Madai ya watumishi na wanachuo wa Chuo cha Misitu Olmotony

Oct 9, 2020
3
1
Pamoja na jitihada zote za Rais Magufuli kutaka utendaji bora wenye weledi katika sekta za Serikali na utawala bora kwenye maeneo ya kazi. Hapa chuoni ni shida na mateso.

Wizara ya Maliasili na Utalii mpo wapi?

Kuna haya yafuatayo:-

Madai:- watumishi tuna madai ya stahiki zetu kwa takribani miezi 9 (semester 3) hatujalipwa. Kigezo ni system ina shida. Je, vyuo vingine ambavyo vipo chini ya wizara hii hii mbona hali haipo hivyo? Achane kututesa na kutunyanyasa.

Madai upande wa wanachuo: wanachuo wamekuwa wakicheleweshewa bima za afya (nhif) sasa ni takribani miezi 6.

Madhara ya hili:

Ni kuchelewesha utendaji wenye tija kwenye uandishi wa miradi.

Ni kushuka au kushuka kwa ufaulu, na.

Kushuka kwa morali ya kazi.

Tunaomba wizara yetu pendwa ya maliasili na utalii kuja kututatulia hili tatizo hapa chuoni. Maana limekuwa sugu sana na mateso kwa sisi watendaji.
 
Back
Top Bottom