Mada maugo v/s fransis cheka

Mada maugo v/s fransis cheka

RasJah

JF-Expert Member
Joined
Nov 5, 2009
Posts
703
Reaction score
64
Wakuu kwa wale watakao kua PTA mutujuze nani atatoka na mkanda wa IBF na Mkoko wa milioni nane leo
Nawasilisha
 
pambano linaanza saa ngapi wakuu na uwanja upi. Nataka nitinge huko sina issue ya kufanya leo.......asanten
 
pambano linaanza saa ngapi wakuu na uwanja upi. Nataka nitinge huko sina issue ya kufanya leo.......asanten

Kutakuwa na mapambano ya utangulizi kuanzia saa 10 na saa 12 ndo pambano lianaanza rasmi dhidhi ya wawili hawa
 
Ndo nipo ndani ya ukumbi wa PTL nikisubiria pambano hili la kukata na shoka huku mashabiki wa cheka toka morogoro wakiwa wanapiga fuvuzela na kuuliza cheka mnamjua? Nitawapa update kadiri pambano linavyoendelea
 
Shine tupe upadates mkuu, saa kumi ndio hiyooo imewadia. Vipi afande sele keshapanda kumwaga mistari?? am told fransis cheka kaja na mabus ya washangiliaji toka moro. Mada nae kuna bonge la vijana toka maeneo ya ukonga,banana
 
Shine tupe upadates mkuu, saa kumi ndio hiyooo imewadia. Vipi afande sele keshapanda kumwaga mistari?? am told fransis cheka kaja na mabus ya washangiliaji toka moro. Mada nae kuna bonge la vijana toka maeneo ya ukonga,banana

Mpaka sasa hakuna pambano lililoanza na Afande bado hajafika ila vijana toka moro ndo nimewaona wamekuja na costa
 
Update
Refa ndo kaingia kukagua uwanja kwaajili ya mapambano ya utangulizi bila shaka kwenye mida ya saa 11 yanaeza anza rasmi
 
Update
pambano la kwanza la utangulizi ndo linaanza kwakweli sijaweza kuwtambua kwa majina ntawajuza pindi ntakapopata majina kwani mtangazaji hasikiki vizuri kutokana na base ya spika ni kubwa sana
 
Update
zengwe la pambano la kwanza mpiganaji mmoja ajaonekana na sasa mwenzake imembidi ashuke na sasa ni pambano la wanawake la utangulizi la wanawake mmoja nimempata kwa jina la asha ngedere ambapo mdo anapanda sasa tena kwa kujivuta sana, anafuatiwa na salma ambae amejitahidi kuwahi kupanda uwanjani tutaendelea kujuzana
 
Shine utujuze kila dakika inayoenda hasa pambano rasmi likianza!!
 
huyu mada maugo bora ashinde apate hilo gari tushamchoka na matusi yake kwenye madaladala...mtu ana mdomo mchafu kama nini!
 
Update
hatimae asha ngedere apigwa kwa point na salma ktk pambano la round 4. Na sasa linafuata pambano ka tangulizo jingine ambapo wapiganaji wanachelewa kweli kuingia uwanjani
 
Shine big up sana mkubwa... kazi kubwa unatufanyia wana JF. sie tuko huku mtwara ila upadates zako zitaidia kurusha hewani kwenye kipindi cha michezo hapa mtwara. Btw Majura nae yupo na anatoa live kwenye blog yake
 
Update
Mapambano ya utangulizi yameisha ambayo yalikuwa 7 yakachezwa sita kutokana na lile la kwanza mpinzani hajaonekana uwanjani cheka na maugo ndo walitakiwa waingie refa kaukataa uwanja ndo unafanyiwa marekebisho kidogo ndo waingie
 
Mkanda wanaoupambania ndo umepitishwa jukwaani kuonyeshwa
 
Update
cha kushangaza linaongezwa pambano jingine la 8 la utangulizi ambalo litakuwa la mwisho ktk haya ya utangulizi mmoja wao akiwa mdogo ake cheka
 
Shine...usitusahau wadau ambao hatupo PTA!mada huanzaga na kasi sana round za mwanzoni lakini kadri round zinavyoenda hupotea na kuanza kurusha makofi!sijui leo kama pambano litakuwa la burudani!matumla vs cheka ndo bout hujaa skills sana!
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom