Sasa ukikuta ajenda hazieleweki ndio utoe lame excuses? Hapo madaktari wamechemsha na wamejidhalilisha. Na wakigoma this time wajue wananchi hawatalaumu serikali.
Rais amesamehe wezi kwani yeye judge? Au mnataka awe anaingilia uhuru wa mahakama?
Rais amesamehe wezi kwani yeye judge? Au mnataka awe anaingilia uhuru wa mahakama?
tatizo unasikiliza propaganda za serikali.Toka mwanzo walijaribu kuzima mgomo kwa propaganda na vitisho wakashindwa.sasa ofisi ya waziri mkuu ikajaribu kurudia njia zile zile chafu badala ya kukaa na ma daktari na kupata ufumbuzi wa kudumu.kwa kugundua hilo ndio maana madaktari walisusia hicho kikao cha alhamis. Kwa taarifa yako,kamati ya waziri mkuu ilijishtukia kua ilikosea,then wakapanga kikao kingine ambacho kilifanyika ijumaa. ktk kikao cha ijumaa,wakakubaliana kua kwa kua makubaliano yeyote yatakayofikiwa ya kuboresha utoaji huduma ya afya Tanzania yatahitaji utekelezaji wa wizara ya afya,ambayo kwa sasa inaongozwa na watu ambao kwa kiasi kikubwa ndio waliochangia kutokea kwa mgomo wa jan-feb,lazima hao waondolewe kwanza kama alivyo ahidi PM ndipo majadiliano memgine yaendelee.Nafkiri umepata pichaSasa ukikuta ajenda hazieleweki ndio utoe lame excuses? Hapo madaktari wamechemsha na wamejidhalilisha. Na wakigoma this time wajue wananchi hawatalaumu serikali.
Liyumba hakshitakiwa, jeetu patel hakushitakiwa, maranda hakushitakiwa? Lukaza hakushitakiwa? Balali hakuondolewa? Si ndio EPA hao au mlitaka rais awaweke kizuizini bila kuwapitishia mahakamani?
Acheni kuongea kama watu msiojua sheria na taratibu.
Hawa madaktari wanaogoma ingekuwa kipindi cha nyerere mnachukua majina halafu utekelezaji unafuata...
Nimesikia kwa vyombo vya habari kuwa next wiki madokta huenda wakagoma ati kwa kuwa bado wizara inaongozwa na mawaziri wale wale waliosababisha mgomo wa awali kitu ambacho serikali kupitia kwa PM ilikuwa imeahidi itakishughulikia.
Kuna tetesi nimezipata kuwa Dr Mponda aliandika barua ya kujiuzuru kwa raisi naye JK akamwambia kuwa " wewe bado u mchanga kwenye siasa, huo ni upepo tu utakwisha, chapa kazi achana na mambo ya kujiuzuru".
Kwa maono yangu madokta mkigoma mtakuwa mnawaumiza raia wasio na hatia kwasababu serikali hii chini ya JK haitakaa iwasikilize kwa maana ya kutatua mgogoro huo. Napendekeza mgomo na maandamano yenu yaelekezwe katika kuupinga utawala mzima wa JK na wateule wake vinginevyo mnajilisha upepo, JK will never respond to your cry!!
Nawasilisha
Madaktari wakirudi kazini wakati madai yao hayajasikilizwa itakuwa utoto, kwanini waliacha watu wakafa mwezi Januari?
Mi nasema tuone kama Jk ni roho ngumu kiasi gani akiona watu wakifa, ilhali anauwezo wa kutekeleza madai ya madaktari na hataki. Eti ni upepo tu, utapita? Madaktari gomeni. Tuone huo upepo utapitia upande gani. Watu watakufa, lakini haki yenu ikipatikana itawaokoa wengi zaidi.
usijadili kitu ambacho hujakifanyia utafiti na kujua ukweli wake. Wale walioitwa kwenye kamati ya pinda walikuwa ni tana ambao mwakilishi ni kanali wa jeshi,watu wamaabara,mwakilishi wao alikuwa mtumishi wizarani. Toka lini kanali wa jeshi akatetea wananchi? Badala ya kuzungumzia maboresho ya wizara wakaishia
Mkuu naona ufaham wako kuhusu EPA ni mdogo au umeamua kuwa mbishi tu au nawe ni mnufaika wa pesa hiyo. Pesa iliyoibwa ni nyingi kuliko iliyo rudi, jumla pesa zinazodaiwa kukwapuliwa na waliofunguliwa kesi ni ndogo kuliko kiasi kilicho rudishwa. Makosa yakifanyika na awamu ya nyuma haimpi waranti raisi ajaye kusamehe kihuni kama alivo fanya. Je, hao "changanyikeni" ni akina nani?.Pesa zimeibwa kipindi cha Mkapa na wizi chini ya Ballali ambaye alitolewa Washington na Mkapa akaletwa sasa kikwete anahusika vp na huo wizi?
Je unajua Jeetu karudisha sh ngapi na wahindi wenzake? Unajua hao kina Lukaza wameleta sh ngapi? Au unajua za maranda tu? Unajua hao changanyikeni nao walileta ngapi?
Sawa tuseme wizi umefanywa na CCM lakini Ballali kama proffessional kuidhinisha malipo yasiyo halali ni makosa. Mimi siwezi kuona signature yako wewe halafu ukanambia eti ulishurutishwa kusaini.kwahiyo ya kusema Ballali kasingiziwa mi nakataa. The guy is dead tumuombee apumzike salama basi.