Madai ya Mengi: Polisi kujichunguza yenyewe? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Madai ya Mengi: Polisi kujichunguza yenyewe?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Zak Malang, Oct 14, 2010.

 1. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #1
  Oct 14, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  WanaJF:

  Hii imekaaje? Polisi kuchunguzana kuhusu tuhuma zinazoelekezwa kwao wenyewe? Daima jamaa hawa hulkindana, hivi kweli haki itatendeka? Soma habari hii:

  IGP Mwema: Tunachunguza Polisi waliotajwa na Mengi

  [​IMG] Aunda timu ya polisi
  [​IMG]
  Imekwisha kuanza kazi
  [​IMG]
  Takukuru nao wachunguza  [​IMG]
  Inspekta Jenerali wa Polisi, Said Mwema

  Inspekta Jenerali wa Polisi, Said Mwema, ameunda timu ya maofisa waandamizi wa polisi kuchunguza njama za maofisa watatu wa Jeshi hilo za kutaka kumbambika dawa za kulevya mtoto wa Mwenyekiti Mtendaji wa IPP, Abdiel Mengi.

  Habari za njama hizo chafu zilifichuliwa na Mwenyekiti Mtendaji wa IPP, Reginald Mengi, juzi alipozungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dar es Salaam.

  Mengi aliwataja maofisa hao watatu kuwa ni Mkuu wa Kitengo cha Kudhibiti Dawa za Kulevya, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Godfrey Nzowa, Mkuu wa Upelelezi wa Kanda

  Maalum ya Dar es Salaam, Charles Mkumbo na askari mwingine wa kitengo cha Polisi wa Kimataifa (Interpol), aliyemtaja kwa jina moja la Hendry. Wote waliahidiwa kulipwa kiasi kukubwa cha fedha kuanzia Sh. milioni 15 hadi dola za Marekani 40,000.


  IGP Mwema alisema timu hiyo ambayo iliundwa juzi usiku mara baada ya taarifa za madai hayo kutoka kwenye vyombo vya habari, ilianza kazi rasmi jana asubuhi na itaongozwa na Mkuu wa Upelelezi wa Jinai, (DCI), Robert Manumba.

  Katika madai hayo, Mengi aliviambia vyombo vya habari kuwa, maofisa hao waandamizi wa jeshi hilo, walitaka kumbambika dawa za kulevya Abdiel katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere Septemba 26, mwaka huu.

  IGP Mwema alieleza kuwa alipokea taarifa za tukio hilo juzi usiku kwa njia ya simu ndipo alipoamua kuunda timu hiyo mara moja kwa ajili ya uchunguzi wa madai hayo.

  "Kwa kawaida Jeshi la Polisi tuna kitengo cha kupokea malalamiko ya polisi wenyewe na wananchi, hili la Mengi tumelipokea kwa unyenyekevu kupitia vyombo vya habari, na kwa sasa tayari utekelezaji umeanza kuna timu nimeiunda," alisema.

  Mwema alisema ameunda timu hiyo ili haki itendeke na ukweli ujulikane.

  Alitaja baadhi ya watu waliopo kwenye timu hiyo kuwa ni Naibu DCI, Kamishna Msaidizi wa Jeshi hilo, Peter Kivuyo, Kamishna Msaidizi Mwandamizi, Samson Kasala, pamoja na wadau wengine wa usalama.

  "Siku zote penye ukweli uongo hujitenga, tumeunda timu hii ili tuweze kujua ukweli ni upi, lakini ili iwe ya uwazi zaidi, litakalojitokeza tutawaarifu na hatua zitachukuliwa kwa wale wote watakaobainika walitenda kosa," alisema.

  Hata hivyo, Mwema alipoulizwa timu hiyo ameipa muda gani kukamilisha uchunguzi, alisema kutokana na taarifa alizipokea juzi usiku kwa njia ya simu (bila kumtaja aliyempigia), aliamua kuchukua hatua haraka kwa kuunda timu hiyo.

  "Swali lako mwandishi nitalifanyia kazi nitakapokutana na timu husika, nitakaa nao ili tupange ichukue muda gani wa uchunguzi huo, lakini hadi sasa tayari wameshaanza kumhoji mhusika aliyetoa taarifa hizo (Mengi)," alisema. Katika hatua nyingine, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) nayo kwa upande wake imesema kuwa inaendeleza uchunguzi wa tukio hilo ulioanzishwa na vyombo vingine vya upelelezi chini ya ofisi ya DCI.

  Taarifa iliyotolewa jana na Takukuru kwa vyombo vya habari na kusainiwa na Ofisa Uhusiano, Doreen Kapwani, ilisema kuwa watafanya hivyo kutokana na malalamiko hayo kudaiwa kuhusishwa na vitendo vya rushwa.


  Aidha, Takukuru imewataka wale wote wenye ushahidi kuhusiana na tuhuma hizo kutoa ushirikiano ili waweze kufanikisha uchunguzi wao.

  Mpango huo kwa Mujibu wa Mengi, ungetekelezwa siku Abdiel alipokuwa asafiri kikazi kwenda India na wenzake wanne Septemba 26, mwaka huu.

  Aidha, Mengi alisema bahati nzuri mtoto wake aliahirisha safari hiyo ndipo mchezo huo uliposhindwa kufanikiwa, lakini watuhumiwa hao walikuwa wamekwisha kupokea nusu ya malipo ya kazi hiyo.

  Alisema Kamishna Nzowa, Kamanda Mkumbo Henry, waliahidiwa donge la Dola za Kimarekani 40,000 wakati vijana wawili ambao ni wafanyakazi wa uwanja wa ndege waliahidiwa Sh. milioni 15 kila mmoja.

  Mengi alisema baada ya kupata taarifa kutoka kwa wasamaria wema, alilazimika kufuatilia tukio hilo kwa kina na kubaini kuwa maofisa hao walipokea nusu ya malipo ambayo ni Dola za Marekani 20,000 kila mmoja wakati vijana wa uwanja wa ndege walipewa Sh. milioni saba kila mmoja.


  Pia, alisema kuwa mchezo huo ulimhusisha kijana mmoja anayefanya kazi kwenye kampuni za simu nchini ambaye hakumtaja jina lake.

  Alisema kijana huyo aliahidiwa Sh. milioni 15 na kwamba alipewa Sh. milioni saba kama malipo ya awali.

  Mengi alisema kashfa hiyo iliasisiwa na mfanyabishara mmoja nchini ambaye ni miongoni mwa wale aliowataja kuwa mafisadi papa mwaka jana, na kwamba alitenga Sh. bilioni tatu kutekeleza uovu huo.


  CHANZO:
  NIPASHE
   
 2. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #2
  Oct 14, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Labda na mimi niulize swali...Hivi yule mtu Afisa wa Polisi alikuwa akiitwa Abdallah Zombe alishinda au kushindwa kesi?...na sasa yuko wapi?
  Kesi ya Ngedere hiyo broda/sisto!
  Kwanza unaambiwa kuwa hata huyu Kamanda Nzowa anatumiwa na wenyewe, sasa si waona shughuli iliyopo?
   
 3. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #3
  Oct 14, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Sidhani kama polisi anaweza kujichunguza mwenyewe
   
 4. NGULI

  NGULI JF-Expert Member

  #4
  Oct 14, 2010
  Joined: Mar 31, 2008
  Messages: 4,812
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Mengi chanzo chake cha habari kimesimama alitakiwa akikodishie serikali kifanye nao kazi kwa mkataba na sisi wanyonge tujikomboe kwa maovu kama haya(kama ni kweli)
   
 5. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #5
  Oct 14, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0

  Zombe alishinda kesi kwa sababu ingawa JK aliunda Tume iliyoonekana huru chini ya Jaji Kipenka, polisi, wakishirikiana na waendesha mashitaka waliiboronga kesi kimakusudiu ili ashinde -- kwa kumfungulia charge moja tu. Ilitakiwa afunguliwe charge nyingi ili mojawapo imnase!

  Kuhusu Mengi, mimi nadhani asipoikataa hiyo tume ya mapolisi watupu, basi huenda atajikuta yeye ndiye mzushi. Atambue anapambana na watu ambao wanapesa nyingi mno (walikuwa tayari kutumia Sh bil 3 katika zoezi hilo) na hivyo polisi hao kutiwa mfukoni ni rahisi tu. Halafu kuna JK -- yeye huyu hawezi kumsaidia Mengi katika hili sakata kwa sababu anawaogopa hao mafisadi waliomuingiza madarakani, na ambao wanafanya kila njia aendelee hadi 2015. This country has become a bloody f***** country!!!
   
 6. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #6
  Oct 14, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Mimi nauliza: Hivi Mengi hakuwa ametoa taarifa polisi kabla ya kuita waandishi wa habari? IGP Mwema anasema alipata habari hiyo kwa kupigiwa simu na mtu (hakumtaja) usiku ule na hapo akaanza kuslishughulikia suala hilo kwa kuunda tume.

  Ataunda Tume kwa kusikia tu habari kwenye vyombo vya habari? Kisha fanya mara ngapi namna hiyo?

  Mimi nadhani Mwema anajikosha tu, Mengi alikuwa ametoa taarifa polisi lakini walimpuuza ndo maana alitoa kwenye bomba. Au pia inawezekana Mengi aliamua kufanya uchunguzi mwenyewe (kumbuka naye ana mtandao mkubwa) nahakutaka kutoa taarifa polisi kwa sababu polisi wangevurunda tu kimakusudi, kitu ambacho kingeharibu kabisa hata uchunguzi wake binafsi.

  Kwa hapo inabidi nimvulie kofia mzee Mengi, maana anajua how corrupt the entire police force is!!
   
 7. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #7
  Oct 14, 2010
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135

  Chochote watakachoamua ndio watafanya, sasa hivi usipokuwa na nguvu huna haki. Ukiwa na nguvu na pesa at least unaweza kutumia pesa zako kupata haki. Sitegemei lolote kutokana na uchunguzi huo wa polisi. Kama kutakuwa na lolote itakuwa kama kesi ya Zombe, mpaka leo walioporwa na kuuawa hawana wa kuwatetea, so damu yao imepotea bure and we have to live with it. More still to come.
   
 8. eucalyptos

  eucalyptos JF-Expert Member

  #8
  Oct 14, 2010
  Joined: Jan 23, 2010
  Messages: 381
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Hii nyuzi niliisikia tu kwani sikubahatika kuangalia runinga that day.

  This is what the so called police, takukuru, vikosi maalum (incl madawa ya kulevya) does.
  4 long time watz wamelalama kuhusu vyombo hivi na unyanyasaji wake kwa raia. Hawako kulinda usalama wa watz but wako tayari kufanya lolote lile ili kupata pesa. HAWA NI WABAYA KULIKO MAJAMBAZI ETI kwani tuwakaribiapo huhisi kuwa "mikononi mwa wachungaji" kumbe ni "MIKONONI MWA MBWA MWITU" It's very dangerous.

  Kwenye issue ya madawa ya kulevya hapa ni MOTO, mtandao wanaujua na ni wao (they are in), ndiyo maana hata mitaa inayojulikana wazi kwa uuzaji, usambazaji na utumiaji kama Magomeni, Jangwani & Kindoni inaendelea kufanya hivyo bila woga wala wasi hata kificho.

  Polisi ya Tz na vyombo vyote vya usalama vinahitaji kusafishwa bila hivyo HAKUNA HAKI HATA KIDOGO.
   
 9. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #9
  Oct 14, 2010
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,328
  Likes Received: 1,794
  Trophy Points: 280
  Hii nayo imekaa kama movie ya mafia. Ngoja tuone maendeleo yake.
   
 10. f

  fimbo ya mnyong New Member

  #10
  Oct 14, 2010
  Joined: Oct 5, 2010
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hii ni hatari, tutapona kweli ama kweli nchi yetu imeuzwa
   
 11. czar

  czar JF-Expert Member

  #11
  Oct 14, 2010
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 340
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Polisi haiwezi ikajichunguza na kutoa ripoti sahihi kwa umma, hasa polisi ya Bongo. Kibaya zaidi suala lenyewe linahusisha wakuu wa vitengo hapo ndo kabisaa tusitegemee ripoti tutakayoielewa, italetwa lakini itakavyochakachuliwa kila mtu atakoma. Na marafiki wa IGP ni nani? Kama sio wakuu wa vitengo? Sasa usikute hata yeye ishu hii anaijua.
   
 12. M

  Mfwatiliaji JF-Expert Member

  #12
  Oct 14, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 1,325
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Yaani kwa hii move,
  inaonyesha jinsi baadhi waTZ walivyoamua kuvua ubinadamu na kuwa kama wanyama hatari wa porini.
  Bahati njema wamejipeleka kwenye wrong target..RM hatakubali yaishe kirahisi, walikusudia kuangamiza kizazi chake. Kama alivyosema ni kwamba na yeye amejiandaa, kwamba liwalo na liwe.
   
 13. M

  Mboko JF-Expert Member

  #13
  Oct 14, 2010
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 1,067
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Kwa upande wangu mie kama mwananchi mpenda maandeleo kungepashwa kuundwa kamati nje ya jeshi hilo na sio wenyewe sasa kweli ushawahi kuona panya akimkamata paka,hapo igp hakufanya lolote.inabidi asasi ambazo si za kiserikali kuagizwa na huyo igp ziunde kamati then hapo haki itatendeka kwani hao polisi wanalindana.

  Wajua hawa watu ni washenzi sana kwa mfano yule yuko kwa post flani hivi atafanya mambo machafu then wa upande mwingine atamkingia kifua kwani next time naye itatokea kwake, kwa maoni yangu nasema hapo hakutatendeka haki
   
 14. Mallaba

  Mallaba JF-Expert Member

  #14
  Oct 14, 2010
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 2,560
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  Sijawahi kuona pepo akikemea setani tokaaaaaaaa. Ila itawezekana tu endapo hao watajwa hawakushirikiana na viongozi wengine, lakini inavyoonekana huo ni mtanda mkubwa wa Mafisadi Papa na wanatumia pesa chafu sana hivyo huu uchunguzi sijui kama utafika kokote.
   
 15. Mpambalyoto

  Mpambalyoto JF-Expert Member

  #15
  Oct 14, 2010
  Joined: Mar 26, 2010
  Messages: 752
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wanasema ukiona mchungaji na mchinjaji lao moja, jua kondoo mwafwa!
   
 16. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #16
  Oct 15, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,223
  Likes Received: 1,412
  Trophy Points: 280
  Nyiye mnataka mtuhumiwa achunguzwe na nani?. Mbona nyie mmesha lituhumu jeshi la polisi kuwa ni wakosefu na kuwa mengi ni muonewa?!. Hivi mkipewa kazi ya uchunguzi mtatenda haki?!.
   
 17. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #17
  Oct 15, 2010
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,516
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Safi mwema but ili kutoharibu uchunguzi hawa watu wangesimamishwa nyazifa zao kwanza.
   
 18. PhD

  PhD JF-Expert Member

  #18
  Oct 15, 2010
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 3,819
  Likes Received: 818
  Trophy Points: 280
  hapa kuna harufu kubwa ya umafia acha niingie kazini kutafiti ukweli na undani wa taarifa hii, nitatoa ripoti mapema iwezekanavyo hapa JF.
   
 19. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #19
  Oct 15, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,223
  Likes Received: 1,412
  Trophy Points: 280
  Marksman, unataka mutuhumiwa wa uharifu achunguzwe na nani?, mbona wewe umekwisha hukumu kuwa jeshi l a polisi ni wakosefu na Mengi ni muonewa?!. Hivi wewe ukupewa kufanya uchunguzi utatenda haki kweli?. Mbona hupendekezi ni nani afanye uchunguzi? au ITV ndiyo inatosha kufanya uchunguzi na kuhukumu na sisi sote tukubaliane na hilo?. Rember " love somebody before you judge him/her"
   
 20. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #20
  Oct 15, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Mwema alipigiwa simu na fisadi mwenye ishu kwamba deal imebumbuluka.
  pole zake mengi maana kama niwajuavyo polisi wanaweza kumchinjia baharini
   
Loading...