Bodi na Mabaraza walia na suala la mmomonyoko wa maadili katika Sekta ya Afya

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Bodi na Mabaraza ya kitaaluma ya sekta ya afya yamekutana kuandaa mpango mkakati wa pamoja wa kuweza kudhibiti mmomonyoko wa maadili kwa watoa huduma za afya nchini hali ambayo hivi sasa imeongezeka kwa kiwango kikubwa kwa wanataaluma wengi.

Hayo yameelezwa leo na Msajili wa Baraza la Wauguzi na Wakunga ambaye pia ni Mwenyekiti wa Wasajili wa Bodi na Mabaraza ya kitaaluma Bi. Agnes Mtawa wakati wa kikao cha pamoja kilichofanyika kwenye ukumbi wa wizara jijini Dodoma

Mtawa amesema hivi sasa maadili, uwajibikaji na utendaji wa kazi kwa watumishi wa sekta ya afya umekua ukishuka kila siku hivyo sasa wanajipanga kuweza kufanya kazi kwa pamoja ili kuweza kuinua hali ya utoaji huduma za afya kwenye Vituo vya Afya.

“Hali ilivyo sasa kumekua na ongezeko la mmomonyoko wa maadili ambao unaathiri utoaji wa huduma zetu za afya kwahiyo tumekaa na kupanga maeneo yote ambayo tunahusika na kutekeleza kwa pamoja ili kuhakikisha wanataaluma wetu wanafanya kazi kwa kufuata maadili,taratibu,kanuni na sheria za taaluma zetu pamoja na wananchi wanapata huduma bora”.Alisema.

Aidha, amesema kuwa katika maeneo ya kazi wamepanga kuweka mfumo madhubuti ambao utawawezesha kama bodi na mabaraza kuweza kuwapata taarifa kwa wale ambao wamekuwa wanafanya kazi nje ya maadili na kuchukua hatua stahiki kwenye ngazi zote za utumishi.

Kwa upande wa wauguzi,Mtawa amesema kweli kumekuwa na malalamiko ambayo wananchi wamekuwa wakiwalalamikia wauguzi na wakunga kutokana na baadhi yao kutotekeleza majukumu yao ipasavyo.

“lakini pia malalamiko mengine ni wananchi kutokujua mipaka ya utekelezaji wa majukumu ya wauguzi na wakunga hivyo kwa kuweka mfumo wa ushirikiano utaweza kuhakikisha wanapatia ufumbuzi malalamiko hayo”.

Hata hivyo amesema sheria zote za mabaraza ya kitaaluma yanatambua viongozi wasimamizi katika ngazi zote za vituo vya afya hivyo wanawajengea uwezo ili kutoa elimu na kuwakumbusha wataalam masuala ya maadili na uwajibikaji kule wanapotoa huduma pamoja na kuchukua hatua kwa wale ambao wanaendeleza vitendo ambavyo vinawakera wanachi.

Naye Msajili Baraza la Famasi Bi. Elizabeth Shekalaghe amesema kuwa upande wa dawa bado kumekuwa na tazizo kutokana na kutowajibika kwa wanataaluma na kutozingatia maadili wakati wa kutekeleza majukumu yao.

“Sisi tunategemewa na wananchi katika kuhakikisha kwamba wanapata dawa,ni kosa kwa mwanataluma kutoa dawa kwa mgonjwa ambayo imekwisha muda wake”.

Shekalaghe amesema Sheria ya Famasi, Sura 311 ikisomwa pamoja na Kanuni za Maadili na Utendaji wa Taaluma za Mwaka 2020,zimeweka bayana kuwa mwanataaluma anapokutwa na kosa la kutowajibika na Baraza kuthibitisha hilo anastahili kusimamishwa katika utendaji na ikibidi kufutiwa usajili pamoja na leseni yake.

“Niwaeleze wafamasia na fundi dawa sanifu na wasaidizi kwamba unapokosa wakati unapofanya kazi kwenye sekta ya umma haiwezekani ukaenda kwenye sekta binafsi ukidhani kuwa ni mbadala kwa sababu Baraza la Famasi ni chombo cha Serikali na unapokosa huwezi kufanya kazi sehemu nyingine hivyo ni bora mkawajibika na kuzingatia maadili katika maeneo yenu ya kazi kwani hatutosita kumchukulia hatua yeyote atakayeenda kinyume na maadili na taratibu zilizowekwa”Alisisitiza

Aidha, amesisitiza kufanya kazi kwa kushirikiana na kuwataka watendaji kwenye halmashauri kuibua hoja na kutoa taarifa za ukiukwaji ili matatizo hayo yaweze kushughulikiwa kuliko kuwasubiri viongozi kwenda huko chini.

Wakati huo huo Msajili wa Baraza la Madaktari Tanganyika Dkt. David Mzava amewataka madaktari wote nchini kufuata taratibu za utoaji huduma bora kwa wagonjwa kwani wananchi wamekuwa wakilalamika sana katika eneo hilo kwani mgonjwa anapotoka kwa daktari anatakiwa awe amefarijika.

Dkt. Mzava amesema kutomshirikisha mgonjwa ipasavyo ni kukiuka miiko na viapo vya taaluma vya utoaji huduma za afya kwenye taaluma hii.

Pia amewata madaktari kuzingatia utaratibu wa kuhakikisha wanamtaarifu mgonjwa ana tatizo gani ili mgonjwa aweze kuchukua hatua kwenye kuongoza nini afanyiwe kwenye matibabu anayofanyiwa.

“Ni vyema mwana taaluma kuzingatia kuwaona wagonjwa wako kwa wakati ili kujua kama mgonjwa ana dharura. Hivi sasa wagonjwa wengi wanaonwa na mwana taaluma mwenye ngazi ya chini muda wote hii hapana kwani kuna ngazi mbalimbali za kumuona mgonjwa”.Alisisitiza
 
Wazingatie pia maslahi ya watumishi maana ni kilio kila kona haiwezekani mtumishi Analipwa lakini Tatu kwa miaka saba no increment bodi ya nimkopo 8-15 % halafu utegemee huyo mtumishi Kuwa ataishi bila kuomba rushwa kwa wagonjwa
 
Back
Top Bottom