Mada Maugo na Mabondia wa Urusi

John7371

JF-Expert Member
Apr 29, 2018
2,994
6,641
“Niliwahi kukataa pambano raundi ya kwanza huko Russia. Nilipigwa ngumi, nakinga mikono lakini nasikia ni kama chuma kimetua, naangukia kwenye kamba. Kocha wangu hataki kutupa taulo. Raundi imeisha anasema ingia ujitahidi, nikamuambia siingi, ukitaka ingia mwenyewe” -Mada Maugo

Kumekuwa na baadhi ya shuhuda juu ya Mabondia wa Russia na Ukraine kutoka kwa baadhi ya mabondia wa hapa nyumbani kwamba ni mabondia hatari sana na hivyo waswahili wajiepushe na mapambano yao,Je,kuna ukweli kwenye haya?
 
Ukweli ni kwamba mabondia wa huko wanadanganya uzito tena kwa kushirikiana na mapromota wa mabondia wa Tanzania

Inamaana mabondia kutoka Tanzania wanapigana na mabondia wa uzito wa juu bila wao kujua sababu wanafanyiwa ujanja ujanja wakati wa kupima uzito.

Jiulize mbona kwenye chat za mabondia bora duniani hao jamaa wa Urusi sio wengi kivile kaka kweli wana ubora huo unaosemwa?
 
Sasa mwakinyo ni muda huu wake kwenda Urusi akatuwakilishe vyema
 
Back
Top Bottom