Freed Freed
JF-Expert Member
- Jun 27, 2017
- 6,221
- 6,461
Habari zenu jukwaani.
Ktk kipindi cha mjadala jumatano jioni tarehe 10/01/2018, BBC radio walimulika mapenzi ktk vyuo vikuu baina ya wahadhiri wa kiume na mabinti wanafunzi.
Watu walitiririka maoni yao na mjadala ulishirikisha wanafunzi, wahadhiri na wanataaluma wengine. Kwa ujumla pande zote zililaumiwa kwa tabia hii ovu ambapo inadaiwa baadhi ya lecturers wana mbinu ya kuwapata mabinti kwenye vitivo vyao huku wakiwapa alama za juu za ufaulu lakini kiuhalisia mhitimu hana uwezo wa kile kilichopo chetini kwake.
Pia wanafunzi wengine hudaiwa kujipendekeza wenyewe na sio kupewa alama tu bali pia pesa za kufanya mashindano ya kufukuzana na fashion na kundi rika lao.
Aidha wachangiaji wamedai baadhi ya wanafunzi wamekuwa na uthubutu wa kuwatupilia mbali ama kuwakataa kabisa wahadhiri hao mabazazi.
Kwa ujumla pande zote mbili zimelaumiwa kwa tabia hizi za vyuoni Africa Mashariki na kuaswa kuwa waadilifu na kutoa taarifa mahali husika pale upande mmoja unapokiuka maadili ya kitaaluma.