Tetesi: Madaktari walio Internship Kutolipwa Posho kuanzia Mwaka Huu

Bukanga

JF-Expert Member
Dec 13, 2010
2,857
1,936
Kuna tetesi kuwa serikali imekusudia kufuta posho za madaktari wa mazoezi (Interns) kuanzia madaktari wanaotarajia kumaliza masomo yao mwaka huu. Katika utaratibu huo mpya madaktari wa mazoezi watapewa nyumba na chakula katika hospitali watakazoenda kufanyia kazi (Internship) lakini hawatakua na posho yoyote ya kujikimu.

Taarifa kutoka chanzo ndani ya serikali inasema lengo ni kubana matumizi, na kuokoa fedha nyingi ambazo zimekuwa zikitumika kuwalipa madaktari hao, ambazo hazilipiwi kodi.!
 
nyumba na chakula!......technically,..kuwakalisha hosteli na msosi wa boarding school...After 5yrs of intense studying & concentration...:mad:
Alafu naskia hata mishahara ya madaktari waliopo kazini imepunguzwa. Huenda siku zijazo watu wakaanza kukimbia hii taaluma.
 
Alafu naskia hata mishahara ya madaktari waliopo kazini imepunguzwa. Huenda siku zijazo watu wakaanza kukimbia hii taaluma.
Mwanzo walikuwa wanakimbilia kwenye siasa huko nako magu kabana hakuna posho za ajabu, wao waisome namba huko huko tu
 
...Taarifa kutoka chanzo cha kuaminika ndani ya serikali inasema lengo ni kubana matumizi, na kuokoa fedha nyingii...!

Hicho chanzo kimesema lini habari hii itatolewa rasmi kwa Umma? Hili mbona janga sasa.
 
Mimi siamini kama anajua kuwa Kuna Mkurugenzi kateuliwa akiwa amefukuzwa chuo cha TIA kwa sababu ya uzembe na kukosa maadili. Huyo Bwana aligombea ubunge Kwa Kangi Lugora na amepangiwa kuwa mkurugenzi Wa Wilaya ya Hai.
Pia kuna wakurugenzi wa zamani ambao wamebakizwa ambao utendaji wao ni wa mashaka kuliko hata baadhi ya walioachwa.
 
Tangu mwaka jana walikuwa wanajadili hilo. Nahisi kwa sababu ya uchaguzi wakaona wasubiri kwanza.
 
Back
Top Bottom