Revealed: Kumbe JK na madaktari Ikulu waliongea haya... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Revealed: Kumbe JK na madaktari Ikulu waliongea haya...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by bibikuku, Mar 13, 2012.

 1. bibikuku

  bibikuku JF-Expert Member

  #1
  Mar 13, 2012
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 828
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Hii ni kwa mujibu wa gazeti la Mwananchi la leo.


  Siri ya JK, madaktari Ikulu yafichuka

  Monday, 12 March 2012

  Kizitto Noya | Mwananchi

  MADAKTARI wametoboa siri ya mazungumzo yao na Rais Jakaya Kikwete wakisema mkuu huyo wa nchi alisita kutoa jibu la moja kwa moja kama atamwajibisha Waziri wa Afya, Dk Hadji Mponda na Naibu wake, Lucy Nkya ama la, badala yake alitaka apewe muda wa kushughulikia suala hilo.

  Hata hivyo, walisema pamoja na jibu hilo walikubali kurejea kazini kutokana na imani waliyonayo kwa Rais wakiamini kuwa ujumbe kuhusu madai yao umefika.

  Ijumaa iliyopita, Rais Kikwete na viongozi Chama cha Madaktari Tanzania (MAT), walifanya mazungumzo Ikulu yaliyokuwa na lengo la kutafuta suluhu ya mgomo huo wa pili ulioanza Machi 7, mwaka huu na kutishia kuvuruga utoaji wa huduma za afya nchini.

  Rais wa MAT, Dk Namala Mkopi alisema jana kwamba suala la kutaka kuwajibishwa kwa mawaziri hao ili kuwepo imani katika mazungumzo yao na Serikali halikuwekwa bayana... “Rais hakuweka bayana kama atawafukuza badala yake alisisitiza apewe muda.”

  Dk Mkopi aliendelea: “Ila alitia shaka katika mambo mawili; alisema kuwafukuza mawaziri hao kutachelewesha utekelezaji wa madai ya madaktari kwa kuwa atakuja waziri mpya ambaye ni mgeni kwa madai hayo na pili alisema ni tabu pia kuwaacha kwa sababu ni vigumu kwao (mawaziri) kutekeleza madai ya watu wasiowaamini.”

  Hata hivyo, Dk Mkopi alisema mbali na hoja hizo mbili katika kuwawajibisha mawaziri hao, Rais hakuzungumzia jambo jipya zaidi ya kujadili madai ya awali ya madaktari hao na kuomba apewe muda kuyashughulikia.

  “Kimsingi, kilichofanyika ni imani yetu kwa Rais. Hakutueleza chochote cha ziada zaidi ya kutuomba turudi kazini kwa ahadi kwamba atashughulikia madai yetu ya msingi,” alisema Mkopi na kuongeza:

  “Sisi tukaamua kumwamini kwa sababu yeye ni mtu wa mwisho wa kumfikishia madai yetu. Tukaona hatuna haja ya kubishana naye zaidi ya kumwachia muda alioomba kuyatekeleza madai hayo.”

  Alipoulizwa endapo walikubaliana na rais madai hayo yatekelezwe katika kipindi gani Dk Mkopi alijibu: “Hapana... hatukukubaliana muda kwa sababu kufanya hivyo ni kuondoa imani ya mtu unayemwamini. Tuliamini tu kwamba atatekeleza madai yetu kama alivyoahidi... na hivyo ndivyo ilivyokuwa kwake alivyotuamini sisi kwamba tungerudi kazini.”

  Kuhusu namna Rais alivyopokea mgomo wa madai yao, Dk Mkopi alisema: “Kimsingi alionyesha kusikitika sana. Anasema yeye binafsi (Rais) aliamua kuwekeza sana kwenye sekta ya afya na asingependa kuiona sekta hiyo inavurugwa.”

  Kabla ya juzi
  Kabla ya mgomo huo uliomalizika juzi, tayari madaktari hao waligoma kwa siku 17 kuanzia Januari 20 hadi waliporejea kazini Februari 7 mwaka huu.

  Katika mgomo huo, madaktari hao walitaka utekelezaji wa maslahi yao mbalimbali ikiwemo kuongezewa mishahara, kupatiwa nyumba, kuongezwa posho na pia kuwajibishwa kwa watendaji wa wizara ambao walikuwa ni Katibu Mkuu, Blandina Nyoni, Mganga Mkuu, Dk Deo Mtasiwa na mawaziri hao.

  Mgomo huo ulitikisa nchi na Januari 29, mwaka huu Waziri Mkuu, Mizengo Pinda alipanga kukutana na wanataaluma hao katika Ukumbi wa Karimjee, Dar es Salaam lakini waligoma jambo lililomkera na kutoa onyo la kuwafukuza kazi wote watakaoshindwa kuripoti katika vituo vyao vya kazi huku akipiga marufuku mkusanyiko wao popote nchini.

  Amri hiyo haikusaidia na badala yake iliongeza makali ya mgomo na ndipo Februari 6, mwaka huu, Pinda alipoamua kuacha shughuli bungeni na kuwafuata katika Hospitali ya Taifa Muhimbili na kufanya nao mazungumzo.

  Katika mkutano huo, Pinda alitangaza kuwasimamisha kazi Nyoni na Dk Mtasiwa huku akisema hatma ya Dk Mponda na Dk Nkya ilikuwa mikononi mwa Rais na kwamba angemfikishia ujumbe huku akiwaambia: “Kitakachotokea nadhani mnakijua.”

  Lakini wiki iliyopita, akizungumzia mgomo huo wa pili alisema isingekuwa rahisi kumpa mkuu wa nchi saa 72 kuwawajibisha mawaziri hao.
   
 2. T

  Topical JF-Expert Member

  #2
  Mar 13, 2012
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  embu fanyeni kazi malalamiko kilo kona ...
   
 3. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #3
  Mar 13, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,268
  Trophy Points: 280
  Very old news for now......
   
 4. bibikuku

  bibikuku JF-Expert Member

  #4
  Mar 13, 2012
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 828
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Too late kwa madokta kueleza haya leo, nakubaliana na wewe
   
 5. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #5
  Mar 13, 2012
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Ukweli ni kwamba JK amewapiga goli la kisigino madaktari wetu.

  Kwa jinsi navyomfahamu, biashara ya kushughulikia issues za madaktari ziliishia pale waliposhikana mikono na kuagana. Huyo ndiyo kikwete. Madaktari wala wasitarajie lolote la maana.

  Ukitaka uamini ona alivyoongea na hao anaowaita wazee wa darisalamu! Ni kama alikuwa anawabeza madaktari.

  Kwa ufupi, madaktari ndiyo mmeliwa hivyo.
   
 6. WA-UKENYENGE

  WA-UKENYENGE JF-Expert Member

  #6
  Mar 13, 2012
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 2,904
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Madaktari wajipange tu upya!! Kukosea ni sehemu ya kujifunza na kuendelea kwenye mafanikio. Haijalishi ni lini lakini filing za blah blah blah ziwekwe na zitumike muda muafaka ukifika.
   
 7. HAZOLE

  HAZOLE JF-Expert Member

  #7
  Mar 13, 2012
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 1,331
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  tutafika tu.....!
   
 8. M

  Mr.Mak JF-Expert Member

  #8
  Mar 13, 2012
  Joined: Feb 23, 2011
  Messages: 2,635
  Likes Received: 496
  Trophy Points: 180
  Nilisha sema mgomo huu wa pili umewatia aibu na utawadharaulisha sana. Mtafanya kazi kubwa kujisafisha. Ona sasa unavyohaha,na ivi kweli umemsikiliza rais! Acheni kuwa wa rejareja kwa kutumiwa,kwa post hii hata madaktari wenzako ambao hawakwenda ikulu watakudharau.
   
 9. c

  cesc Senior Member

  #9
  Mar 13, 2012
  Joined: Nov 25, 2008
  Messages: 156
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  bravo presida
   
 10. taffu69

  taffu69 JF-Expert Member

  #10
  Mar 13, 2012
  Joined: Feb 26, 2007
  Messages: 2,089
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Ila serikali isijipongeze sana kuwa imeibuka mshindi katika sakata hili! Kwa unyeti wa sekta ya afya ulivyo, naogopa sana yasije yakatokea mamabo kama yunayoyaona kwenye sekta ya elimu. Serikali ilikataa kuwasikiliza waalimu na kutekeleza madai yake; yanayotokea sasa kuna wanafunzi wanamaliza darasa la saba hawajui kusoma wala kuandika; vijana hao wasiojua kusoma wala kuandika wanachaguliwa kujiunga na elimu ya sekondari, wahitimu wa form four wanazidi kufeli na wengine hata maadili yamewaponyoka wanaamua kuandika matusi kwenye mitihani pamoja na mengineyo mengi.

  Kwa upande wa madaktari kama wataamua kufanya mgomo baridi kama inavyoonekana kwa waalimu tutarajie maafa makubwa sana kwani kuna uwezekano wa idadi ya vifo kuongezeka na hata vilema pamoja na matatizo mengine yanayoambatana na sekta hiyo.
  "EE MUNGU IBARIKI TANZANIA"

   
 11. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #11
  Mar 13, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Si ndio hayohayo alioleza Kikwete jana? kuna kipi kipya hapo?
   
 12. Miya

  Miya JF-Expert Member

  #12
  Mar 13, 2012
  Joined: Mar 29, 2011
  Messages: 817
  Likes Received: 1,208
  Trophy Points: 180
  Bibikuku hyo sio habari ya leo ni ya trh.12 Jk kabla hajaongea na wazee
   
 13. Gamba la Nyoka

  Gamba la Nyoka JF-Expert Member

  #13
  Mar 13, 2012
  Joined: May 1, 2007
  Messages: 6,591
  Likes Received: 6,755
  Trophy Points: 280
  Mgomo wa pili wa madaktari ni blunder kubwa sana kwao!. Mgomo huu ni abandonment ya madai ya msingi ya maslahi na mazingira mazuri ya utendaji wa kazi na badala yake kuwekeza katika personal conflicts za tit-for-tat response!.

  Sasa jiulize akishaondoka waziri wa afya ndiyo nini?, ndiyo maslahi yameboreshwa?, ndiyo mazingira mazuri ya utendaji wa kazi yameboreshwa?.

  Je raisi akiamua kutomwajibisha waziri, madaktari watamshinikiza raisi ajiuzuru?.
  Maana at the end, kama tatizo ni raisi then watakuwa wanafiki kumtaka waziri ajiuzuru na kumuacha raisi.

  Huu mgomo wa pili, nadhani ni kihoro/uwoga wa badhi ya viongozi wa madaktari kuhofia kwamba waziri akibaki madarakani anaweza kuwamaliza mmoja mmoja, kwa hiyo wanaleta siasa ili aondoke pale wizarani!. That is too bad!!!!.

  Madaktari watuachie wananchi, tuwawajibishe mawaziri wetu kwa kumshinikiza raisi kupitia majukwaa yetu kama vile vyama vya siasa, wabunge, ngo etc, wao watimize kiapo chao na sheria ya uajili waliyotiliana na serikali pindi wanapewa ajira, ila wakiamua kugoma basi wagome kwa mambo ya msingi yenye kulenga kujenga kitaasisi na si katika tit-for-tat response zisizo na maana yoyote!
   
 14. N

  Nsaro New Member

  #14
  Mar 13, 2012
  Joined: Mar 12, 2012
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Madokta ni wasomi, wana hekima vilevile, never argue with a fool people might not notice the difference, ujumbe umefika wananchi wanapoamua inawezekana, hongereni :hand:
   
 15. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #15
  Mar 13, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,064
  Likes Received: 6,518
  Trophy Points: 280
  masikio yamesikia, yetu ni macho tu sasa.
   
 16. mchadema

  mchadema JF-Expert Member

  #16
  Mar 13, 2012
  Joined: Jul 8, 2011
  Messages: 412
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 33
  madaktari hawaja aibika hata kidogo!! watakao umia ni watz kwa kuhudumiwa na watu waliokataa kusikiliizwa. Unaheri we fisadi unayetibiwa India kwa kodi za watz
   
 17. mchadema

  mchadema JF-Expert Member

  #17
  Mar 13, 2012
  Joined: Jul 8, 2011
  Messages: 412
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 33
  hii post inaoniyesha ni jinsi gani ulivyo gizani,iliyochemka ni serikali yako inayoendelea kushindwa kufanya maamuzi hata kwa maswala yasiyohitaji ubongo na yanayogarimu uhai wa taifa, kiuchumi na kiafya.

  Wewe ni mmoja kati ya wachache mmnao wanyonya watz, mkijitahidi kila mara chadema waonekane wabaya ili nyie muendelee kuwanyonya watz. ULAANIWE WE GAMBA LA MLAANIWA. MAWAZO YAKO YASIDUMU HATA NDANI YA SEKUNDE NDANI YA WATZ.
   
 18. NGUVUMOJA

  NGUVUMOJA JF-Expert Member

  #18
  Mar 13, 2012
  Joined: Jul 1, 2011
  Messages: 1,353
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Nchi hii inaongoza, sio kwa kufanya kazi za kujenga Taifa, bali kwa malalamiko. Kila mtu analalamika nchi hii, Kuanzia juu kabisa (Mh.Rais) hadi wa chini kabisa (ndugu zangu walalahoi).

  Pakiundwa tume ya kusikiliza malalamiko ya Watz. nna uhakika hata hao watakaokuwa wajumbe wa hiyo tume nao pia watakuwa na malalamiko.

  Ndugu zangu tunaelekea wapi?
   
 19. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #19
  Mar 13, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Wacha kulalamika!
   
 20. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #20
  Mar 13, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,011
  Likes Received: 1,816
  Trophy Points: 280
  Kwa hiyo kwa yale masaa sita waliongea nini? Madaktari wamemwamini Rais na waliongea in camera na Mgomo umeisha tuache chokochoko tuwaache madaktari wafanye kazi na serikali ifanye kazi yake kwa mujibu wa mazungumzo yao.
   
Loading...