Mada maalumu ya picha za watu maarufu waliowahi kuwepo na waliopo duniani

View attachment 1798723View attachment 1798724

Julius Caesar maarufu kama Kaisari alikuwa ni mtawala wa kisiasa na kijeshi enzi za Warumi.

Anakumbukwa hasa kwa mafanikio mbalimbali yanayoonekana kuathiri dunia hadi leo.

Baadhi ya mafanikio hayo ni:

1.Kama kiongozi wa kijeshi aliteka Gallia (Ufaransa) na kuifanya jimbo la Kiroma. Kutokana na hiyo lugha ya Kifaransa na lugha nyingi kama Kireno, Kihispanyola n.k (kwa ujumla wake huitwa Romace languages) ni lugha zenye ukaribu sana na Kilatini, lugha ya Roma ya Kale.

2.Waroma wa Kale walimheshimu kushinda viongozi wote waliomfuata au kutangulia akatangazwa kuwa mungu.

Jina lake lilipata kuwa neno kwa ajili ya cheo cha watawala wa Kiroma waliomfuata. Kutokana na badiliko hilo la jina "Caesar" kuwa cheo, lugha mbalimbali zilipokea cheo hicho kama vile Kijerumani ("Kaiser"), Kirusi ("Tsar") na Kiswahili ("Kaisari" - kutokana na neno la Kijerumani).

3. Aliunda kalenda ambayo imekuwa msingi wa kalenda ya kimataifa leo (Kalenda ya Juliasi). Kwa heshima yake, mwezi wa saba unaitwa Julai.

4.Katika historia ya Roma yee ndie aliepelekea kufa kwa Jamhuri ya Roma (Roman Republic) na kuzaliwa Dola la Roma (Roman Empire) aliloliwekea misingi na lililotawala sehemu kubwa ya bara la Ulaya na Asia kwa miongo mingi.

Moja ya misemo (quotes) maarufu ya Kaisari ni pamoja na "Veni, Vidi, Vici" kwa Kiingereza "I came, I saw, I concured" kiswahili "Nilikuja, Nikaona, Nikashinda" huu msemo aliutumia katika ripoti yake ya vita baada ya kushinda vita iliyomchukua muda mfupi dhidi ya Pharnaces II wa Pontus.
Chaliifrancisco shukrani sana kwa maelezo mazuri,uzi mzuri sana naongeza vitu kichwani ingependeza kila anayewekwa hapa hasa hawa watawala waliofanya mapinduzi makubwa kukawa na maelezo kidogo kuwaelezea.

Sent from my Redmi Note 5 using JamiiForums mobile app
 
Picha ya kudhaniwa na ya kuchora ya mfalme sedekia wa Yuda.
Huyu ndie aliekuwa mfalme wa mwisho wa taifa la Israel ambaye alisabisha taifa hilo kuvamiwa na kuharibiwa mji wa yerusalem.
Mji uliangamizwa kabisa, watoto wa mfalme huyo waliuwawa wote .
Ni moja ya watawala waliowahi kupitia nyakati ngumu kuliko wote kabla ya kuondoka kwenye uso wa dunia.
Zedekiah(0).jpg
Zedekiah.jpg
 
Milton Obote pamoja na Edward Kabaka mutesa .
Edward mutesa alikua rais wa taifa la Uganda , akitokea kwenye koo ya mfalme wa buganda Kabaka.
Alishika madaraka ya nchi akiwa kama mkuu wa nchi na Milton Obote akiwa waziri mkuu.

Lakini Milton alifanikiwa kumuondoa madarakani na kumuondoa nchini mpaka akafia uhamishoni.

Milton alipinduliwa na jenerali yower kaguta Museveni.
Milton-Obote.jpg
1347-296x450.jpg
 
Cecil Rhodes.
Ni mwingereza aliewahi kuishi nchini Afrika ya kusini.

Huko alikua mfanyabiasha na aliweza kuwa mfanyabisha mkubwa wa madini
Aliingia kwenye siasa na kupata nafasi za kiuongozi huko Afrika ya kusini.

Kwenye biashara zake aliweza kutanuka mpaka kufikia maeneo ya kaskazini kwa nchi ya Afrika ya kusini, huko alitengeneza makoloni yake yaliojulikana kama Rhodesia ya kusini na Rhodesia ya kaskazini.

Hizi ndio nchi za Zambia na Zimbabwe.

Historia ya Afrika ina mengi ya kujifunza badi , kujua wapi tulipo, tulipotoka na tunapoelekea.
 

Attachments

  • HRT_BISHM_283-001.jpg
    HRT_BISHM_283-001.jpg
    32.9 KB · Views: 7
  • RHODES_CECIL.jpg
    RHODES_CECIL.jpg
    28.4 KB · Views: 6
Picha ya kudhaniwa na ya kuchora ya mfalme sedekia wa Yuda.
Huyu ndie aliekuwa mfalme wa mwisho wa taifa la Israel ambaye alisabisha taifa hilo kuvamiwa na kuharibiwa mji wa yerusalem.
Mji uliangamizwa kabisa, watoto wa mfalme huyo waliuwawa wote .
Ni moja ya watawala waliowahi kupitia nyakati ngumu kuliko wote kabla ya kuondoka kwenye uso wa dunia.View attachment 2500663View attachment 2500665

Mfalme wa Yuda
 
2007 aliuwa kwa kupigwa risasi 2 na bomu juu ! Kufa kwake kuliambatana na watu 30
Bomu lake lilitegeshwa na simu yake ya blackberry (kwa wale wanaoikumbuka hii simu).

Alipigiwa akiwa kwenye hadhara na alipopokea tu kumbe ndiyo ilikuwa trigger ya bomu.
 
IMG_6742.jpg


Hii ni sanamu ya mfalme wa dola ya Rumi Constantine. Constantine anashikilia mfalme wa kwanza wa Rumi kubadili dini na kuwa Mkristo, pia Constantine aliufanya ukristo kuwa dini rasmi ya dola ya Rumi.
Mfalme Constantine ndiye muasisi wa miongoni mwa miji maarufu ya kale, mji wa Constantinople.
 
Thomas of Aquitaine (Tomas wa akwino)
Ana julikana kama mwalimu wa kanisa, profesa wa theologia , Mtakatifu katika kanisa, msimamizi wa wanafunzi wote,wanateolojia wote nk.

Ni mtu mzaliwa wa huko Italy kati ya mwaka 1224.

Alikua pia mtawa wa kanisa katoliki, ambaye aliacha athari chanya kubwa sana katika mafundisho ya kanisa haswa elimu juu ya Mungu.

Aliweza pia kutunga vitabu vingi sana ambavyo mpaka leo hivi vinatumika katika vyuo vya theologia.

Moja ya kitabu maarufu alicho kiandika ni Samma theological.

Ni kitabu kilichotoa definition sahihi ya Mungu.
Kukikiwa na mgawanyiko wa sehemu 3 zinazo mzungumzia Mungu kwa uhalisia wake, jinsi Mungu anavyo patikana kwa watu, na jinsi Mungu anavyo patikana kwa Yesu.

Katika sehemu hio ya tatu hakuweza kukamilisha kwa jinsi alivyo kusudia, kwa namna hiyo hiko kitabu kinajulikana kuwa hakikukamilika, au kiliishia njiani.

Pamoja na hayo yote ni mtu ambaye dunia ilijaliwa na natumaini nyakati zitapita lakini Thomas hata sahaulika kwa urahisi .

Maisha yake na kazi zake alizofanya akiwa hai zikiwekwa sehemu moja kama simulizi natumaini litakua ni simulizi kubwa kuliko masimulizi yoyote yale.
sv.-tomas-akvinsky.jpg
Summa-Theologica_5-Volume-Set.jpg
 
IMG_6229.jpg


Pichani ni Lionel Messi mchezaji bora wa muda wote kwenye mchezo wa mpira wa miguu. Mwaka 2022 ulikuwa mwaka mzuri sana kwa Messi kwani alifanikiwa kutimiza ndoto yake ya tangu utotoni, kushinda kombe la dunia akiwa na timu yake ya taifa ya Argentina.
 
View attachment 2501821

Hii ni sanamu ya mfalme wa dola ya Rumi Constantine. Constantine anashikilia mfalme wa kwanza wa Rumi kubadili dini na kuwa Mkristo, pia Constantine aliufanya ukristo kuwa dini rasmi ya dola ya Rumi.
Mfalme Constantine ndiye muasisi wa miongoni mwa miji maarufu ya kale, mji wa Constantinople.
Pia ikumbukwe kwamba huko kubadili dini kuliambatana na kukaa darasani kusoma mafundisho kama wanavyo soma sasa wale wanaotaka kuingia ukatoliki, huwa wanaitwa wakatakumeni.
Darasa lao ni kwa miaka mitatu mfululizo, hata huyo mfalme alifundushwa dini kwa miaka mitatu ndio akapokekewe katika ukatoliki na ukristo kwa ujumla.
 
View attachment 2501834

Pichani ni Lionel Messi mchezaji bora wa muda wote kwenye mchezo wa mpira wa miguu. Mwaka 2022 ulikuwa mwaka mzuri sana kwa Messi kwani alifanikiwa kutimiza ndoto yake ya tangu utotoni, kushinda kombe la dunia akiwa na timu yake ya taifa ya Argentina.
Hakika, huyu ndugu ulimwengu wa soka hauta msahau kwa miaka ya hivi karibuni.
 
akini pia ina, mashaka yake, 1-jamaa aliiteka ndege sababu ya njaa ya pesa?
2-bomu alilobeba, lilikuwa la kazi gani kama lilikuwa sio la kulipuliwa.
3-alipitaje na bomb bila kuwa dictated pale airport, pamoja na kuwa kuna scans imara.
4-Ndege aliyoiteka inasemekana huwa inatumika sana sana na watu wa security wa ndani ya serikali, ilikuwaje mtu yeyote ku book ticket ya ndege hiyo bila kuwa checked vizuri ni nani hata kama shirika la ndege ni public.
Ijapokuwa masuali yako ni ya zamani kidogo lakini enzi za DB Cooper hakukuwa na security issues kusafiri na ndege.

Watu walikuwa hawachekiwi ni kama unapanda basi tu, hata tiketi unanunua airport bila hata passport wala kitambulisho.

Usilinganishe na hali ya sasa hivi
 
IMG_7008.jpg


Napoleon Bonaparte, jenerali 1799-1804 na mfalme wa ufaransa 1804-1814.

Napoleon anatazamwa kama mmoja wa majenerali bora wa muda wote kuwahi kutoke akiwa katika kundi moja na watu wenye uwezo mkubwa wa kijeshi kama Julius Caesar, Alexander Mkubwa na Genghis Khan.

Napoleona alipigana vita vingi vikubwa dhidi ya mataifa mbalimbali ya ulaya katika mfululizo wa vita vijulikanavyo kama vita vya kiNapoleon. Vita hivyo vilipelekea Napoleon kuishinda na kushikilia sehemu kubwa ya ulaya hadi pale alipishindwa katika vita vya Waterloo dhidi ya waingereza.

Napoleona alikufa mwaka 1821 akiwa mpweke katika kisiwa cha St. Helena kilichopo katikakti ya bahari ya pacific akiwa na umri wa miaka 51.
 
Back
Top Bottom