Madaktari walikumbana na nini Ikulu? vinara wa mgomo hatujawasikia tena, hata kwii hakuna.
Mlitaka kuonana na Mkulu nyinyi wenyewe, vipi? tupeni mkasa wa huko, maana hii si kawaida. Kuna fununu kuwa wale vinara wote hawataki hata uongozi wa hicho chama cha madaktari, kwa ufupi wameufyata.
Madai yenu hayajatimizwa, na kuufyata mmeufyata na nna uhakika mmekoma na hamtorudia tena, labda waje viongozi wengine ambao hawajui yaliyowafanya muufyate. Kwi kwi kwi Teh teh teh.
Cheza na dola nyinyi.
Chezea kikwete wao?
Mwanadiplomasia huyo!
Unawakejeli wakati walikuwa wanakutetea wewe ili upate kupata vipimo vyote pindi uendapo hospitali za serikali au wewe ndiwe mwimbili ndo airport yako then matibabu India
Taarifa rasmi ni kwamba hadi sasa vikao vya majadiliano kati ya madaktari na team ya serikali bado vinaendelea na taarifa ya majadiliano hayo itatolewa kwa madaktari na wadau wengine muda si mrefu.Ni lazima ieleweke kwamba hakuna vitisho wala kunyamazishwa kwa viongozi wa madktari.Lengo letu ni kutafuta suluhu ya kudumu itakayopelekea mgogoro kama huu usijirudie tena na kama ukitokea basi utatuliwe mapema bila kuathiri wagonjwa kama ilivyotokea.
DR.EDWIN CHITAGE
MJUMBE WA KAMATI YA MAJADILIANO.
Walikuwa si watetezi bali wauwaji, huwezi cheza na maisha ya wagonjwa eti kwa kuwa unatetea maslahi ya wagonjwa wengine. Huo ni punguani wa hali ya juu. Walichokipanda wamekivuna na nnajivuna kuwa na Rais kama Kikwete ambae amewafanya waufyate.
Nna uhakika wamekoma na hawatothubutu tena.
Naona umekuja na lugha mpya. Kama kweli ulikuwepo Ikulu, umejifunza namna ya kuongea. Hakuna aliyeongelea vitisho humu. Tunasema mmekoma, mmeufyata na hamta rudia tena.
Jee, ni wangapi kati yenu waliojiuzulu baada ya kutoka Ikulu? Mbona hilo hausemi?
IQ ya madaktari ni level ya juu sana kwako. Unataka wakupe ripoti kwani wewe pia daktari? Endelea kufikiria kwa kutumia masaburi.Walikuwa si watetezi bali wauwaji, huwezi cheza na maisha ya wagonjwa eti kwa kuwa unatetea maslahi ya wagonjwa wengine. Huo ni punguani wa hali ya juu. Walichokipanda wamekivuna na nnajivuna kuwa na Rais kama Kikwete ambae amewafanya waufyate.
Nna uhakika wamekoma na hawatothubutu tena.
Ribosome Nakuunga mkono mkuu kabla ya kuonana na Raisi yalikuwa yanapiga mikelele ili kutafuta sympathy ya wananchi miuwaji mikubwa ile imechimbwa mkwara karibu ijiharishie kwa woga sasa hivi inapiga mzingo kwa maslahi yaleyale wanataka mkuu asisafiri ili hiyo hela walipwe wao? Mbona walivyokutana na waziri mkuu walituambia yaliojiri kwenye mkutano. hawana lolote hawa wanaiba dawa na vifaa wanapeleka kwenye dispensary zao sasa wanataka Serikali iongeze vifaa na madawa ili waibe zaidi mafisadi ya roho za watu mkwara mmoja tu kimya kwi kwi kwi kwi kwi!!!!!!1
Nahisi we jamaa ni mgonjwa kabisa na ninadhani ulizaliwa na Mtindio wa ubongo (Cerebral Palsy. Hivi sijui ueleweshwe vipi ili uelewe kwamba hapa hakuna cha kutishwa wala kuufyata, kilichofanyika ni busara tu madaktari kurudi kazini huku majadiliano yakiendelea. Na hii ni kutokana na rais kuonesha nia ya kutatua mgogoro huu, ambao wasaidizi wake walikuwa wanacheza danadana.
Nadhani kuwadhihaki na kuwatukana haitatusaidia, walijaribu kutuonesha kuna matatizo na hayo matatizo yako katika sekta zote nchini. nachukulia huko kama tu kutukana wakunga.............
Nadhani waliowahi kuhitaji huduma za hospitali zetu wanajua hali ilivyo mule ndani, bado kuna upungufu na wao kukaa kimya si kwamba shida zetu zimekwisha. Bado mazingira yao ya kazi si mazuri na ukihitaji huduma utaipata kwa tabu.
Kwa bahati nzuri wengi kwenye hili jamvi tuna fursa ya kupata hizo huduma za afya kwa urahisi iwe kwa kulipia au kwa wale walio katika mifumo ya bima za afya, ila kwa wengi wa watanzanania bado hali ni ngumu, na haielekei kubadilika siku za karibuni.