Tetesi: Madaktari walio Internship Kutolipwa Posho kuanzia Mwaka Huu

.... unafikiri kusoma medicine ni kama kusoma human resource , lazima serikali iweke motivation watu wasome hizo kozi nakuhakikishia watu watasoma na madegree yao watakaa na vyeti Gheto alaff watafte ajira mbadala
Kwa kauli hizi lazima wewe utakuwa ulikuwa unaingia na majuche, simbi, ama desa kwenye chumba cha mtihani. Aliyefaulu bila vikwazo hawezi kudharau fani ya mwingine...!
========
Tunahitaji madaktari wenye wito, walimu wenye wito, na kada nyingine hivyo hivyo. Ukiona huyo hataki kuumia kwa muda ili aokoe maisha ya mwingine ujue huyo hana wito.
 
Magu amuulize mkapa, na JK walipogoma interns hali ilikuwaje?! Intern doctors ndio wanaendesha hospitali hizo... Walileta madactari wao wa jeshi hawakutosha... Watangulizi wake walishindwa labda yeye ataweza ..

Naomba ibaki tetesi tu!
Hapana njiwa, wacha iwe kweli ili watanzania wote waisome namba vyema. Na ili wajue ccm ni ile ilee..
 
Hongera mkuu wa Kaya kwa maamuzi sahihi,hawa madaktari wanafunzi wanapewa fedha zisizo na idadi na wanazifuja kwa wanawake na starehe zisizo na tija kwa taifa
Ulitaka wazitumie wapi? Na vipi wanashindwa kutekeleza majukumu yao kwa sababu ya matumizi yao hao?
 
Kuna tetesi kuwa serikali imekusudia kufuta posho za madaktari wa mazoezi (Interns) kuanzia madaktari wanaotarajia kumaliza masomo yao mwaka huu. Katika utaratibu huo mpya madaktari wa mazoezi watapewa nyumba na chakula katika hospitali watakazoenda kufanyia kazi (Internship) lakini hawatakua na posho yoyote ya kujikimu.

Taarifa kutoka chanzo ndani ya serikali inasema lengo ni kubana matumizi, na kuokoa fedha nyingi ambazo zimekuwa zikitumika kuwalipa madaktari hao, ambazo hazilipiwi kodi.!
Motivation ina kuwa down!!!
 
Kuna mtu ametoa issue hapa kuwa Tanzania imekuwa nchi ya umbeya kweli hili linajidhihirisha na ni umbeya wa hali ya juu kwakweli. Maana habari haina kichwa wala miguu watu wanatoa povu kuchangia na kuanza kubashiri maisha ya interns utadhani limethibitishwa tuache umbeya jamaniiiiiiiiiiiiiiiiiii
 
Nchi haina pesa jamani mmeshaambiwa na samia vumilieni hadi hapo baadae mambo yatakapotengemaa
 
Mbona madactar wameandamwa sana kwani secta zingine hazipo? Mbona hatusikii wakasema wanajeshi?
 
..........five solid yrs, thn unakuja kupewa Chakula na Nyumba tuu, cjui matumizi mengine itakuaje........nawaza tuu kwa nguvu
 
Alafu naskia hata mishahara ya madaktari waliopo kazini imepunguzwa. Huenda siku zijazo watu wakaanza kukimbia hii taaluma.
naam taaluma hii itakosa watu kabisa na wale waliopo watakimbilia nje au private. na hapo si kuwa watanzania tumeacha kuumwa!. japo inawezekana kwa selekali hii, sidhani kama habari ya kweli!
 
Hizo nyumba zitatoka wapi? Hafu niko intern unipangie menu ya chakula kama mwanafunzi wa sekondari!! This is absolutely nonsense!
Kumbuka tunafanyiwa mambo ya hovyo kama haya after intense labour. Watu tumekomaa na pharmacology, physiology, medicine na surgery halafu anakuja mtu mmoja ambaye hata shule hana anasema "hakuna posho kwa interns!"
Kwa kweli inatia hasira.
 
naam taaluma hii itakosa watu kabisa na wale waliopo watakimbilia nje au private. na hapo si kuwa watanzania tumeacha kuumwa!. japo inawezekana kwa selekali hii, sidhani kama habari ya kweli!
Haya mambo eti ya kubana matumizi yatatufikisha pabaya. Mwenyezimungu apishe mbali
 
Back
Top Bottom