Mada moto BBC radio: Wahadhiri wa vyuo vikuu kuwataka wasichana kinguvu ili wawape alama za juu za ufaulu.

Freed Freed

JF-Expert Member
Jun 27, 2017
6,248
6,509
Habari zenu jukwaani.

Ktk kipindi cha mjadala jumatano jioni tarehe 10/01/2018, BBC radio walimulika mapenzi ktk vyuo vikuu baina ya wahadhiri wa kiume na mabinti wanafunzi.

Watu walitiririka maoni yao na mjadala ulishirikisha wanafunzi, wahadhiri na wanataaluma wengine. Kwa ujumla pande zote zililaumiwa kwa tabia hii ovu ambapo inadaiwa baadhi ya lecturers wana mbinu ya kuwapata mabinti kwenye vitivo vyao huku wakiwapa alama za juu za ufaulu lakini kiuhalisia mhitimu hana uwezo wa kile kilichopo chetini kwake.

Pia wanafunzi wengine hudaiwa kujipendekeza wenyewe na sio kupewa alama tu bali pia pesa za kufanya mashindano ya kufukuzana na fashion na kundi rika lao.
Aidha wachangiaji wamedai baadhi ya wanafunzi wamekuwa na uthubutu wa kuwatupilia mbali ama kuwakataa kabisa wahadhiri hao mabazazi.

Kwa ujumla pande zote mbili zimelaumiwa kwa tabia hizi za vyuoni Africa Mashariki na kuaswa kuwa waadilifu na kutoa taarifa mahali husika pale upande mmoja unapokiuka maadili ya kitaaluma.
 
Sio mbaya ni namna ya kujiongeza katika kitengo chako kama ukiona ina manufaa kwako ...

Maisha yetu yamejaa ubinafsi sana tunaangalia jambo kwa maslahi binafsi yetu bila kujali athari za huko mbeleni..
 
Vijana wa vyuoni wanaamini zaidi kwenye vyeti. Wanaamini vyeti ndio maisha yao na bila vyeti maisha hakuna wakati kiuhalisia sio kweli.
Unaweza kuendesha maisha hata bila ya kuwa na vyeti vya magumashi.
 
chuo tanzania ni kufaulu iwe kwa njia halali au haram, suala-la- mapenzi ni vigumu kulidhibiti, hata waweke adhabu ya kifo
 
Siku moja nilishuhudia tulifanya test, baada ya kumaliza test kuna binti alifanya test ila baada ya hapo akaenda tena ofisini akaambiwa chana, anza upya.

Sikujua what was behind these.
 
Kuna siku yule Lara1 alisema ..mwalimu asipo kukula papa class .maosha yatakukula tigo mtaani.. Nafasi na taasisi nyingi upande wa ajira wanaahusudu sana the Almighty vyeti/ na G.P.A kwaiyo wanawake wengi wanaona kwani sh ngapi.. Na wengine ni kushindwa kupambana Vikwazao wanaowekewa ..
 
bila hata kumfelisha... kwa maisha ya sasa wadada wanavyopenda maisha mazuri na kuolewa ni wadada wachache sana ambao wana guts za kumkataa lecture akiwatongoza.. labda huyo lecture awe mzee mtu mzima..

ila kijana kijana na awe hajaoa wadada hawachomoi....
 
Wakirusha kipindi hicho youtube tuwekee tukione..

Hii tabia ndio ilivyo miaka mingi kwenye vyuo haswa vya Africa pia. Inasikitisha
 
Lecturer anamjuaje mwanafunzi kama sio mwanafunzi mwenyw kujilengesha. Tatizo Kwa wanafunzi sio wahaziri
 
nachokumbuka alisema hataniacha lakini maisha ya chuo yalimfanya anisahau ila maumivu yalishapona kovu limegoma kutoka na sitamsahau tunda kwa alichonifanyia fala huyu
 
Nikifiaka hapa ndipo nawakubali wachina, mchina haangalii vyeti! anaangalia perfomance kazini tu! i wish waajiri wote wangefata mfumo huu.
 
Back
Top Bottom