Madaktari wa Serikali wanaojiongezea kipato kwenye Hospitali binafsi kukiona...

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,641
218,091
Serikali yaandaa kibano kwa madaktari wanaochepuka kwenye hospitali binafsi

Agosti 14, 2017

Serikali inatarajia kutoa mikataba ya uwajibikaji kwa waganga wakuu wa mikoa, wilaya na waganga wafawidhi wa hospitali zote nchini ifikapo mwezi ujao na ambayo itadhibiti wale wanaojikita zaidi katika hospitali binafsi kwa ajili ya kutafuta kipato cha ziada.

Kwa mujibu wa mikataba hiyo, daktari atakayeshindwa kufikia malengo atakuwa amejiachisha kazi mwenyewe.

Akizungumza na Nipashe juzi, Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Dk. Zainabu Chaula, alisema lengo la mikataba hiyo kwa waganga wakuu wa mikoa, wilaya na waganga wafawidhi wa hospitali ni kuboresha huduma za afya kwa kuwa haziridhishi.

“Huu mkataba utakuwa ni kwa kila mwaka, lakini sio wa kutishana na wala sio jambo jipya ni la kawaida… tunachotaka ni uwajibishaji,” alisema Dk. Chaula.

“Tunatamani uanze kutolewa Septemba mwaka huu (mwezi ujao), hivyo tutawaita, ili kuwajulisha kuhusiana na hili kwa kuwa kutakuwa na kikao mwezi huu.”

Dk. Chaula alisema kwa madaktari wanaofanya kazi katika vituo vingine vya afya huku majukumu yao waliyopangiwa na serikali wakiyaacha watadhibitiwa na mkataba huo.

“Hapo ndipo tutaondoana,” alisema Naibu Katibu Mkuu (Tamisemi) huyo. “Mtu anaacha kuona wagonjwa, anaenda kwenye kliniki yake (binafsi) anapata pesa na huku nako anadai fedha.”

“Mimi nimesomea udaktari (na) ninafanya kazi zangu kwa uadilifu, nilitamani wote wawe kama mimi.

“Sasa mtu akienda kinyume siwezi kumuacha.

“Tunachokitaka ni huduma za afya ziwe bora.”

Dk. Chaula alisema mkataba huo umeshaandaliwa kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, isipokuwa kuna baadhi ya vipengele vya kufanyia maboresho.

“System (mfumo) ya (wa) mkataba huo ni hivi… mimi nafanya kazi na Katibu Mkuu ndiye anayeniangalia utendaji wangu, Katibu Mkuu anakuwa na Waziri,” alisema Dk. Chaula.

“Mkurugenzi wa Tamisemi atakuwa karibu na waganga wakuu wa mikoa 26. Sasa mganga mkuu wa mikoa anaingia mkataba na waganga wakuu wa wilaya; hivyo kila mtu anamshika mwenzake.

“Hivyo mganga mkuu wa mkoa hawezi kukubali kuangushwa na mganga mkuu wa wilaya.

“Mfano waziri ameibua jambo kwenye halmashauri hapo anayewajibika ni mganga mkuu wa mkoa (kwamba) kwa nini hajawajibika?”

Alisema lengo la mkataba huo ni kila mmoja kutimiza wajibu wake bila kutumwa na kutakiwa kujitathmini mwenyewe.

“Mimi nimeteuliwa kwenye eneo la afya hivyo siridhiki na huduma, natamani ziwe nzuri (na), ili ziweze kuwa nzuri tukaona tupeane mikataba, ili kila mtu atimize majukumu yake,” alisema zaidi Dk. Chaula.

“Ndiyo maana tunataka kuwekeana malengo mahususi nikikuambia uniletee taarifa tarehe tano, ni lazima niipate tarehe tano. Usipoileta ina maana utakuwa una shida.
“Yaani nikitaka kitu fulani kikamilike kwa wakati na wewe hujafanya hivyo ina maana hujawajibika.

“Ifike wakati ukiona hujafanya vizuri katika nafasi yako uone hiyo nafasi hustahili, utajiengua mwenyewe… huko ndipo tunakoelekea.”

Dk. Chaula alisema kuwekwa kwa mkataba huo kutasaidia kupatikana kwa mabadiliko katika huduma za afya, ambayo kwa sasa hayawezi kuonekana kwa kuwa hali ilikuwa tete.

“Huu mkataba ni kila mwaka.

“Yaani kwenye mwaka wa fedha tunasimama na kuangalia je, umetimiza majukumu yako? Kama hujakamilisha majukumu yako utashuka, mwingine atapanda.”

MKATABA MWINGINE
Mganga Mkuu wa Mkoa mmoja ambaye hakutaka jina lake liandikwe gazetini alieleza Nipashe kuwa suala hilo la mkataba lilijadiliwa katika mkutano mkuu wa mwaka wa Waganga Wakuu wa Mikoa na Wilaya uliofanyika mkoani Dodoma mwezi uliopita.

Alisema wametakiwa kufanya kazi kwa malengo na kuonyesha mikakati ambayo wataitekeleza katika kipindi hicho, hivyo kama daktari hatofanya vizuri, uwezekano wa kupatiwa mkataba mwingine ni vigumu.

“Sisi kila siku tunatakiwa kufanya kazi kwa malengo,” alisema.

“Kwa mfano unasema mimi kwa safari hii nitahakikisha vituo kadhaa vinakamilika, nitahakikisha kutakuwa na upatikanaji wa dawa kwa asilimia 100, ndio malengo yenyewe ambayo tunajiwekea.”

Alisema mfumo huo umepitishwa katika mkutano huo kwa ajili ya watendaji wote – waganga wafawidhi wa hospitali, waganga wakuu wa wilaya pamoja na wa mikoa.
Alisema kwa sasa wanasubiri maelekezo ya serikali namna ambavyo watasaini mkataba huo.

“Tunangoja maelekezo namna ambavyo tutasaini (maana) kwa mfano mimi kama mganga mkuu wa mkoa, naingia mkataba na mganga mkuu wa wilaya,” alisema.

“Lengo la serikali ni kuona huduma za afya zinakuwa bora; yule atakayeshindwa kutekeleza mikakati yake hatapatiwa mkataba (mpya).”

Alisema jambo hilo ni nzuri, tatizo lipo kwa watendaji wavivu wanaoweza kuuchukia mfumo huo.

“Serikali ya sasa inataka tufanye kazi kwa kujituma na kuweka uzalendo mbele kwa wale wanaofanya kazi kwa kusuasua ama wale wenye mikataba na hospitali nyingine wanaweza kuuchukia huo mfumo ila kwa mimi sioni kama kuna tatizo,” alisema.

Chanzo: Nipashe

Mytake:
Ukiona mwenzio ananyolewa wewe tia maji , udaktari usio na mipaka kwaheri !
 
2020 watajuta hawa watu!!

Wao wanawaza kubana watumishi lakini hawajali kabisa maslahi na haki za watumishi.

Viongozi wa awamu hii wamejisahau kupita kiasi mpaka wanashangaza!!

Wanawaza tija wanasahau motivation!!

Pathetic!!
 
Waongeze mshahara. Halafu wasitutishe hata tukiacha kazi serikalini tutafanya deal zetu, pole kwa wale madaktari wababaishaji lakini wenye shule zetu tunadunda. Yaani watu tusome degree miaka mitano na internship mwaka mmoja na residency miaka mitatu halafu tutishwe na watu wenye videgree vya miaka mitatu!!! Shame on you
 
That is an unfortunate lay rhetoric.
Kati ya kada zisizopaswa kuchezewa ni udaktari.

Its so easy kwa daktari aliye in high demand nchi nyingine, kufungasha virago na kuondoka just like that.

Hatujasahau lile sakata la daktari aliyeamua kuacha kazi baada ya kubugudhiwa na kiongozi wa kisiasa unprofessionally nafikiri huko Singida.

Busara katika kuongoza professionals ni muhimu.
 
Hawatajuta wala nini....
Maneno hayo yamesemwa sana toka 1995 mpaka leo hamna lolote la maana lililowahi kujutisha watu...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Waongeze mshahara. Halafu wasitutishe hata tukiacha kazi serikalini tutafanya deal zetu, pole kwa wale madaktari wababaishaji lakini wenye shule zetu tunadunda. Yaani watu tusome degree miaka mitano na internship mwaka mmoja na residency miaka mitatu halafu tutishwe na watu wenye videgree vya miaka mitatu!!! Shame on you
Dr chaula amesema " mtu anaacha kuona wagonjwa anaenda kwenye kliniki yake, anapata pesa na huku nako anadai pesa , hapo ndio tutaondoana "
 
Waongeze mshahara. Halafu wasitutishe hata tukiacha kazi serikalini tutafanya deal zetu, pole kwa wale madaktari wababaishaji lakini wenye shule zetu tunadunda. Yaani watu tusome degree miaka mitano na internship mwaka mmoja na residency miaka mitatu halafu tutishwe na watu wenye videgree vya miaka mitatu!!! Shame on you
Kwani wingi wa miaka kusoma degree kunaifanya degree iwe na thamani? Si kweli!
Thamani ya degree ni ule umuhimu wake tu wa namna inavyosaidia jamii.
Kwa taarifa tu degree muhimu kuliko zote ni ile ya kusomea usalama wa taifa!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
That is an unfortunate lay rhetoric.
Kati ya kada zisizopaswa kuchezewa ni udaktari.

Its so easy kwa daktari aliye in high demand nchi nyingine, kufungasha virago na kuondoka just like that.

Hatujasahau lile sakata la daktari aliyeamua kuacha kazi baada ya kubugudhiwa na kiongozi wa kisiasa unprofessionally nafikiri huko Singida.

Busara katika kuongoza professionals ni muhimu.
Tunavyopiga kelele mara zote mnatupuuza kwa vile hamjaguswa , sasa kwenye hili ndio mnakurupuka ! , hakuna aliye salama ndani na nje ya ccm .
 
"Kwa serikali hii kila kiongozi anajiona yeye ni kambale mradi ana masharubu" mwache afanye anayotaka lakini akumbuke cheo ni dhamana siku akitumbuliwa na kurudi kwenye ward ndiyo atayakumbuka maamuzi yake
 
Kwani wingi wa miaka kusoma degree kunaifanya degree iwe na thamani? Si kweli!
Thamani ya degree ni ule umuhimu wake tu wa namna inavyosaidia jamii.
Kwa taarifa tu degree muhimu kuliko zote ni ile ya kusomea usalama wa taifa!

Sent using Jamii Forums mobile app
Usalama wa kung'oa kucha na kuteka akina Roma ? Kwanini unadharau elimu ya watu wengine , nani kakupa kiburi hicho ?
 
Back
Top Bottom