Huu ni mchanyato wa habari!!Habari wana JF, hivi karibuni tumeona tukio moja likitokea huko Mtwara la Kusimamishwa Daktari mmoja aliyehusika katika kuomba rushwa kutoka kwa mgonjwa aliyetakiwa kufanyiwa upasuaji.
Japo ushahidi ni mgumu wa mazingira ya hiyo rushwa, ni ukweli usio na kificho kuwa Wahudumu wa afya walio wengi wamekuwa si waaminifu tena wasiokuwa na chembe ya huruma kwa binadamu wenzao kiasi cha kutojali uhai wa wagonjwa wanaowahudumia.
Tukio la Mtwara limefuatana na matukio mawili ya kusikitisha yaliyotokea katika jiji la Mwanza, wilaya ya Nyamagana kwenye hospitali ya wilaya ya Nyamagana (Butimba) na hospitali ya mkoa ya Sekou Toure.
Likitangulia la hospitali ya Butimba, mama mmoja alijifungulia chooni watoto mapacha na wakafariki kwa kile kilichodaiwa ni uzembe wa manesi waliokuwa wakimtolea kauli chafu mjamzito huyo kuwa awaite Majaliwa na Magufuri waje wamhudumie.
Tukio jingine lililofuatia ni kufariki kwa mama na watoto wake mapacha katika hospitali ya mkoa (Sekou Toure) kwa kucheleweshwa kuongezwa damu.
Kutokana na matukio hayo, kuna manesi na madaktari wametiwa nguvuni kutokana na kasi iliyopo sasa ya kurejesha nidhamu na uwajibikaji katika utumishi wa umma. Sasa Madaktari wamefanya mgomo katika hospitali ya Butimba kwa madai wanaogopa usalama wa kazi yao kwa kuwa wao hawawezi kuzuia kifo kwa mgonjwa pale muda wake unapokuwa umefika.
Mheshimiwa Rais, sichelei kusema hawa madaktari wanataka kutunishiana misuli na serikali yako kwa kile kilichotokea Mtwara. Kwanini Wananchi wote wanaokumbwa na masahibu haya kutoka kwa wahudumu wa afya katika maelezo yao wanaambiwa wawaite Majaliwa na Magufuli wawahudumie?
Mheshimiwa watumie vijana wako wa TISS wakupe taarifa kamili ili ujue utapambana vipi na udhalimu wa baadhi ya watumishi wa afya ambao wanafikiri kuwa wao ni bora katika jamii kuliko watu wengine wakisahau kuwa wao pia ni product ya mwalimu, hivyo tunaishi kwa kutegemeana.
Upuuzi upi mkuu? Uhuru wa mawazo ni upuuzi? Au hayo yanayotokea ni upuuzi? Maybe wewe unatibiwa nje ya nchi kadhia wanazozipata watanzania mahospitalini huzijui! Kama upo katika sekta hiyo pia tunaweza kujadili.mpuuzi sana wewe unatafuta sifa kama huyo unayeimwita
Lakini mkuu matatizo ya rushwa na kauli mbovu kutoka kwa wahudumu wa afya zimeanza muda mrefu. Hakuna utafiti ambao umefanywa kuhusu rushwa ukaiweka pembeni sekta ya afya.Ninacho kiona ni uhusiano mbovu kati ya wahudumu wa afya na jamii wanayo itumikia yahani uhusiano mbovu kama ule wa jeshi la polisi na jamii, nani a naye wachonganisha? jibu ni wazi Siasa mbovu.
Hueleweki unaongelea madaktari au manesi au wahudumu wa afyaKwa nini umeuita mchanyato wa habari mkuu?
Yaani*Ninacho kiona ni uhusiano mbovu kati ya wahudumu wa afya na jamii wanayo itumikia yahani uhusiano mbovu kama ule wa jeshi la polisi na jamii, nani a naye wachonganisha? jibu ni wazi Siasa mbovu.
Wala usijisumbue!! BTW kazoea kuonea vidagaa na anaogopa mapapa...aanze na yule waziri wake february...Habari wana JF, hivi karibuni tumeona tukio moja likitokea huko Mtwara la Kusimamishwa Daktari mmoja aliyehusika katika kuomba rushwa kutoka kwa mgonjwa aliyetakiwa kufanyiwa upasuaji.
Japo ushahidi ni mgumu wa mazingira ya hiyo rushwa, ni ukweli usio na kificho kuwa Wahudumu wa afya walio wengi wamekuwa si waaminifu tena wasiokuwa na chembe ya huruma kwa binadamu wenzao kiasi cha kutojali uhai wa wagonjwa wanaowahudumia.
Tukio la Mtwara limefuatana na matukio mawili ya kusikitisha yaliyotokea katika jiji la Mwanza, wilaya ya Nyamagana kwenye hospitali ya wilaya ya Nyamagana (Butimba) na hospitali ya mkoa ya Sekou Toure.
Likitangulia la hospitali ya Butimba, mama mmoja alijifungulia chooni watoto mapacha na wakafariki kwa kile kilichodaiwa ni uzembe wa manesi waliokuwa wakimtolea kauli chafu mjamzito huyo kuwa awaite Majaliwa na Magufuri waje wamhudumie.
Tukio jingine lililofuatia ni kufariki kwa mama na watoto wake mapacha katika hospitali ya mkoa (Sekou Toure) kwa kucheleweshwa kuongezwa damu.
Kutokana na matukio hayo, kuna manesi na madaktari wametiwa nguvuni kutokana na kasi iliyopo sasa ya kurejesha nidhamu na uwajibikaji katika utumishi wa umma. Sasa Madaktari wamefanya mgomo katika hospitali ya Butimba kwa madai wanaogopa usalama wa kazi yao kwa kuwa wao hawawezi kuzuia kifo kwa mgonjwa pale muda wake unapokuwa umefika.
Mheshimiwa Rais, sichelei kusema hawa madaktari wanataka kutunishiana misuli na serikali yako kwa kile kilichotokea Mtwara. Kwanini Wananchi wote wanaokumbwa na masahibu haya kutoka kwa wahudumu wa afya katika maelezo yao wanaambiwa wawaite Majaliwa na Magufuli wawahudumie?
Mheshimiwa watumie vijana wako wa TISS wakupe taarifa kamili ili ujue utapambana vipi na udhalimu wa baadhi ya watumishi wa afya ambao wanafikiri kuwa wao ni bora katika jamii kuliko watu wengine wakisahau kuwa wao pia ni product ya mwalimu, hivyo tunaishi kwa kutegemeana.
Ukifuatilia uhusiano kuwa mbovu kati ya watumishi wa afya na jamii Mwanza, chanzo ni hao watumishi wa afya kutokana na rushwa iliyokithiri. Waulize watu wa Mwanza wakuambie hali rushwa ilivyo mahospitalini.Yaani*
Kweli mkuu jamii inawadharau hao madaktari kama Mwanza nilisikia Dr.fulani akisema kuna uhusiano mbaya kati ya jamii na watumishi wa hosp.hiyo
Sijui tunapoelekea katika hili
Ndugu inaonekana kama kuna mass mobilization dhidi yao sasa, nani kamobilize jamii dhidi ya watu wa afya?......... sikatai kuwa afya kuna matatizo, nadhani njia wanazo zitumia kuwajibisha watovu wa nidhamu ndo zenye matatizo .Lakini mkuu matatizo ya rushwa na kauli mbovu kutoka kwa wahudumu wa afya zimeanza muda mrefu. Hakuna utafiti ambao umefanywa kuhusu rushwa ukaiweka pembeni sekta ya afya.