Madaktari na Miandiko Yao!

Etugrul Bey

JF-Expert Member
Aug 6, 2020
3,520
6,503
Around saa tatu usiku napata bahati ya kutembelea duka Moja la madawa,nyie wenyewe mnaita Sijui famasi kitu kama hicho.

Nimesema bahati coz si kila Mtu hupata nafasi hiyo, Kama unaona sio bahati, ebu nikuulize mara ya mwisho kwenda famasi ni lini?

Anyways Kama nilienda kununua dawa zangu binafsi au za mtu mwingi haupaswi kujua we pigia mstari hapo kisha twende kwenye kusudio la huu uzi.

Mara Pap! Kaingia Mrembo kama wale wa curb Verde kama wewe huwa unaangalia afcon pale Ivory Coast nadhan umeshanielewa.

Akatoa bandiko lake toka Kwa daktari, la haula! Mhudumu kasoma dawa ya kwanza ya pili ile anaenda ya tatu aah wapi! Mwandiko hausomeki, kilichoendelea ni binti kurudi tena kwa daktari ili mambo yawe sawa.

Eti madaktari kuna mahusiano gani ya taaluma yenu na miandiko yenu isiyosomeka Kwa Baadhi yenu?

Jamani wakinijibu naomba mnitag.

Ni hayo tu!
 
Wakati Mwingine Ni ngumu kuelewa kwanini Dr anaandika vile, ila umuhimu wake ni mkubwa Mno .
ukiniuliza mm mtazamo wangu, naona kama ndio wanafanya ndio utambulisho wao, lkn wajue wanawaumiza watu wengi kwa swaga zao mbovu
 
ukiniuliza mm mtazamo wangu, naona kama ndio wanafanya ndio utambulisho wao, lkn wajue wanawaumiza watu wengi kwa swaga zao mbovu
Uko sahihi lakini pia wanafanya hivo kuepusha vifo vinavotokana na wagonjwa kukalili dawa na kwenda kununua dawa famasi kwa mazoea
 
Uko sahihi lakini pia wanafanya hivo kuepusha vifo vinavotokana na wagonjwa kukalili dawa na kwenda kununua dawa famasi kwa mazoea
Hapana, ukweli ni kwamba ma Dr wanaona wagonjwa wengi mno kuliko inavyotakiwa kwahiyo kutokana na idadi kubwa ya wagonjwa wanajikutaka wanaandika haraka haraka na automatically mwandiko unabadilika na kuwa haueleweki kwa watu wa kawaida japo wenyewe kwa wenyewe wakisoma wanafahamu.
 
Jibu sahihi
 
Shida ipo kwa huyo mtu wa famasi
1:huenda hana taaluma ya ufamasia na ni kama amewekwa na akapewa ujuzi wa dawa mbili tatu auze(nina ushahidi na hilo) kumshikia bosi mfamasia anayefanya mahali pengine.

Kwa taaluma ya watu wa afya kuna vifupi ambavyo wao wakiandika moja kwa moja wanaelewana kwamba wamemaanisha nini hata kwa dawa ni vivo hivyo.

Kwahiyo tupate uhakika wa elimu ya mfamasia kwanza.
 
Back
Top Bottom