Mada maalumu ya picha za watu maarufu waliowahi kuwepo na waliopo duniani

IMG_7011.jpg


Kutana na Alexander Mkubwa, mfalme wa Macedonia aliyeanza kutawala aliwa na umri wa miaka 20 tu na kuwa mtawala wa robo tatu ya watu wote duniani alipofikisha miaka 30!

Inasemekana Julius Caesar alipojiona amefanya mambo makubwa kwa kutwaa maeneo makubwa kwa ajili ya ufalme wa Rumi akiwa na umri wa miaka 50, aliangua kilio pale alipoambiwa alexander alifanya mara 10 ya kile alichofanya akiwa na miaka 30 tu.

Anatajwa kama miongoni wa watu wenye uwezo mkubwa kivita akiwa katika kundi mojana Julius Caesar, Genghis Khan na Napoleon Bonaparte.
 
Jesse Owens alimkasirisha Hitler baada ya kushinda medali 4 za dhahabu kwa mpigo huko Berlin mwaka 1936.

Alipopata ushindi wa medali ya tatu tu Hitler aliondoka uwanjani kwa hasira kwani yeye alidhania haiwezekani kwa mtu mweusi kuweza kupata ushindi ule. Chumbani kwa hotelini kwake alipofikizia yalipenyezwa mapicha ya nyani (hasira za wazungu kwa ushindi wake huo).

On August 3, 1936, he won the first of four gold medals in the following categories: 100 meter, 200 meter, the long jump, and 4 × 100 meter relay.

01.jpg
 
IMG_7012.jpg


Huyu ni Genghis Khan, Khan au kiongozi wa juu kabisa wa taifa la Mongolia aliyetawala kile kinachoaminika kuwa miongoni mwa falme kubwa zaidi za muda wote. Ufalme wa mongolia ulianzia China hadi kwenye mipaka kati ya ulaya magharibi na masharik.

Pia natajwa kuwa miongoni mwa watu wenye uwezo mkubwa wa kijeshi kuwahi kutokea akiwa kwenye kundi moja na Alexander Mkubwa, Julius Caesar na Napoleon Bonaparte.
 
IMG_7014.jpg


Shaka Kasenzangakona, Shaka Zulu, chifu wa wazulu aliyetawala eneo lubwa la Afrika ya Kusini ya leo. Shaka alikuwa mtoto haramu kati ya mfalme ya wazulu, Kasenzangakona na binti mfalme wa Elangeni, Nandi.

Uharamu wa Shaka ulipelekea kukataliwa na baba yake hivyo yeye na mama yake waliishi maisha ya kutangatanga hadi pale walipopewa hifadhi na mfalme Dingiswayo kutokana na uwezo wake mkubwa kijeshi.

Baada ya Dingiswayo kufa askari wa jeshi, chini ya Ngomane walimchagua shaka awe mfalme wao mpya, mda mchache baadaye Kasenzangakona naye alikufa hivyo shaka akarudi Uzulu kwenda kuchukua Ufalme wa wazulu kwani amini kuwa ni haki yake kama mtoto wa kwanza wa Kasenzangakona.

Hapo ndipo safari ya Shaka kuzipiga falme nyingine na kuishia kutawala eneo kubwa la kusini mwa afrika. Shaka zulu alikufa mwaka 1828 baada ya kuuawa na kaka zake Mhlanga na Dingane kwa kile walichodai kuwa ni katika kuchukua hatua dhidi ya kuzidi kwa ukatili wa Shaka ulisababishwa na kifo cha mama yake Nandi.

Shaka anatajwa kuwa miongoni mwa viongozi wenye uwezo mkubwa kijeshi kama ilivyo kwa Julius Caesar na Napoleon Bonaparte.

Ukitaka kuamini kuwa Shaka alikuwa hatari, Sikia, baada ya shaka kukuza vuguvugu la mfekane huko afrika kusini, baadhi ya wangoni walishindwa kuvumilia hivyo wakakimbia vita na kuja maeneo ya afrika mashariki. Walipofika afrika mashariki, wangoni waliokimbia vita waligeuka kuwa mwiba mchungu kwa watemi wababe wa maeneo ya Afrika mashariki kama mtemi Mirambo.

IMG_7015.jpg


Ufalme wa shaka katika kilele chake
 
IMG_7019.jpg


Gaius Octavius Augustus Caesar, mfalme wa kwanza wa Ufalme wa Rumi, mfalme wa Rumi aliyetawala kwa muda mrefu zaidi l (miaka 40), mtu aliyesababisha Yesu azaliwe kwenye banda la ng’ombe na kondoo, miongoni mwa watu matajiri kuwahi kutokea, sababu ya mwezi wa nane kuitwa mwezi Agosti, mmiliki binafsi wa misri, mtoto wa kufikia wa Julius Caesar.
 
Shaka Zulu, chifu wa wazulu aliyetawala eneo lubwa la Afrika ya Kusini ya leo. Shaka alikuwa mtoto haramu kati ya mfalme ya wazulu, Kasenzangakona na binti mfalme wa Elangeni, Nandi.

Uharamu wa Shaka ulipelekea kukataliwa na baba yake hivyo yeye na mama yake waliishi maisha ya kutangatanga hadi pale walipopewa hifadhi na mfalme Dingiswayo kutokana na uwezo wake mkubwa kijeshi.
Alikuwa na ukatili wa ukichaa kabisa
 
Alikuwa na ukatili wa ukichaa kabisa

Kweli kabisa, mapenzi ya Shaka kwa mama yake yalimfanya apate shida kiakili baada ya mama yake kufa. Aliamrisha nchi yote afanye maombolezo kwa miaka 3 na kuweka marufuku kwa wanawake kishika mimba katika kipindi chote hicho, adhabu ya kifo ilifuata kwa waliovunja amri hiyo.

Katika kipindi hicho cha maombolezo, Shaka aliua watu wengi zaidi katika kipindi hiki kuliko wale walio walikufa katika vita zake.
 
Back
Top Bottom