokta
  I'm doing Medicine from my heart..I just Love it.
  Hali ilivyo Bongo,nitafanya my personal biznezz tu kuliko kuajiriwa na serikali na kuanza kupigana makelele.
   
 13. MchunguZI

  MchunguZI JF-Expert Member

  #13
  Jun 29, 2010
  Joined: Jun 14, 2008
  Messages: 3,623
  Likes Received: 590
  Trophy Points: 280
  Usidhani ni kwa madaktari tu, ni taaluma zote. Hapa tuwaache wansiasa tu ndo waishi maana huko BoT na TRA kuna familia zao.
   
 14. p

  p53 JF-Expert Member

  #14
  Jun 29, 2010
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 613
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Haya mkuu ujitahidi utafute mtaji,halafu ujitahidi pia upate na kadi ya ccm,halafu pia kuachana na zile code of ethics/integrity uanze kula madili na jamaa wa wizara...
  Mengine kamuulize yule Daktari bingwa wa moyo kutokea Texas,Ferdinand Masau.
  Kila la kheri yahke..
   
 15. p

  p53 JF-Expert Member

  #15
  Jun 29, 2010
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 613
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Mkuu dawa yake ni kuwalipa vizuri ili waache kuzuga serikalini au kukimbilia nje.Mtu huwa anafanya vizuri pale kwenye maslahi,ile notion ya wito imeshapitwa na wakati.Uwepo wa daktari hospitali tangia asubuhi hata mpaka majogoo hautasaidia kama hana moyo wa kufanya kazi.Ataishia kuandika jina la mgonjwa,umri kisha atamwambia akapime malaria.Kama kuna magonjwa mengine serious ambayo angeweza yagundua kwa kuchukua historia nzuri na physical exams,basi yatakuua kimyakimya ukadhani umerogwa au muda wa kugundulika,yatakuwa kwenye terminal stage tayari kwa kuua!
   
 16. m

  mti_mkavu Senior Member

  #16
  Jun 29, 2010
  Joined: Dec 23, 2008
  Messages: 116
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Bwana mkubwa,

  Ule mchezo wa daktari wa kumwandikia kipimo mgonjwa, na kumuelekeza kafanyie hospitali fulani(kwa mkyuba sijui wapi) halafu mnaenda kuvuta mshiko kulingana na wagonjwa mliyowaandikia waende huko toka hospitali za serikali mnazofanya sio mzuri ni njaa ya wazi. Pia mgonjwa unaenda hospitali ya serikali daktari anakuambia ukitaka kuniona vizuri njoo hospitali fulani au operesheni mazingira haya ya serikali hayafai. Kwa kweli hicho ndicho kinachonikera kwa madaktari wengi wa serikali, eti kipimo hiki kafanye hospitali fulani. nimeshuhudia wiki hii mtu kaambiwa picha hiyo ya X ray haifai ulipopigia nenda kafanyiwe sehemu fulani. Hata kama ni njaa sio kihivyo, uhai muhimu kwanza. Kwa nini msitafute namna ya kupata hela ya halali kama fast track n.k? Wagonjwa twaenda vile tunashida tu.

  Nawakilisha, na ninaunga mkono hoja ya serikali hamna kufanya sehemu mbili. Wafanye kama watakuwa waaminifu huko walipo serikalini.   
 17. p

  p53 JF-Expert Member

  #17
  Jun 29, 2010
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 613
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Mkuu hiyo inaweza kuwa siyo tu njaa ya Daktari bali pia kwa faida ya yako ili upatiwe tiba muafaka kulingana na tatizo ulilonalo.Siyo siri kuna ma technologists wazuri zaidi ya wengine.Matokeo ya laboratory tests na imaging tests yanaaathiriwa sawa na human/equipment imperfection.Sasa ili kupata vipimo sahihi ni lazima apatikane technologist mzuri na vifaa vizuri na ndiyo maana unaweza ambiwa kafanye kipimo fulani kwa fulani.
  Anyway inawezekana kukawa na mianya ya kupeana cha juu lakini ina faida sana kwa mgonjwa pia.
   
 18. M

  Mkandara Verified User

  #18
  Jun 29, 2010
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Mti mkavu,
  Nakuunga mkono sana.. Hali ilifikia kuwa mbaya sana kwa wagonjwa nchini na hakika wanaotetea Madaktari wa serikali kufanya kazi private wanashindwa kuelewa mfumo mzima ulivyokuwa mbovu. KJama hawa madaktari wanataka kuendesha biashara zao binafsi wafanye kazi huko full time na sio kuchukua wagonjwa wa hospital za serikali, kuwaghiribu kisha kuwalipisha gharama kubwa ktk Hospital zao binafsi ati ndiko kwenye huduma nzuri..The same person atakuwaje anahudumia vizuri kwake na siko alikoajiriwa?

  Hapa hawa Madaktari wanachezea maisha ya binadamu kabisa, na kulipwa mishahara midogo sio sababu ya kutoa huduma hafifu ktk hospital za serikali..,mshahara mdogo acha kazi fungua yako na ufanye kazi vizuri sio kwenda Muhimbili ili mradi upate kuiba wateja baada ya kazi. Swala la walimu na viongozi ni swala linaloweza kutazamwa pia lakini kwa uangalifu zaidi ya madaktari kwa sababu hawa madaktari wamefikia kucheza na Uhai wa watu.

  Hawakatazwi na mtu yeyote kufungua biashara zao binafsi na kutotegemea mshahara wa serikali lakini unapoajiriwa na serikali kisha muda mrefu unautumia ktk hospital yako hii inapunguza huduma za hospital za serikali na matokeo yake kila hospital ina pungukiwa madaktari. Yanayotokea leo hospitali za serikali hayatokani na ukosefu wa Madakari au madawa isipokuwa ni UFISADI wa Madaktari unaoharibu kabisa huduma nzima ya Afya nchini..

  Kwa uhakika huduma za Hospital za serikali zmepungua kuliko wakati wowote toka tupate Uhuru.. Wanawake wajawazito wanakugfa kuliko wakati wowote, Malaria, Kufia kikuu ni magonjwa yanayotibika lakini yanaua kuliko hata Ukimwi.

  Wanataka ushindani wafungue za kwao na watafute wateja na sii kuwachukua wale wasio na jinsi na kuwahadaa kwa maradhi yasiyoponyeka isipokuwa ktk hospital zao. Halafu sii kweli daktari anaweza kukutibu vizuri ktk zahanati yake kuliko Muhimbili hali kule hana vifaa vya kutosha, huu ni wizi mtupu na maranyingi wanaiba hata madawa na vifaa toka hospital za serikali.

  Ikiwa shule au mwalimu sii mzuri unaweza kuondoka sahule hiyo at least mhudumiwa ana choice lakini sii ktk Maradhi. Hao viongozi wetu kufanya biashara ni swala la muda tu...Hili linaangukia ktk miiko na maadili ya viongozi (Siasa) na kama sikosei JK tayari alikwisha piga marufuku viongozi wa serikali kujihusisha na Biashara.. Aliwaomba wachague aidha siasa au Biashara, hivyo kama unamjua Kiongozi yeyote ngazi ya juu serikalini akijihusisha na biashara nadhani bila shaka huyu kiongozi anavunja sheria..Mahakama ya miiko na maadili imeshafunguliwa hivyo ni swala la ku report tu mtuhumiwa.
   
 19. K

  Kazi Ndiyo Kipimo Cha Utu JF-Expert Member

  #19
  Jun 30, 2010
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 1,221
  Likes Received: 110
  Trophy Points: 160
  Kuna Madaktari waadilifu bado wanafanyakazi vizuri tu serikalini na huko kwenye viosk yaani hospitali binafsi lkn hawa ni wachache walio wengi wanafanya hospitali za serikali na hasa muhimbili ni sehemu ya kujengea jina na pakupatia wagonjwa na kuwahamishia kwenye viosiki.
   
 20. Q

  Qadhi JF-Expert Member

  #20
  Jun 30, 2010
  Joined: Oct 27, 2009
  Messages: 235
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Generally speaking,tulipofikia ni pabaya mno..hali ya maisha sijui au ni kuendekeza(maana sisi wengine hatujaanza kuingia rasmi kwenye misukosuko ya life)imetufanya tu develop roho ya paka kiasi cha kutothamini kabisa utu na maisha ya mtu.For me,ni bora nisichukue hiyo dhamana ya kuajiriwa na yoyote kuliko ku play around na life ya mtu,ni hatari sana.

  Nakumbuka lile sekeseke la mgomo wa ma daktari pale muhi2..dah,yaani jamaa walikuwa wanaenda kukusanya maiti tu wodini.Ni mtihani kwa kweli,mamlaka zote husika zinatakiwa kuwa makini,otherwise sisi vijana tuliopo mashuleni tunaanza kupata fikra za kushika njia kuliko kwenda kuingia kwenye lawama za kuua ndugu zetu
   
Loading...