Madaktari wanahitaji kuungwa mkono | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Madaktari wanahitaji kuungwa mkono

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by jogi, Feb 2, 2012.

 1. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #1
  Feb 2, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,799
  Trophy Points: 280
  Heshima wakuu, leo nimelazimika kusema kuhusu mgogoro wa ma-md. na serikali yetu. Mgomo wao 'binafsi' nauunga mkono bila kushawishiwa, iliripotiwa humu jamvini kuwa chadema walinyimwa ushirikiano stahiki toka kwa ma-Md. wanaogoma, i.e. kupewa kwa maandishi madai yao (medical doctors).

  Ikaelezwa pia kuwa ilikuwa ni hofu ya kuugeuza mgomo kuonekana wa kisiasa, naanza kuona ma-Md. wanaelekeza lawama kwa chadema kanakwamba hawakumbana waziri mkuu pinda kwenye maswali ya papo kwa papo, niwaulize wanataaluma ma-Md. Mlitaka chadema wajenge hoja nzito kwa vielelezo vya magazeti wakati vielelezo mnavihodhi?

  Kwa kuwa naamini pinda amejipanga kuwagaragaza wataalamu wetu, wajipangaje hawa ma-md. ku-win heart and mind za wananchi dhidi ya strategy za kifedhuli za kuwatumia wabunge wa ccm kina diana chilolo ku-divert hoja bungeni, kuzomea n.k

  CHADEMA japo hawaogopi kuzomewa bungeni wanapowatetea wananchi, ingewaongezea hoja yenye nguvu ya vielelezo, ambavyo mpaka sasa ni serikali tu ndiyo ina madai rasmi ya ma-Md. Madaktari,mkishikwa shikamaneni, ama mnahitaji tuwaungeje mkono?

  Tuna nia ya kuandamana kuishinikiza serikali ihakikishe tiba inapatikana mahospitalini, tutapigwa mabomu, virungu hata risasi, tutakapofikishwa hospitali baada ya kadhia hiyo inakuwaje nanyi mmewagomea hata wanaowaunga mkono?
   
Loading...