Mada zinazoomba ushauri zimeshamiri, Nini tatizo?

Kifurukutu

JF-Expert Member
Aug 29, 2013
4,628
6,669
Wakuu kila nikikatisha Mmu naona mada zinazohitaji ushauri kuhusiana na mahusiano yao na wapendwa wao zimekuwa nyingi hasa kipindi hiki.

Si jambo baya kuomba ushauri tena kwa watu wanaojua mambo hasa hapa mmu, lakini najiuliza ni nini tatizo kwa vijana wa sasa kushindwa kupambanua mambo katika uhusiano wa kimapenzi na kuamua uamuzi sahihi wenyewe?

Je ndio uwezo wa vijana wetu wa sasa wanauwezo mdogo wa kufikiri, kutafakari na kuamua mambo?

Najiuliza tu nini kimewakuta vijana wa leo katika mahusiano, yaani jambo dogo tu la kujiamulia lazima ulilete humu mmu!
 
Mie nadhani maisha mtaani yamekuwa tight sana so kijana kusema afikirie kutafuta pesa ya kodi ya pango,kulisha wazee sometimes kusomesha wadogo zake bado hajahonga mengine kama masuala ya mapenzi anaona asiyaweke kichwani anaomba msaada wa ushauri ili kichwa kipumzike japo kidogo.wale wanaokuwa wazito kuomba ushauri ndo hivyo wanajinyonga maana wanakuwa na msongo mkubwa sana wa mawazo.
 
Acha kuomba ushauri kuna watu hata kutongoza hawajui wanataka kutoa matangazo utafikili wanatangaza ajira mwenye shida atume maombi
 
Hamia kwenye majukwaa mengine aiseeeee......
Huku tuachie wenyewe wahusika bhana.....
UaijilaIimshe kuvaa kiatu ambacho hakikutoshi
 
Wakuu kila nikikatisha Mmu naona mada zinazohitaji ushauri kuhusiana na mahusiano yao na wapendwa wao zimekuwa nyingi hasa kipindi hiki.

Si jambo baya kuomba ushauri tena kwa watu wanaojua mambo hasa hapa mmu, lakini najiuliza ni nini tatizo kwa vijana wa sasa kushindwa kupambanua mambo katika uhusiano wa kimapenzi na kuamua uamuzi sahihi wenyewe?

Je ndio uwezo wa vijana wetu wa sasa wanauwezo mdogo wa kufikiri, kutafakari na kuamua mambo?

Najiuliza tu nini kimewakuta vijana wa leo katika mahusiano, yaani jambo dogo tu la kujiamulia lazima ulilete humu mmu!
mkuu sio kila kinachopostiwa Jf lazima kikupendeze!
Pita ivi
 
Back
Top Bottom