Mpita Njia
JF-Expert Member
- Mar 3, 2008
- 6,997
- 1,163
Makatibnu au wenyeviti?
HABARI za kuaminika zilizochapishwa katika magazeti mbalimbali nchini hivi leo zinasema kwamba Viongozi wanne wa chama cha Mapinduzi wanamshtaki Bw. Said Kubenea, Mhariri wa gazetil lililosimamishwa na serikali ya Chama hicho kwa madai ya uchochezi ambayo hayakupitia polisi wala mahakamani shilingi Bilioni 4.
Questioning the News inauliza hivi Kubenea mwenyewe ana thamani ya milioni 10.
Na, je, viongozi wote wa mikoa wa CCM wakiwekwa pamoja wana thamani ya bilioni 4 unless, of cource, EPAnization imepenyeza mpaka ngazi hizo za chini?
Sintoshangaa, kama viongozi hawa wote wako upande mmoja wa itikadi au imani......
HABARI za kuaminika zilizochapishwa katika magazeti mbalimbali nchini hivi leo zinasema kwamba Viongozi wanne wa chama cha Mapinduzi wanamshtaki Bw. Said Kubenea, Mhariri wa gazetil lililosimamishwa na serikali ya Chama hicho kwa madai ya uchochezi ambayo hayakupitia polisi wala mahakamani shilingi Bilioni 4.
Questioning the News inauliza hivi Kubenea mwenyewe ana thamani ya milioni 10.
Na, je, viongozi wote wa mikoa wa CCM wakiwekwa pamoja wana thamani ya bilioni 4 unless, of cource, EPAnization imepenyeza mpaka ngazi hizo za chini?
Sintoshangaa, kama viongozi hawa wote wako upande mmoja wa itikadi au imani......
Si ameshawaambia watangulie tu mahakamani ili wakate issue kule? Sasa hayo wanayozunguka zunguka kumpa siku saba za nini? Si watangulie huko? Maana sijui kama atawajibu!Ni kweli halafu wanataka kuombwa radhi ndani ya siku saba!!!!!
Wenyeviti wanane wa CCM wa mikoa , wamefungua kesi Mahakama Kuu dhidi ya gazeti la MwanaHalisi, wakitaka walipwe bilioni 4, kwa madai ya kukashfiwa na gazeti hilo. Katika hati ya mashitaka, wenyeviti hao wanataka kila mmoja alipwe Sh milioni 500, kutokana na gazeti hilo kuripoti kuwa makada hao wa CCM, wanashiriki kwenye njama za kutaka kumngoa madarakani Rais Jakaya Kikwete katika uchaguzi mkuu ujao wa 2010.
Wenyeviti hao ni Deo Sanga (Iringa), Clement Mabina (Mwanza), Khamisi Mgeja (Shinyanga), John Guninita (Dar es Salaam), Nawab Mullah (Mbeya), Onesmo Ngole (Arusha), William Kusila (Dodoma) na Hypolitus Matete (Rukwa). Wenyeviti hao wanailalamikia kampuni inayochapisha gazeti la MwanaHalisi, Mhariri wa gazeti hilo, Kiwanda cha Pritech na Kiwanda cha Standard, ambavyo vinachapisha gazeti hilo pamoja na Saed Kubenea, ambaye ni mwandishi wa habari hiyo.
Duh hii kali Kubenea ana vijisenti vya kutosha kuwalipa waheshimiwa sanaaa !.
Gazeti linalolalamikiwa na wenyeviti hao ni lililotoka Oktoba 8, mwaka huu, likiwa na habari kuwa Njama za kumngoa Kikwete zafichuka, huku habari hiyo ikiambatana na picha ya Rais Kikwete, mwanawe Ridhiwan na Rostam Aziz.
Wanadai katika kesi hiyo, kuwa mwandishi akifahamu nafasi walizo nazo walalamikaji katika jamii, aliamua kwa makusudi kuchapisha habari hiyo, wanayodai ya uongo, ambayo imewaondolea uaminifu wao kwa kiongozi wao wa chama, Rais Kikwete.
Kikwete ni Mwenyekiti wa CCM ambaye ndiye anayeongoza vikao vya Kamati Kuu, Halmashauri Kuu ya Taifa na Mkutano Mkuu wa Taifa, ambao walalamikaji ni watajwa wa baadhi ya vikao hivyo. Wamenukuu aya iliyosema kundi la watuhumiwa wa ufisadi limejipanga kumngoa Rais Jakaya Kikwete ili asigombee urais mwaka 2010, ikimaanisha kuwapo kwa njama chafu za kuwarubuni baadhi ya watu, wasipitishe jina la Kikwete kugombea nafasi hiyo.
Kwenye hati yao, pia wamenukuu aya iliyosema katika CCM taarifa zinasema kundi lililopanga kugombea urais mwaka 2010, limekuwa linapigania kuwapo watu wake katika nafsi za juu za uongozi katika Halmashauri Kuu ya Taifa na Kamati Kuu.
Wanadai kuwa habari hiyo, ilienda mbali zaidi na kuwaingiza wenyeviti hao wanane, kuwa wako katika mpango huo mchafu, kuhakikisha Rais Kikwete hachaguliwi na chama chake, kugombea urais katika uchaguzi mkuu ujao. Kwenye hati hiyo, walalamikaji wanaonyesha aya inayomtaja Guninita, akitajwa kwamba mjenga mkakati, akitumiwa na baadhi ya watuhumiwa wa ufisadi, wenye ushawishi mkubwa ndani ya CCM.
Wameonyesha pia namna gazeti hilo, lilivyotaja sehemu za Mwanza, Dodoma, Arusha na Dar es Salaam, kuwa tayari baadhi ya mikutano ya mikakati imeanza. Walalamikaji wanachambua kashfa katika habari hiyo, kuwa ni kichwa cha habari, kilichosomeka njama kumngoa Kikwete zafichuka na wao kuhusishwa kwenye mpango huo na kumtaja Guninita, kama kiongozi wa mkakati huo.
Pia, wanadai kuwa wamekashfiwa, kwa kuelezwa kuwa ni miongoni mwa kundi la mafisadi, wenye njama hizo, wakati ikitambulika kuwa fisadi ni mtu mwovu, ambaye anaishi kwa ulaghai wa rushwa na mfujaji wa mali ya umma.
Kutokana na mazingira hayo, wenyeviti hao wanaiomba mahakama, itamke kuwa habari hiyo iliwachafua mbele ya jamii wenyeviti hao wa CCM, imwamuru mhariri wa gazeti hilo, awaombe radhi, awalipe fidia waliyoainisha pamoja na riba pia ilipwe kuanzia kesi hiyo ilipofunguliwa; na gazeti hilo liwalipe gharama za mahakama. Gazeti hilo limefungiwa na serikali, baada ya kuchapisha habari hiyo, kwa madai kuwa ilikuwa ya uchochezi, yenye nia ya kumkosanisha Rais Kikwete na mtoto wake Ridhiwan.