Mimi kanishangaza Magufuli tu...
Juzi kati tu hapa katutangazia nyungu inaponya coronavirus... na kama kawaida, kuna watu walishangilia kwa vifijo na nderemo!
Siku chache baadae, Waziri wa Magufuli nae akaeleza ni namna gani angependa tuwe na Siku ya Nyungu ya Kitaifa!! Kwa kumuunga mkono Magufuli, watu wakaanza kupiga nyungu huku wakisambaza video mitandaoni!
Hapo tukawaona baadhi ya Wabunge wa CCM, Wachungaji, na wajinga wajinga wengine mitandaoni wakionesha kupiga nyungu!!
Hata wiki mbili hazijapita, Magufuli yule yule anatangaza tena kutaka kupeleka ndege Madagascar kufuata dawa ya coronavirus!
Sasa ya nini kuingia gharama ya kupeleka ndege hadi Madagascar wakati tayari Tanzania tuna nyungu?! Hiyo ndege si bora isafiri mikoani kukusanya malimao ili watu tupige nyungu!!
Dah, yaani nawahurumia sana wakazi wanaoishi maeneo yenye simba na fisi, manake mjomba simba au fisi akila mkono wa mtu mmoja tu, hapo kijijini lazima wapige kambi kutokana na utamu wa nyama iliyopigwa hadi malimao!