Madai ya CCJ ya kipuuzi - Msekwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Madai ya CCJ ya kipuuzi - Msekwa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Luteni, May 28, 2010.

 1. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #1
  May 28, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Kama nilivyobashiri kuwa CCM na Tendwa watakuja na majibu ya kupuuza madai ya Ccj ndivyo inavyotokea sasa bado tutasikia mengi toka kwa Tendwa,

  SIKU moja baada ya Chama Cha Jamii (CCJ) kutoa shutuma kali za kuhujumiwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) ili kisipate usajili wa kudumu, madai hayo yamepuuzwa na uongozi wa juu wa chama tawala.

  Akizungumza na Tanzania Daima jana, Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara na Spika wa zamani, Pius Msekwa, aliwataka Watanzania kupuuza madai hayo aliyoyaita ya kizushi.

  “Ndiyo binti yangu, kwani wewe unayaamini hayo?” Msekwa alimuuliza mwandishi wa habari hizi aliyeomba kupata kauli ya CCM kuhusu madai ya kufanya hujuma pamoja na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa ili kukinyima usajili wa kudumu CCJ.

  Hakuishia hapo Msekwa aliendelea kusema, “Jawabu lako ni kupuuzia maneno usiyoyaamini… usiyape uzito maneno ya kipuuzi na kizushi ambayo hata wewe huyaamini, eee basi tuishie hapo endelea kuyapuuzia,” alisema Msekwa.

  Katika madai yake, CCJ ilinukuu kauli mbalimbali za kejeli, zenye kuonyesha kuwa ni ndoto kwa chama hicho kipya kushiriki kwenye uchaguzi mkuu ujao zilizotolewa na viongozi wa chama tawala na Msajili wa Vyama vya Siasa, John Tendwa, kwa nyakati tofauti.
   
 2. B

  Boramaisha JF-Expert Member

  #2
  May 28, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 820
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Huyu mzee anazeeka vibaya! Walichofanya CCJ ni kunukuu aliyoyasema huko nyuma. Kwa nini anataka Watanzania wayapuuzie aliyoyasema mwenyewe?
   
 3. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #3
  May 28, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
  .........and.................ACTION!
   
 4. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #4
  May 28, 2010
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Sisi wenye akili tuna jua yeye Msekwa ndiye mpuuzi na anafaa kupuuzwa!
   
 5. Shalom

  Shalom JF-Expert Member

  #5
  May 28, 2010
  Joined: Jun 17, 2007
  Messages: 1,315
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Upo mzee wa texas?
   
 6. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #6
  May 28, 2010
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Nipo kiongozi najiandaa August kwenda kwenye Kampeni!
   
 7. Shalom

  Shalom JF-Expert Member

  #7
  May 28, 2010
  Joined: Jun 17, 2007
  Messages: 1,315
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Tutakutana huko mzee!

  Na wewe unakwenda kwenye hichi chama kipya nini?
   
 8. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #8
  May 28, 2010
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Bado ni siri mkubwa ila utaona vipeperushi! Jamaa yetu ana ID kibao siku hizi....nimemshtukia font zake!
   
 9. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #9
  May 28, 2010
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  Kama hajakanusha basi ina maana alisema au sio jamani?
   
 10. M

  MzeePunch JF-Expert Member

  #10
  May 28, 2010
  Joined: Jun 8, 2009
  Messages: 1,412
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Nadhani mwandishi hakumbana vizuri kwa maswali huyo Msekwa. Ina maana anakanusha kauli za viongozi wa Chama Cha Majambazi (CCM) ambazo CCJ wameziweka vizuri sana kuonyesha kuwa wanahujumiwa? Halafu huyu Msekwa naye siku hizi akili zake zinakuwa kama za Makamba tu. Ni pumba tupu.
   
 11. Tonge

  Tonge JF-Expert Member

  #11
  May 28, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 696
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Msekwa kafilisika kisiasa, namshauri apunzike siasa asije adhilika maana sasa anaongea tumba tupu.CCJ oyeeeeeeeeeeeee
   
 12. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #12
  May 28, 2010
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Not that easy CCJ
   
 13. E=mcsquared

  E=mcsquared JF-Expert Member

  #13
  May 28, 2010
  Joined: Apr 1, 2009
  Messages: 221
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Kwa mtizamo wangu, kwa mtu mwingine yeyote anayejua siasa ila siyo mwanasiasa, angeweza kudhani kuwa CCM imennuliwa na CCJ ili kuipigia debe kwa wananchi. Pengine labda mimi huwa nafikiria kinyume tofauti na binadamu wenzangu. Mikwala kwa CCJ ni debe moja kali sana kwa CCJ, kwa mtu aliye makini na siasa za hapa!
   
 14. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #14
  May 28, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Tatizo sijasoma Msekwa anasema upuuzi wenyewe ni upi? Kwa sababbu ni rahisi sana kumuita mtu mpuuzi kuliko kuonesha upuuzi wenyewe. Kwamba viongozi wa CCM hawajatoa kauli za kuonekana kujua kile msajili wa vyama vya siasa atafanya dhidi ya CCJ tena kwa uhakika mkubwa na kuwatisha wale wote wanaotaka kujiunga nacho? Kwamba CCM kupitia Marmo - Mbunge na kada wa CCM wamekula njama kukinyima CCJ usajili wa kudumu?
   
 15. Kitila Mkumbo

  Kitila Mkumbo Verified User

  #15
  May 28, 2010
  Joined: Feb 25, 2006
  Messages: 3,347
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Mlinitaka aseme 'ndiyo tumekula njama'-are you serious? Karibu kwenye siasa za upinzani MM mtayakuta mengi. Hapo bado hamjashinda uchaguzi lakini mkurugenzi wa uchaguzi anamtangaza ambaye hakushinda, na akishatamka yeye ndiyo imetoka hiyo, welcome to TZ politics!!
   
 16. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #16
  May 28, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  very true.. kuna gharama na ni lazima ilipwe.
   
 17. A

  Akili Kichwani JF-Expert Member

  #17
  May 28, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,504
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  .. ccj ni wapuuzi tu, watajiandaaje kushiriki uchaguzi wakati hawana chama?.... haya ndiyo ya kuchemsha maji ya ugali kisha unaanza safari ya kwenda kusaga unga! ...sasa akikuta mashine imeishiwa dizeli anasema mwenye mashine anamkosesha ugali wakati maji tayari yameishacheka, .. hawa ccj wataimba sana mwaka huu kila kukicha wanakuja na visingizio kibao, wamemuingiza mjini mpendazote na sasa kaamua kufa nao, heri mrema angalau enzi zake aliambulia kugombea na urais akajiandikia kahistoria... haahah...... watanzania bwana ... upuuzi mtupu
   
Loading...