Sasa si muache tu kazi serikalini mwende mkaendeleze hizo clinic zenu binafsi, badala ya kubaki huku na huku na hitimaye mnafanya kazi nusu nusu na utendaji kuonekana haufai. Make up your mind and quit from the government ili madaktari wengine waajiriwe. Udaktari siyo kazi ya kibabaishaji km siasa kwamba inategemeana na upepo unavyovuma. Udaktari unaendana na maadili, principles na masharti ya ajira. Kama unaamua kubaki serikalini basi fuata taratibu za ajira yako; unaweza kuona wagonjwa kwenye clinic yako on your private time, day off, baada ya kazi etc.
Kwa mshahara wa 1.3M hakuna atakayefanya kazi kwa ufanisi kama akizuiwa kufanya shughuli zingine.Utakuwa ni mzunguko wa kuajiri na kuacha kazi.Nakubaliana na wewe kwamba udaktari sio kazi ya kibabaishaji kwa hiyo maamuzi kuwahusu yasiwe ya kibabaishaji maana adhari zake ni za moja kwa moja na za haraka.
Nadhani tuwekeze kuhakikisha Hospital zina Madawa na Vifaa vya Matibabu.
Kusema ukweli toka nizaliwe sijawahi kufika Hospitali na kukosa Daktari au Muuguzi isipokuwa ninachelewa kumwona Tabibu au Daktari kutokana na wingi wa Wagonjwa ila kila Mara nakosa Dawa na Vipimo.