Madai ya serukamba-je sita na mwakyembe wanaihujumu ccm ipi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Madai ya serukamba-je sita na mwakyembe wanaihujumu ccm ipi?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwikimbi, Mar 7, 2009.

 1. M

  Mwikimbi JF-Expert Member

  #1
  Mar 7, 2009
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,745
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  MADAI YA SERUKAMBA, SITA NA MWAKYEMBE WANAIHUJUMU CCM IPI?

  Mbunge wa kigoma mjini, peter serukamba, amekaririwa na gazeti la mtanzania la leo linalomilikiwa na mbunge wa igunga, akiwalumu spika sita na mwakyembe kuwa wanakihujumu chama cha mapinduzi yaani ccm, kwa mujibu wa habari hiyo iliyochapishwa katika kurasa wa mbele wa gazeti hilo, serukamba anarusha madongo zaidi kwa spika na mwaKyembe kwa kuwaonya kuwa si wabunge pekee wenye akili nchini. Yeye anadhani kuwa kitendo cha spika na mwakyembe kutoa maoni yao kuishauri serikali iachane nna mitambo kukuu ya dowans ni kuihujumu ccm.

  Sisi ambao siku zote tunakereketwa zaidi na utaifa wetu kuliko ufurukutwa au ukereketwa wa chama chochote cha siasa, tuna kila sababu ya kujiuliza maswali mengi kuhusu matamshi ya mheshimiwa huyu .

  Tunajiuliza kwa kukataa kukubaliana na hoja ya kununua mitambo kukuu yenye harufu ya ufisadi, na kwamba kwa kuinunua mitambo hiyo ingekuwa kinyume cha sheria ya manunuzi ambayo serukamba kama mbunge alishiriki kuitunga, akina sita na mwakyembe wanaihujumu ccm ipi?

  Kwamba spika sita na mwakyembe wamekuwa mstari wa mbele kukemea ufisadi katika bunge letu kwa ukereketwa wa taifa letu na kwa ajili ya wananchi wake ambao wako kwenye lindi zito la umaskini tofauti na serukamba na wateule wachache , akina sita wanaihujumu ccm ipi?

  Kwamba inafahamika wazi kuwa hata mmiliki wa dowans ni ghost, yaani mtu asiyejulikana , na kuwa mtu huyu asiyejulikana amefungua mashtaka dhidi ya tanesco, na hao hao tanesco wanataka kununua mitambo hiyo ya mmiliki asiyejulikana , je wanaopinga hili wanaihujumu ccm ipi?

  Ni wazi kuwa ccm anayozungumzia serukamba si hii tunaoifahamu, yaani kile chama kilichoanzishwa kwa kuunganisa vyama vya ASP, NA TANU vyama vilivyokikomboa nchi hii. Hivyo ccm chama kilichojijengea umaarufu kwa kuongozwa na watu kama akina marehemu sokoine na nyerere ambao walifanya kazi usiku na mchana kumkomboa mwananchi bila hila wala ufisadi, ningetaka serukamba anipe jibu, je ni ccm hii anayosema inahujumiwa au ni ingine?

  Hivi serukamba angetaka mwakyembe na sita, pamoja na sisi wengine tunyamaze wakati kundi la watu wachache kama yeye na wengine wasiozidi ishirini wakiendelea kuikomba asali ya taifa? Yaani tunyamaze wakati wao kupitia kagoda, wakiendelea kukomba hazina ya nchi pale benki kuu,hadi imalizike. ? tunyamaze wakati vijana wetu wakishindwa kuendelea na elimu ya chuo kikuu licha ya kufaulu kwa kukosa ada, wakati serukamba akiwashangilia na kuwalinda mafisadi?

  Ni wazi na nakutaka serukamba unielewe kuwa wewe ni kibaraka wa kikundi cha watu wachache wanaoijiita ccm ambao ni majambazi wa rasilimali za taifa letu, wewe serukamba unaonekana kufaidi kwa ujangili huo wa mali zataifa letu. Kwa kuwa wewe ndiwe msemaji wa washenzi hawa. Au kwa namna au lugha sahihi wewe ni kibaraka namba wani wa wezi wa Richmond, deep green, epa, dowans, nk.

  Kwa hiyo mheshiwa serukamba, ni kweli kuwa sita na mwakyembe na wengine tunaolipenda taifa letu, tunaihujumu ccm ile unaoijua wewe yaani chama chama mafisadi na Wala siyo ile ccm ilyoasisisiwa na mwalimu nyerere.

  Huu ni wakati muafaka kwako na vibaraka wenzako muamue kumtambua mama yenu ambaye ni taifa la Tanzania, na kusahau kushujudia majangili na wezi wa rasilimali za taifa. Kama bado hujatambua hili umechelewa sana, na huna nafasi tena kwa kuwa mapambano yameanza na kamwe hatutshindwa damu ikiwa bado inazunguka katika mishipa yetu ya damu

  ALUTA CONTINUA

  MWIKIMBI M. MWITORI
   
 2. k

  kela72 Senior Member

  #2
  Mar 7, 2009
  Joined: May 5, 2008
  Messages: 168
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mie nadhani muweka hazina wa ccm yaani Rostam, alifanya mpango mitambo ya Dowans inunuliwe na serikali ili apate pasa ya kumsaidia tena best wake Kikwete na CCM kwa ujumla. Sasa kina spika wanaonekana kupingana na chama!
   
 3. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #3
  Mar 7, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Kama kweli mnaipenda Tanzania megukeni tu na wananchi walio wengi watawaona na kuwaunga mkono ,ni lazima mumuwache mkono Sultani CCM ambae wafuasi wake ndio nyie kwa nyie ,mnatupiana madongo na kujificha humo humo.

  Mnachofanya ni kutubabaisha wananchi na tusijue yupi anaipenda nchi hii ,ndio maana yake ,mfuasi mmoja wa Sultani CCM anasema kama hatukununua hii mitambo WaTanzania watalala giza ,mfuasi mwengine wa Sultani CCM anasema tusinunue mitambo hii imechakaa tena ina kesi mahakamani. Yaani mnatufanya wengine tukae midomo wazi na kushangaa pengine na kuul;iza kabisa kuna nini ndani ya kambi ya Sultani CCM ? Isije kuwa mnataka kupinduana ?
   
 4. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #4
  Mar 7, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,187
  Trophy Points: 280
  Naunga mkono kuwa kupinga UFISADI ni kuihujumu CCM. Sera kuu ya CCM ni UFISADI - sasa kama unapiga vita UFISADI, jiondoe CCM. MAFISADI wote nchi hii hukimbilia CCM kwa hifadhi, sasa inapotokea kuwa huungi mkono Ufisadi, ni wazi unahatarisha usalama wa mafisadi ndani ya CCM na hili haliwezi kukubalika kwa namna yoyote. Serikali ya CCM imeundwa kwa misingi ya UFISADI, iliingia madarakani kwa mianya ya KIFISADI na inaendesha shughuli zake nyingi KIFISADI. Hivyo tunaweza kwa sahihi kabisa kuhitimisha kwa kusema CCM ni Chama Cha Mafisadi.
   
 5. Ndamwe

  Ndamwe Senior Member

  #5
  Mar 7, 2009
  Joined: Jun 11, 2008
  Messages: 107
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  ...."Kwa hiyo mheshiwa serukamba, ni kweli kuwa sita na mwakyembe na wengine tunaolipenda taifa letu, tunaihujumu ccm ile unaoijua wewe yaani chama chama mafisadi na Wala siyo ile ccm ilyoasisisiwa na mwalimu nyerere."

  KWANZA HILI NENO "MHESHIMIWA"MIMI NAONA LIONDOKE KATIKA KUWATAMBULISHA HAWA MAFISADI. UTAMUHESHIMU VIPI FISADI? Heshima mtu anaitengeneza mwenyewe na si kumuita mtu asiyestahili, hawa na wezi kama wezi wengine wa kawaida, heshima inatoka wapi hapo. Naona kuna haja ya kubadilisha huu utangulizi kwa watu wabunge na madiwani kwani haiingii akilini mtu aitwe mueshimiwa halafu ni mwizi, nk.
   
 6. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #6
  Mar 7, 2009
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Serukamba haijui CCM na ndio maana anasema wakina Sitta na Mwakyembe wanaihujumu CCM!! CCM asilia ambayo moja ya miiko yake mikubwa ni ' RUSHWA NI ADUI WA HAKI, SITATOA WALA KUPOKEA RUSHWA" ndio hiyo wanayoitetea wakina Sitta na Mwakyembe; hiyo CCm ya wakina Serukamba ni hii ya mabaradhuri, wezi, mafisadi wanaojidai kuwa wanaipenda nchi kumbe wanatanguliza matumbo yao mbele !! Serukamba ni mtu anaeiabisha CCM na ndio maana hata wana ccm halisi wanamyima kura za kuwa mjumbe wa halimashauli yao kuu. Katika wabunge mufilisi wa akili huyu ni nambali one!!
   
 7. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #7
  Mar 7, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,413
  Likes Received: 81,452
  Trophy Points: 280
  Huyu Serukamba ni mtetezi wa mafisadi na inawezekana na mwenyewe ni fisadi. Nitafurahi sana kama atashindwa katika uchaguzi ujao maana hastahili kabisa kuwa muwakilishi wa wapiga kura wa jimbo lake.
   
 8. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #8
  Mar 7, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Anachosema Serukamba ni kweli. Sitta na Mwakyembe wameihujumu CCM. Hiyo mitambo ya Dowans huenda ikawa ilikuwa njia mojawapo ya CCM kujichotea hela za uchaguzi wa 2010. Sasa Sitta na Mwakyembe wameweka mchanga kwenye kitumbua chao.
   
 9. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #9
  Mar 7, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,413
  Likes Received: 81,452
  Trophy Points: 280
  Uchaguzi wa UVCCM, Wazazi na kama sikosei UWT uliahirishwa kwa kukosa pesa, sasa CCM wakipiga mahesabu ya gharama za uchaguzi wa 2010 hayafiki kokote ndiyo maana wakaja na mradi wa vitambulisho shilingi 200 bilioni na ununuzi wa dowans shilingi 60 billioni. Wakishakatiwa mgawo wao hapo basi mahesabu yatakamilika bila matatizo yoyote.
   
 10. n

  nzala Member

  #10
  Mar 7, 2009
  Joined: Dec 24, 2008
  Messages: 43
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Huyu Serukamba, ni mmoja wa wasemaji wa wale ambao ni wezi wa rasilimali za Taifa, yaani Rostam na washirika.Vi vema watu aina kuwapuuza kwani ni vichaaa!

  Big up mwikimbi kwa thread yako!
   
 11. G

  Giroy Member

  #11
  Mar 7, 2009
  Joined: Dec 17, 2008
  Messages: 82
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nashukuru sana jwa wachangiaji ktk mada hii.Anayetete ufisadi ni fisadi pia,bwana serukamba na hao wanakutuma mmeshindwa,kelele zenu Sita, Mwakyembe na wengine imesaidia sana,nawashukuru wote ambao mmechangia kuukataa ufisadi huu waDowans.SERUKAMBA FISADI MKUBWA WEWE,ONGEA MAMBO YANAYOJENGA,KIGOMA WANAHITAJI MAENDELEO WEWE UNAKUWA MUWAKILISHI WA MAFISADI. UNASHANGAZA SANA WEWE PETER.
   
 12. Monsignor

  Monsignor JF-Expert Member

  #12
  Mar 7, 2009
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 523
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wajameni mnashangaa nini kuhusu huyu mbunge? Si ni mbunge kutoka Kigoma ama hamjapitia ile thread inayouliza Wabunge wa Kigoma wanamatatizo gani?
   
 13. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #13
  Mar 7, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Serukamba ni mpuuzi, mpaka sasa bado hajaona kuwa anajiaibisha na kuwaabisha watu waliomchangua. Inabidi aambiwe wazi kuwa maslahi ya taifa lazima yawekwe mbele. Sio upuuzi ambao kila kukicha anendelea kuuonesha.
   
 14. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #14
  Mar 7, 2009
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Hahahahaha ama kweli wabunge wa Kigoma wanavituko!
   
 15. A

  Audax JF-Expert Member

  #15
  Mar 7, 2009
  Joined: Mar 4, 2009
  Messages: 444
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Serukamba uache mbwembwe hapa hamna cha ccm wala cha vyama vingi,nilitegemea kwa mtanzania yoyote mwenye uzalendo na nchi hii,ajue kuwa kwa sasa hatutaki ufisadi. We Serukamba utajiju na Rostam wako,tafuta njia nyingine mbadala hii ta dowans imeota nyasi. Big up JF
   
 16. O

  Ogah JF-Expert Member

  #16
  Mar 7, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  yeye badala ya kushukuru kuwa angalau kuna wabunge wanaoiweka CCM hai mbele ya wananchi........yeye analeta upuuzi........damn
   
 17. t

  tk JF-Expert Member

  #17
  Mar 8, 2009
  Joined: Feb 7, 2009
  Messages: 270
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Naona jamaa mmekuwa na mawazo mgando. Hamtazami tena hoja za kiuchumi mmeingiza tu akilini mwenu hoja za chuki kiasi kwamba mnashindwa kutambua ukweli.

  Ukweli aliousema Serukamba ni kuwa, iwapo nchi itaingia katika janga la giza, ni Serikali ya CCM ndiyo itakayo laumiwa. Sasa wanaotaka nchi iingie katika giza ni Mwakyembe na Sitta kwa kuzuia Tanesco ichukue hatua za kufaa kuepusha balaa hilo. Sasa huoni kuwa hawa kweli wanaihujumu CCM?
   
 18. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #18
  Mar 8, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  WanaJF kuna nyakati inabidi tuwe tunasameheana, baadhi yetu tunafikia hatua ya kuonesha frustrations kwa kutumia lugha zisizofaa, kutokana na hoja za kipuuzi na uwezo mdogo unaooneshwa na waheshimiwa tunaowachagua kutuwakilisha. Baadhi ya nyakati inakuwa ni vigumu sana kuelewa hawa waheshimiwa wanagombea madaraka au dhamana ya kutuwakilisha kwa nia gani. Pesa, posho na mashangingi tu? na kumwachia Rais kazi ya kuangalia mwelekeo wa nchi. Sifa au kutumia dhamana kwa kuji-gratify, kupata access ya kuongea ujinga kwenye vyombo vya habari? Au kuwawakilisha wanajimbo, watanzania na kutumia akili zao kuhakikisha taifa linaendelea na watanzania tunaishi maisha bora???.
  Mpaka leo hii sijaona chochote cha ajabu sana ambacho kiko kwenye dunia za wanaoishi na kuongozwa kistaarbu ambacho hapa Tanzania hakiwezi kufanyika. Ambako wawakilishi wako serious na kuwawakilisha wananchi na kuhakikisha serikali inatekeleza majukumu inayotakiwa kutekeleza. Wezi na mafisadi wanafukuzwa na kuadhibiwa. Hata Italy ambako nchi inatawaliwa na mafia maslahi ya taifa yako mbele kuliko maslahi ya watu binafsi. Lakini hapa kwetu kuna wabunge ni wapuuzi kweli, mpaka unaweza kujiuliza hawa wabunge walitumi credentials gani kujiuza majimboni.
  Inasikitisha sana kuona mbunge na akili zake timamu anatetea mafisadi, anawapinga na kuwaona wajinga wanaopigania taifa, na yeye kujiona ana akili sana. Naona litakuwajambo la maana kama kutakuwa na utaratibu wa ku-screen watu kabla kuwapa fursa ya kugombea nafasi. Kigezo cha kuwa na umri wa miaka 18 na mtanzania peke yake hakitoshi.
  Tukumbuke kuwa vibrant opposition, CCM safi na juhudi za watanzania ndio vitasukuma mbele nchi yetu. Sio utapeli wa kisiasa.
   
 19. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #19
  Mar 8, 2009
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...mnh, wallahi naona aibu, duh! mbunge wangu anaropokwa utadhani 'kalambishwa?' hii ni aibu, aibu, aibu!
   
 20. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #20
  Mar 8, 2009
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,848
  Likes Received: 2,423
  Trophy Points: 280
  ..huyu ndio yule mbunge ambao watonyaji wanasema ni mbogaa....kama ndivo atatetea chochote cha ma top wake....
   
Loading...