Madaktari wakutana kujadili ndugu kumpiga Daktari!

meningitis

JF-Expert Member
Nov 17, 2010
8,394
4,748
Sakata la Daktari aliyepigwa huko Mtwara limechukua sura mpya baada ya madaktari kuamua kukutana Muhimbili.

Tusubiri yatakayojiri...

Chanzo: Ukurasa wa FB wa MAT
 
Wagonjwa na wanandugu wamepata kichwa au kiburi cha kuwapiga madaktari kutokana na matukio ya Mtwara pale Wazirikuu aliposema mtaje nitakulinda. Let us wait and see
Madaktari wanapaswa wajiulize iweje jamii ipoteze imani nao hadi kufikia hatua ya kupigwa? Inawezekana wao wenyewe wamejishushia heshima kwa kusifia mambo ya kipuuzi kama mgomo wa madaktari, inapotokea daktari anajitapa hadharani kuwa aliongoza mgomo wa madaktari bila kuangalia ni wangapi walidhurika kwenye huo mgomo basi ujue unachochea hasira zisizokuwa za msingi katika jamii.
 
Issue hizi zinatakiwa kuwa handled with care. Ni vyema kabisa watumishi kuwahudumia kwa weledi wananchi lakini sasa wananchi wasitake kufanya mambo ambayo yataleta shida. Hii inanikumbusha mwaka 1971 lilitolewa tamko la serikali kuwashirikisha watumishi katika maamuzi ya sehemu za kazi hasa viwanda na mashirika ya umma. Yakaanzishwa mabaraza ya wafanyakazi yakawa na nguvu kuliko menejimenti, wakuu wa mabaraza ya kazi (wengi wao wakiwa junior staff) wakajiona wana nguvu za kuamrisha menejimenti. Basi ikawa shida kuu. Someni kitabu cha Prof. Shivji mtajionea. Sasa wananchi wanataka kubeba madaraka yasiyo yao. Wao watumie njia muafaka za kuripoti kwa vyombo husika na siyo kujichukulia sheria mkononi.

Waliompiga Daktari wanastahili adhabu chini ya sheria za jinai na tortious liability.
 
Tusifike huko jamani hawa madr. tunawahitaji ni watu muhimu, wanafanya kazi ngumu sana japo na wao kama binadamu wana kasoro zao, ila kumpiga dr. kama mwizi na kuwaacha mafisadi wanatembea kifua mbele na kuwashangilia kwenye majukwaa sio haki kabsaaaa. Mungu anatuona.
 
Mazingira pia yamefanyika kisiasa kuwachonganisha madaktari (na wanataaluma wengine) na wananchi. Yaliyosababisha madaktari kugoma ndiyo tunaona leo serikali ikijaribu kuyashughulikia. Mambo ya kitaaluma yaachwe yafanyike kitaaluma. Sheria zipo zitumike kutatua matatizo yanayojitokeza kuliko kuchukua hatua ambazo zinachochea chuki.
 
Pale Bugando nilikuwa na mgonjwa akiwa katika hali mbaya! Daktari mmoja mfupi kama hizi Goroli nilipomfuata anisaidie akanijibu kuwa anajua wajibu wake!

Akajà baada ya masaa 2 mgonjwa akiwa tayari kafia mikononi mwangu!

Ashukuru Mungu ndugu na jamaa walinidaka, nilikuwa nimrushe nje kutoka gorofa ya 7!

Nashangaa nyie humu mnaongelea Daktari kuchapwa makofi! Hawa ni watu na kazi hizo has a kula in is he a kuzisomea! Maadam sasa ni watumishi hawanabudi kufanya kazi vizuri!

Tusipowachapia hapo Hospitali, wajue kabisa wakisababisha maafa tutawatwanga mitaani kama wahalifu wengine! Shwain
 
mafisadi yanajua namna ya kujisafisha, yananunua pombe wali na nyama, yanatoa sadaka makanisani na misikitini, yanabeba wananchi bure kwenye magari yao yanasomesha wasichana wasiokuwa na uwezo tena shule zao ni bora nchini.

Tatizo hawa hawana shukurani, hebu fikiria mtu anakwambia kamwite magufuli aje amhudumie mkeo wakati unaona yupo karibu kukata roho, unategemea nini kutoka kwa ndugu wa mgonjwa?
 
mazingira hayaboreshwi kwa kuua watu masikini, masuala ya siasa wawaachie wanasiasa na kama unaipenda siasa vua gloves panda jukwaani shika kipaza sauti.
 
Tusione daktari kama mtu pekee anayepaswa kuwajibika, halafu sisi tukawa kama malaika. Kila mtu mahala pake pa kazi anaweza asiwajibike na kuleta madhara. Tujichunguze.
 
Tweet za Umy Mwalimu

1. Ninakemea tabia hii
inayotaka kujengeka
dhidi ya Madaktari.
Nimewasiliana na RC
Mtwara ameshaagiza
wahusik wakamatwe

2. -Nitatoa
kauli ya Wizara juu ya
suala hili siku chache
zijazo. Hasira dhidi
madaktari haziwezi
kusaidia kuboresha
utoaji huduma
 
mafisadi yanajua namna ya kujisafisha, yananunua pombe wali na nyama, yanatoa sadaka makanisani na misikitini, yanabeba wananchi bure kwenye magari yao yanasomesha wasichana wasiokuwa na uwezo tena shule zao ni bora nchini.

Tatizo hawa hawana shukurani, hebu fikiria mtu anakwambia kamwite magufuli aje amhudumie mkeo wakati unaona yupo karibu kukata roho, unategemea nini kutoka kwa ndugu wa mgonjwa?
Na nyie wagonjwa mna kiherehere sana! Wewe unataka ukifika tu ukimbizwe ICU bila kujua kama kuna taratibu za kufuata!! Tuwaache madaktari wafanye kazi yao, sisi hatuna utaalam na hiyo kazi hivyo inabidi tuwe wapole!
 
Pale Bugando nilikuwa na mgonjwa akiwa katika hali mbaya! Daktari mmoja mfupi kama hizi Goroli nilipomfuata anisaidie akanijibu kuwa anajua wajibu wake!

Akajà baada ya masaa 2 mgonjwa akiwa tayari kafia mikononi mwangu!

Ashukuru Mungu ndugu na jamaa walinidaka, nilikuwa nimrushe nje kutoka gorofa ya 7!

Nashangaa nyie humu mnaongelea Daktari kuchapwa makofi! Hawa ni watu na kazi hizo has a kula in is he a kuzisomea! Maadam sasa ni watumishi hawanabudi kufanya kazi vizuri!

Tusipowachapia hapo Hospitali, wajue kabisa wakisababisha maafa tutawatwanga mitaani kama wahalifu wengine! Shwain
Huko alikoenda uliulizia kama alikutana na mgonjwa wa dharura???
Halafu usidhani madaktari wote utawapiga wakuangalie mkuu huu sio mwaka 47 unaweza kula jebs za kutosha kutoka kwa Dr hadi ushangae!
 
Madaktari wanapaswa wajiulize iweje jamii ipoteze imani nao hadi kufikia hatua ya kupigwa? Inawezekana wao wenyewe wamejishushia heshima kwa kusifia mambo ya kipuuzi kama mgomo wa madaktari, inapotokea daktari anajitapa hadharani kuwa aliongoza mgomo wa madaktari bila kuangalia ni wangapi walidhurika kwenye huo mgomo basi ujue unachochea hasira zisizokuwa za msingi katika jamii.
Kuna vitu vinatia hasira! Hebu fikiri sie tuliofiwa na ndugu zetu kipindi kile tunavyowamaindi hawa jamaa, nikikutanao chombingo wajiandae! Ama zao ama zangu!
 
Issue hizi zinatakiwa kuwa handled with care. Ni vyema kabisa watumishi kuwahudumia kwa weledi wananchi lakini sasa wananchi wasitake kufanya mambo ambayo yataleta shida. Hii inanikumbusha mwaka 1971 lilitolewa tamko la serikali kuwashirikisha watumishi katika maamuzi ya sehemu za kazi hasa viwanda na mashirika ya umma. Yakaanzishwa mabaraza ya wafanyakazi yakawa na nguvu kuliko menejimenti, wakuu wa mabaraza ya kazi (wengi wao wakiwa junior staff) wakajiona wana nguvu za kuamrisha menejimenti. Basi ikawa shida kuu. Someni kitabu cha Prof. Shivji mtajionea. Sasa wananchi wanataka kubeba madaraka yasiyo yao. Wao watumie njia muafaka za kuripoti kwa vyombo husika na siyo kujichukulia sheria mkononi.

Waliompiga Daktari wanastahili adhabu chini ya sheria za jinai na tortious liability.
Hasante mkuu kwakuliona hili, wengine naona wanalaumu ma Dr.
 
mazingira hayaboreshwi kwa kuua watu masikini, masuala ya siasa wawaachie wanasiasa na kama unaipenda siasa vua gloves panda jukwaani shika kipaza sauti.
Easily said...sijui kuua ni kupi, kwamba unamwona mgonjwa unayeweza kumtibu lakini vifaa vilivyopaswa kuwepo havipo kwa sababu ya uzembe wa wahusika havipo na lawama unatupiwa wewe! Au ni kuendelea kujifanya unatibu na kuwaekeza wahusika ambao wanadharau kwa sababu wakiugua wao huenda nje kutibiwa kwa fedaha hizo hizo ambazo wangepaswa kuzitumia kuboresha tiba hapa nyumbani? Tusixichongee taaluma tusaidie kupata suluhu.
 
Back
Top Bottom