Mada: Siasa zilivyohamia mitandaoni

Mada: Siasa zilivyohamia mitandaoni

Shujaa Mwendazake

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2015
Posts
4,010
Reaction score
6,766
1629586404891.png
Mwenendo wa siasa nchini Tanzania umehamia mitandaoni hasa Twitter na Club House ambako kampeni na mijadala mbalimbali inafanyika ikiwakutanisha makundi ya watu tofauti wakiwemo viongozi wa Serikali.

Wanasiasa na wanaharakati wamekuwa wakitumia mitandao ya kijamii kutoa maoni na matamko kuhusiana na mambo mbalimbali yanayotokea ndani na nje ya Tanzania kwenye nyanja za kisiasa, kijamii na kiuchumi.

Takwimu zinaonyesha kwamba matumizi ya mtandao wa Twitter yanaongezeka zaidi kila mwezi na watumiaji wake huku mijadala ya kisiasa ikichukua nafasi kubwa.

Uchunguzi unaonyesha kuwa, tangu kupigwa marufuku kwa mikutano ya hadhara hasa ya kisiasa, jambo lililowafanya kubuni njia mbadala kupitia mitandao ya kijamii.

Tishio la maambukizi ya ugonjwa wa Uviko-19 pia ni sababu la mijadala na matamko ya kisiasa kutolewa kupitia mtandao wa Twitter, jambo ambalo limefanya matumizi ya mtandao huo kuongezeka hapa nchini.

Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na taasisi ya kimataifa ya Stat Counter, mtandao wa Twitter unaongoza kwa kuwa na watumiaji wengi kwa miezi minne mfululizo kuanzia Aprili hadi Julai, mwaka huu, ukifuatiwa na Facebook na Instagram.

Soma zaidi: Mitandao ya kijamii ilivyoshika uhai wa vyama vya siasa

Aprili, Twitter ilikuwa na asilimia 26.9 ya watumiaji wa mitandao ya kijamii wakati Facebook ikiwa na asilimia 29.3 na Instagram asilimia 4.49. Watumiaji wa Twitter waliongezeka Mei hadi kufikia asilimia 32.88 wakati Facebook wakiwa asilimia 29.14 na Instagram asilimia 5.1.

Juni, watumiaji wa Twitter walifika asilimia 43.81 wakati wa Facebook wakiwa asilimia 24.5 na Instagram asilimia 4.3. Mwezi uliofuata wa Julai, watumiaji wa Twitter waliongezeka hadi kufikia asilimia 46.47 wakati wa Facebook wakifikia asilimia 27.47 na Instagram asilimia 4.33.

Mmoja wa wanaharakati wanaoendesha mijadala katika mitandao ya kijamii ni Maria Sarungi ambaye Agosti 19, mwaka huu, aliongoza mjadala mwingine kupitia jukwaa lake linalotambulika kama “Maria Space”, mada kuu ikiwa ni Tume Huru ya Uchaguzi.

“Nilichojifunza kutoka Zambia ni kuwa wapiga kura ni key katika uchaguzi, kulinda kura. Lakini kwetu mfumo mzima umeshapinduliwa na hata sheria mbovu hazifuatwi,” ameandika Maria katika ukurasa wake wa Twitter.

Wanasiasa maarufu kama Tundu Lissu, Zitto Kabwe na Godbless Lema wamekuwa wakitumia jukwaa hilo kutoa maoni na kushiriki mijadala mbalimbali ya kisiasa inayoendeshwa katika mtandao huo

Mwananchi
 
Back
Top Bottom