Madaktari wa Serikali wanaojiongezea kipato kwenye Hospitali binafsi kukiona...

..Dr. Chaula bana..eti anaipenda kazi yake ya udaktari....wakati yeye mwenyewe kateuliwa kuwa naibu katibu mkuu na hakukataa Na kusema angependa kubaki kuhudumia wagonjwa anaodai kuwajali...

...unafiki tu huu....anajua kabisa Dr. Chaula kuwa shida inayowafanya madaktari wa serikali kutafta kazi za ziada private ni maslahi(mishahara) duni....kama wangewalipa vema madaktari kungekuwa na haja gani wao kuhangaika huko private?

..yeye mwenyewe Dr. Chaula wakati anasoma kcmc hospital(internal medicine specialty) walikuwa wanafanya part time huko nje private... Ili kukidhi mahitaji,..leo anadanganya umma kwa vile amekalia mpini..unafiki tu...namtolea mfano yeye maana anadanganya wakati tupo tunaomjua tangu akiwa Chuo...

...mkitaka madaktari watulie kwenye mahospitali yenu walipeni vizuri.. Mengine yote blah blah za kisiasa tu...
Wakishapata vyeo wanasahau kila kitu .
 
Huo upuuzi unaoendelea ndio maana wanasheria waliamua kuonyesha true colors!!!! Walimu na madaktari msizubae
 
Serikali yaandaa kibano kwa madaktari wanaochepuka kwenye hospitali binafsi

Agosti 14, 2017

Serikali inatarajia kutoa mikataba ya uwajibikaji kwa waganga wakuu wa mikoa, wilaya na waganga wafawidhi wa hospitali zote nchini ifikapo mwezi ujao na ambayo itadhibiti wale wanaojikita zaidi katika hospitali binafsi kwa ajili ya kutafuta kipato cha ziada.

Kwa mujibu wa mikataba hiyo, daktari atakayeshindwa kufikia malengo atakuwa amejiachisha kazi mwenyewe.

Akizungumza na Nipashe juzi, Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Dk. Zainabu Chaula, alisema lengo la mikataba hiyo kwa waganga wakuu wa mikoa, wilaya na waganga wafawidhi wa hospitali ni kuboresha huduma za afya kwa kuwa haziridhishi.

“Huu mkataba utakuwa ni kwa kila mwaka, lakini sio wa kutishana na wala sio jambo jipya ni la kawaida… tunachotaka ni uwajibishaji,” alisema Dk. Chaula.

“Tunatamani uanze kutolewa Septemba mwaka huu (mwezi ujao), hivyo tutawaita, ili kuwajulisha kuhusiana na hili kwa kuwa kutakuwa na kikao mwezi huu.”

Dk. Chaula alisema kwa madaktari wanaofanya kazi katika vituo vingine vya afya huku majukumu yao waliyopangiwa na serikali wakiyaacha watadhibitiwa na mkataba huo.

“Hapo ndipo tutaondoana,” alisema Naibu Katibu Mkuu (Tamisemi) huyo. “Mtu anaacha kuona wagonjwa, anaenda kwenye kliniki yake (binafsi) anapata pesa na huku nako anadai fedha.”

“Mimi nimesomea udaktari (na) ninafanya kazi zangu kwa uadilifu, nilitamani wote wawe kama mimi.

“Sasa mtu akienda kinyume siwezi kumuacha.

“Tunachokitaka ni huduma za afya ziwe bora.”

Dk. Chaula alisema mkataba huo umeshaandaliwa kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, isipokuwa kuna baadhi ya vipengele vya kufanyia maboresho.

“System (mfumo) ya (wa) mkataba huo ni hivi… mimi nafanya kazi na Katibu Mkuu ndiye anayeniangalia utendaji wangu, Katibu Mkuu anakuwa na Waziri,” alisema Dk. Chaula.

“Mkurugenzi wa Tamisemi atakuwa karibu na waganga wakuu wa mikoa 26. Sasa mganga mkuu wa mikoa anaingia mkataba na waganga wakuu wa wilaya; hivyo kila mtu anamshika mwenzake.

“Hivyo mganga mkuu wa mkoa hawezi kukubali kuangushwa na mganga mkuu wa wilaya.

“Mfano waziri ameibua jambo kwenye halmashauri hapo anayewajibika ni mganga mkuu wa mkoa (kwamba) kwa nini hajawajibika?”

Alisema lengo la mkataba huo ni kila mmoja kutimiza wajibu wake bila kutumwa na kutakiwa kujitathmini mwenyewe.

“Mimi nimeteuliwa kwenye eneo la afya hivyo siridhiki na huduma, natamani ziwe nzuri (na), ili ziweze kuwa nzuri tukaona tupeane mikataba, ili kila mtu atimize majukumu yake,” alisema zaidi Dk. Chaula.

“Ndiyo maana tunataka kuwekeana malengo mahususi nikikuambia uniletee taarifa tarehe tano, ni lazima niipate tarehe tano. Usipoileta ina maana utakuwa una shida.
“Yaani nikitaka kitu fulani kikamilike kwa wakati na wewe hujafanya hivyo ina maana hujawajibika.

“Ifike wakati ukiona hujafanya vizuri katika nafasi yako uone hiyo nafasi hustahili, utajiengua mwenyewe… huko ndipo tunakoelekea.”

Dk. Chaula alisema kuwekwa kwa mkataba huo kutasaidia kupatikana kwa mabadiliko katika huduma za afya, ambayo kwa sasa hayawezi kuonekana kwa kuwa hali ilikuwa tete.

“Huu mkataba ni kila mwaka.

“Yaani kwenye mwaka wa fedha tunasimama na kuangalia je, umetimiza majukumu yako? Kama hujakamilisha majukumu yako utashuka, mwingine atapanda.”

MKATABA MWINGINE
Mganga Mkuu wa Mkoa mmoja ambaye hakutaka jina lake liandikwe gazetini alieleza Nipashe kuwa suala hilo la mkataba lilijadiliwa katika mkutano mkuu wa mwaka wa Waganga Wakuu wa Mikoa na Wilaya uliofanyika mkoani Dodoma mwezi uliopita.

Alisema wametakiwa kufanya kazi kwa malengo na kuonyesha mikakati ambayo wataitekeleza katika kipindi hicho, hivyo kama daktari hatofanya vizuri, uwezekano wa kupatiwa mkataba mwingine ni vigumu.

“Sisi kila siku tunatakiwa kufanya kazi kwa malengo,” alisema.

“Kwa mfano unasema mimi kwa safari hii nitahakikisha vituo kadhaa vinakamilika, nitahakikisha kutakuwa na upatikanaji wa dawa kwa asilimia 100, ndio malengo yenyewe ambayo tunajiwekea.”

Alisema mfumo huo umepitishwa katika mkutano huo kwa ajili ya watendaji wote – waganga wafawidhi wa hospitali, waganga wakuu wa wilaya pamoja na wa mikoa.
Alisema kwa sasa wanasubiri maelekezo ya serikali namna ambavyo watasaini mkataba huo.

“Tunangoja maelekezo namna ambavyo tutasaini (maana) kwa mfano mimi kama mganga mkuu wa mkoa, naingia mkataba na mganga mkuu wa wilaya,” alisema.

“Lengo la serikali ni kuona huduma za afya zinakuwa bora; yule atakayeshindwa kutekeleza mikakati yake hatapatiwa mkataba (mpya).”

Alisema jambo hilo ni nzuri, tatizo lipo kwa watendaji wavivu wanaoweza kuuchukia mfumo huo.

“Serikali ya sasa inataka tufanye kazi kwa kujituma na kuweka uzalendo mbele kwa wale wanaofanya kazi kwa kusuasua ama wale wenye mikataba na hospitali nyingine wanaweza kuuchukia huo mfumo ila kwa mimi sioni kama kuna tatizo,” alisema.


Chanzo: Nipashe

Mytake:
Ukiona mwenzio ananyolewa wewe tia maji , udaktari usio na mipaka kwaheri !

Natamani kusikia malengo yao..ningependa moja liwe, kuhakiksha hakuna mgonjwa hata mmoja anayekufa kwenye hospitali yako....
 
hili suala kama mengine hayahitaji matumizi ya vitisho bali utumiaji wa akili,wenzetu wamefanikiwa kwa hili kwanza kwa serikali kujipanga yaani ujenzi wa hospitali na kuwa na vifaa vya kisasa na upatikanaji mzuri wa dawa,then boresha maisha ya wataalaam wetu wa tiba,na muhimu zaidi kwenye kujiongezea extra income wenzetu wameruhisiwa kuwa na private hosp.ndani ya hospitali ya serikali yaani pale Amana hosp.

unatenga baadhi ya wodi kuwa ni private ones kwa hiyo wenye uwezo wa kulipia wanaruhusiwa kutibiwa hapo na hizi ward zinaendeshwa na madaktari na wataalam wengine ambao wameajiriwa pale,

ila wanawahudumia wateja wao kwa muda wao,na hii inasaidia kama kutatokea emergency case kwenye ile ya serikali,daktari ambaye angekuwa yupo mapumzikoni nyumbani anakuwa bado yupo kwenye maeneo yale yale,

kwa hiyo kupata msaada inakuwa rahisi,hili linawezekana kama utaratibu wa kuratibu ni mzuri na ni doctors wenyewe ndio wanaouratibu,serikali inapata huduma zake kwa madaktari hawa na upande wa pili umewawekea utaratibu wa kujiongezea kipato,its a win win situations.
 
Waongeze mshahara. Halafu wasitutishe hata tukiacha kazi serikalini tutafanya deal zetu, pole kwa wale madaktari wababaishaji lakini wenye shule zetu tunadunda. Yaani watu tusome degree miaka mitano na internship mwaka mmoja na residency miaka mitatu halafu tutishwe na watu wenye videgree vya miaka mitatu!!! Shame on you
Haya ni maneno ya kujifariji,hawa jamaa hawana vidigrii vya miaka mitatu tu,wana na bunduki pia,hamna ujanja wa kuwagomea.Kwanza walishawachonganisha na wananchi kwa hiyo hata mkifanyiwa kitu mbaya utawaona wananchi humu wanavyoshangilia.Halafu isitoshe anayewatisha ni daktari mwenzenu.Kaeni chonjo,huu si wakati wa masikhara.Kama unataka kazi fanya kazi,hutaki ondoka!Yote maisha
 
Yes. Nidhamu ya kazi iwepo. Hakuna tena kwenda kula leisure kwenye vijiwe vya kibiashara huku umeacha kwa muajiri wako. Kama mtu anaona huko anapata faida kubwa a stick huko.Muajiri anataka kazi zake zifanyike muda timilifu ili malengo yake yafikiwe.Malengo yatafikiwaje ikiwa kila muajiriwa atakata muda wa muajiri wake kwa lengo la kujiongezea kipato! Lini kipato kilitosha? Huwezi kuwatumikia mabwana wawili.
Nakubaliana na wewe mkuu 100%


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa si muache tu kazi serikalini mwende mkaendeleze hizo clinic zenu binafsi, badala ya kubaki huku na huku na hitimaye mnafanya kazi nusu nusu na utendaji kuonekana haufai. Make up your mind and quit from the government ili madaktari wengine waajiriwe. Udaktari siyo kazi ya kibabaishaji km siasa kwamba inategemeana na upepo unavyovuma. Udaktari unaendana na maadili, principles na masharti ya ajira. Kama unaamua kubaki serikalini basi fuata taratibu za ajira yako; unaweza kuona wagonjwa kwenye clinic yako on your private time, day off, baada ya kazi etc.
Nakubaliana na wewe mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Waongeze mshahara. Halafu wasitutishe hata tukiacha kazi serikalini tutafanya deal zetu, pole kwa wale madaktari wababaishaji lakini wenye shule zetu tunadunda. Yaani watu tusome degree miaka mitano na internship mwaka mmoja na residency miaka mitatu halafu tutishwe na watu wenye videgree vya miaka mitatu!!! Shame on you
By the way we doctors tulishaanza kujiongeza muda mrefu sana....
Wakituzingua tunawapiga CPZ au Haloperidol
 
Yaani wanaacha kuboresha vitendea kazi na mazingira mazuri ya watumishi kufanyia kazi wanataka kuhamisha goli, yani kinafikia kipindi MSD wamechelewa kuleta dawa DMO anaanza kuwajibishwa,

Wanaacha kuajiri watumishi wengi wa afya wanataka wawabane hawa waliopo
 
inabidi sasa hata wateule wa rais wawe "Professionals" na sio wa kujua "three R" mi nadhani tatizo ndio linaanzia hapo coz kila mmoja anataka kufurahisha mamlaka ya uteuzi na ndio maana katika kipindi cha uongozi huu matamko yamekua mengi kila mmoja na anavyojisikia kutoa ili boss aone kazi inafanyika.
hakuna marefu yasiyo na ncha itafikia kipindi watagusa wasiogusika waliamshe na tuliozoea kunung'unika chinichini tuliunge
 
Pathetic movement ya uongozi... sasa huyu mjinga anataka kulianzisha tena lile la Ulimboka pumbavu sana... Huatutaki vifo kwa uamuzi wa mpumbavu mmoja Raisi naomba amuondoshe huyu mjinga..

Huku Waziri na Raisi wakisema watu walime wajiongezee vipato na huku mjini hakuna mashamba mashambani hospital binafsi... Asaidie watu waongezwe mishahara
 
Haya ni maneno ya kujifariji,hawa jamaa hawana vidigrii vya miaka mitatu tu,wana na bunduki pia,hamna ujanja wa kuwagomea.Kwanza walishawachonganisha na wananchi kwa hiyo hata mkifanyiwa kitu mbaya utawaona wananchi humu wanavyoshangilia.Halafu isitoshe anayewatisha ni daktari mwenzenu.Kaeni chonjo,huu si wakati wa masikhara.Kama unataka kazi fanya kazi,hutaki ondoka!Yote maisha
Hao madaktari wanaosema wataacha waache utaona kama kazi watapata kazi wapi kuna madktari rafiki zangu wamekosa kazi Botwasa wamerudi hapa mmoja Physician na Medical doctor kwa sasa botswana kumefurika wamesomesha vya kutosha jamaa wanapiga part time mitaani usidanganyike.
 
Waongeze mshahara. Halafu wasitutishe hata tukiacha kazi serikalini tutafanya deal zetu, pole kwa wale madaktari wababaishaji lakini wenye shule zetu tunadunda. Yaani watu tusome degree miaka mitano na internship mwaka mmoja na residency miaka mitatu halafu tutishwe na watu wenye videgree vya miaka mitatu!!! Shame on you
Mkuu History remembers kings not souldiers
 
Back
Top Bottom