Ikulu na dr. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ikulu na dr.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Abdillahjr, Oct 22, 2012.

 1. Abdillahjr

  Abdillahjr JF-Expert Member

  #1
  Oct 22, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 694
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  KUNA watu wanne hapa. Wote wanazungumzia jambo lile lile. Lakini watatu wanaofanya kazi ofisi moja wanapingana na mmoja. Tumwamini nani?
  Upande mmoja yupo Dk. Stephen Ulimboka, ambaye alitekwa na kuteswa vibaya, akanusurika kifo. Anasema anamkumbuka aliyemteka. Amemtaja.
  Akasisitiza kwamba amemjua muda mrefu. Akasema mtu huyo anafanya kazi Ikulu. Maana yake ni kwamba Dk. Ulimboka hakutekwa na wahuni.


  Upande mwingine wapo Rais Jakaya Kikwete, Katibu Mkuu Kiongozi wa Ikulu, Ombeni Sefue, na Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Salva Rweyemamu, ambao kwa nyakati tofauti wamesema na kusisitiza kwamba Ikulu haikuhusika na utekaji huo.
  Sasa wananchi wamwamini nani? Nani anasema ukweli? Nani mwongo?


  Lakini tunaweza kuanzia pale alipoishia Dk. Ulimboka, maana yeye ndiye aliyefanyiwa kitendo kibaya. Kwa kuwa ndiye aliyeumizwa, jitihada zozote za kujua ukweli unaohusu tukio lake zitaanzia kwenye kauli yake.
  Hata ingekuwa kesi mahakamani, yeye ndiye angekuwa (na anapaswa kuwa) shahidi namba moja. Ndiye aliyepigiwa simu. Ndiye aliyeshiriki kikao na mazungumzo hayo.
  Ndiye aliyetekwa. Ndiye aliyenyofolewa meno bila ganzi. Ndiye aliyeng’olewa kucha. Ndiye aliyefungwa kamba, akapigwa, akavuliwa nguo na kuachwa uchi. Ndiye aliyetupwa kwenye msitu wa Mabwepande.
  Ndiye huyu anayezungumza haya, tena kwa msisitizo kwamba anayasema akiwa na akili na kumbukumbu nzuri. Tusipomsikiliza Dk. Ulimboka, mhusika mkuu, tumsikilize nani? Tusipomwamini yeye tumwamini nani katika hili?


  Maana, binafsi nasita kumwamini Rais Kikwete. Hakupigiwa, na hakupiga simu iliyosababisha kutekwa na kuteswa kwa Dk. Ulimboka. Yeye na kina Rweyemamu na Balozi Sefue, hawakuwapo wakati Dk. Ulimboka anakamatwa.
  Hawakushiriki – walau Dk. Ulimboka hajawataja – katika jaribio hili la mauaji ililoepushwa na Mungu (kwa sababu anazijua mwenyewe). Wanapata wapi ujasiri huu wa kukanusha kauli ya yule aliyeteswa?


  Au wanafikiri wakikanusha mara kwa mara ukweli utabadilika, wananchi watampuuza Dk. Ulimboka na kuwaamini wao?
  Kama ofisi yao haihusiki, wameshindwa nini kukaa kimya (kwa aibu), au kuagiza vyombo vya dola vifanye uchunguzi wa kina; na kwa kuanzia, vikamtia mbaroni Ramadhani Ighondu aliyetajwa na Dk. Ulimboka, na ambaye uchunguzi wa gazeti la MwanaHALISI ulishamaliza kazi yote ya awali ya kumtambua – ofisini anakofanyia, na nyumbani alikozaliwa?
  Au kwanini serikali imekuwa ikigomea kuunda tume huru ya kuchunguza kilichotokea? Kwanini serikali inakataa ushauri wa wataalamu, wanaharakati, wanasiasa, wakereketwa, wananchi wa kawaida na hata Dk. Ulimboka mwenyewe aliyetekwa?
  Kwanini polisi wamekataa, hadi sasa, kuchukua maelezo ya Dk. Ulimboka na kuyafanyia kazi?
  Katika mazingira kama haya, hata kama vyombo vya dola vitaendelea kugoma kuwakamata wahusika, itaaminika kwa nani? Na isipoaminika, itakuwa na uhalali gani wa kuwatawala wananchi wasioiamini?
  Kwa hali hii, na kwa jeuri hii inayooneshwa na serikali, hata uhai wa Dk. Ulimboka na wanaomtetea uko hatarini. Serikali isiyosikia kwa kiwango hiki, iliyo tayari kutetea na kuficha uhalifu unaohusishwa na maofisa wake, inaweza kuua ili kuficha ushahidi.
  Lakini ushahidi wa suala hili hauwezi kufichika tena. Dk. Ulimboka ameshauanika. Si wengine, tunachofanya sasa ni kuweka kumbukumbu sahihi kwa ajili ya vizazi vijavyo.


  Tunajua madhara yanayoweza kutupata, lakini kwa masilahi mapana ya nchi hii, tunathubutu kupambana na kumwaibisha shetani huyu mbaya aliyeiandama Serikali ya Awamu ya Nne.
  Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliwahi kutamka kwamba Ikulu ni mahali patakatifu. Alikuwa na sababu.
  Kwanza, alitaka kusisitiza utakatifu wa Ikulu. Kwamba, kwa kuwa ndiyo ofisi kuu inayotarajiwa kubeba matumaini ya utumishi wa wananchi wote, inapaswa kuwa kimbilio la wote – wanyonge na wenye nguvu.
  Hata kama ofisi zote zimechafuka, ibaki sehemu moja tu iliyo safi – Ikulu. Kwa maana hiyo, watumishi wote wa Ikulu, tukianza na rais na familia yake, wanapaswa kuwa watu wema mbele ya watu na Mungu.
  Wanapaswa waaminike, na waheshimiwe. Lakini imani na heshima hii lazima vijengwe katika misingi imara isiyotikisika. Je, leo Ikulu yetu inaaminika na kuheshimika hivyo?


  Pili, Mwalimu Nyerere alitaka kusisitiza ukweli kwamba Ikulu haipaswi kutuhumiwa. Ndiyo maana alitoa mfano wa simulizi ya mke wa mfalme. Hata kama hajafanya kosa hilo; kule kutuhumiwa tu kunatosha kumwondolea heshima na utukufu anaostahili. Maana ya ndani ya simulizi hili ni kwamba heshima hailazimishwi.


  Tatu, Mwalimu Nyerere alitaka kuonya – maana alishaona dalili – kwamba ipo siku Ikulu inaweza kusakwa na hata kutwaliwa na watu wasioaminika, na wasioheshimika ipasavyo. Kinachotokea sasa hivi kinazua maswali kama tunakaribia au tmefika huko ambako Mwalimu Nyerere hakutaka tufike.


  Nne, Mwalimu Nyerere alijua kuwa licha ya utakatifu wa Ikulu, si wote walio Ikulu, ni watu wema na watakatifu. Alitaka kuonya kwamba hata Ikulu kuna “wahuni.”
  Hata hivyo, wapo watu wanaodhani kwamba kwa kuwa Mwalimu Nyerere alishapatangaza Ikulu kuwa patakatifu, patakuwa patakatifu tu hata kama yanayofanyika mle si matakatifu. Wamekosea!
  Wapo pia wanaoamini kwamba kwa kuwa wako Ikulu, wakisema neno linapewa uzito ule ule wa kitakatifu, hata kama wanaongopa. Hawa nao wamekosea!


  Na wapo wanaodhani kwamba kwa kuwa Ikulu palishasemekana kuwa patakatifu, hata wakifanya dhambi ndani ya kuta za Ikulu, Watanzania wanalazimika kuzikubali na kuzienzi dhambi za wakubwa kwa sababu ni dhambi takatifu. Hawa wamekosea kabisa.
  Kundi hili la mwisho ndilo linalodhani kwamba ukisema uongo ukiwa Ikulu, uongo huo unageuka kuwa ukweli!


  Katika miaka zaidi ya 10 sasa, yapo mengi yametokea Ikulu ambayo yamepunguza heshima na utakatifu wa Ikulu yenyewe na waliomo. Lakini hili la Dk. Ulimboka linawafanya hata wale waliokuwa bado wana imani na Ikulu hii waone kwamba kuna jambo haliendi sawa.
  Inawezekana watu wa Ikulu ndio pekee wasiojua kinachoendelea kuhusu mkasa uliomkuta Dk. Ulimboka?
  Inawezekana ndio watu pekee hapa nchini wasiojua kuwa umma wa Watanzania unahusisha moja kwa moja sakata hili na jitihada za serikali kuzima mgomo wa madaktari?
  Inawezekana wamemtoa kauli zao hizo, na wanaendelea kupima upepo, huku wakijipanga kufuatilia na kufukuzia wananchi wema wasioridhika na kauli za Ikulu.


  Je, hii itaondoa au itaongeza heshima na imani ya wananchi kwa watawala wao? Hata leo wangeamua kupata maoni ya wananchi, katika hili, nani anaaminika kati ya Rais Kikwete na Dk. Ulimboka?

  SOURCE;
  chrome://newtabhttp//www.freemedia.co.tz/daima/habari.php?id=41765

   
 2. C

  Concrete JF-Expert Member

  #2
  Oct 22, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 3,607
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0
  Tatizo kuu ni huyu kilaza mkuu anayeishi pale magogo kwa kodi zetu huku akiwalamba kisawasawa dada zetu na mama zetu kama anavyotaka, akishirikiana na yule mzembe, kubwa jinga, mshirikina kutoka sumbawanga.
  Hao wengine waliobaki ni kama mazezeta hayatathubutu kusema chochote kuwaogopa waheshimiwa wawili.
   
 3. L

  Lwesye JF-Expert Member

  #3
  Oct 22, 2012
  Joined: Sep 29, 2012
  Messages: 5,297
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Wanajikanyaga lakini wananchi tumeshajua mchezo wao wao ni piga yule ua yule manake wanadhani wataishi pale milele
   
 4. h

  hippocratessocrates JF-Expert Member

  #4
  Oct 22, 2012
  Joined: Jul 1, 2012
  Messages: 3,612
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  Well spoken Abdillahjr..tumeipata, let the mass(people) decide.
   
Loading...