Pinda Pinda Pinda, hao unaowalazimisha wakafanye kazi sio makuli wa kubeba mizigo, hao ni wataalamu, tena taaluma yao ni nyeti sana, sasa wakirudi na kuanza kutibu isivyo itakuaje? Ukienda ukikutwa na Malaria waseme wakukate mkono. Ukiwa na pressure basi wafanya operation ya utumbo, ukiumwa kidole cha mguu, wakate masikio na kutoa macho. Unataka wakafanye hivyo???? Hawa si watu wa kuwalazimisha hata kidogo, bila muafaka hakuna kitakachoeleweka. Hembu tumia busara. Juzi tu mmeona viongozi wenzenu wanaotumia maguvu kilichowakuta huko Libya na Misri, bado tu hamjifunzi. Kwa hakika Ocampo lazima aje awafungulieni mashitaka ya hawa wagonjwa wanaokufa kwa kiburi cha Serikali.
Madaktari, hakuna kurudi kazini, wakiwafukuza kazi kesho, ndugu zenu tupo, hampo kisiwani, hamtakosa ugali na mchicha, tutakula tu huohuo, kwani tumekuwa tunakula kwa siku nyingi. Nawaomba na manesi kesho tangazeni nanyi kuweka zana chini tuone watafanya nini. Hawa wasicheze na nguvu ya Umma! Pinda umetia aibu, sijui utaficha wapi uso wako, na ukienda Bungeni wewe safari hii hurudi kama waziri mkuu tena, lazima ujiuzuru. kama mnashindwa kuongoza si muachie ngazi waje wenye uwezo?? Hao Askari mnajisumbua tu, wapelekeni hao wakatibu basi huko mahospitalini. Crazzy this Country!!