hypothalamus
Senior Member
- Feb 19, 2018
- 126
- 153
Kwa wale wahitimu wa kidato cha nne wanaotamani kujiunga na fani mbalimbali za afya hii inaweza ikawa msaada kwao
Disclaimer:Nimezisort fani hizi kwa "utashi wangu" wa jinsi ninavyoona demand ya fani husika kwa taifa kwa sasa na sio official sorting kutoka mamlaka yoyote ile
1.Diagnostic Radiography
Fani hii humuandaa mwanafunzi kuwa mtaalamu wa utumiaji wa vifaa mbalimbali vya uchunguzi wa magonjwa,tofauti na mtu wa maabara huyu hutumia teknolojia kama za mionzi,sumaku na sauti
Vigezo vyake ni "C" katika Chemistry,Physics na Biology .D kwenye Basic mathematics na English
Fani hii hutolewa Muhimbili na Bugando tu
Fani hii haina degree Tanzania kwa sasa,hivyo diploma bado ni hot cake kikubwa ni comptency ya mwanafunzi
2.Optometry
Fani hii humuandaa mwanafunzi kuwa mtaalamu wa uchunguzi na visadizi vya macho kuona(utaalamu wa miwani)
Vigezo vyake ni "C" katika Chemistry na Biology; na "D" katika Basic Mathematics na Physics
Fani hutolewa KCMC tu
Ni fani nzuri kwa sababu moja ya matatizo yanaongezeka kwa kasi Tanzania ni matatizo ya macho
3.Nursing
Fani hii humuaandaa mwanafunzi kuwa muuguzi wa level ya diploma na mara nyingi huwa ni muuguzi anae fit kwenye aina zote za nursing yani General Nurse
"C" katika Chemistry na Biology; na "D" katika Basic Mathematics, Physics
Kuna baadhi ya vyuo huwa hawaangalii C kwenye chemistry
Uzuri wa Nursing inafursa nyingi nje na ndani ya hospitali
Ndani ya hospitali hakuna department ambayo hutomkuta Nurse
Nje ya hospital ma nurse wanafanya kazi kwenye NGOs,mashirika ya kimataifa ya afya na wakimbizi,foundations za afya kama Mkapa foundation
4.Pharmeutrical sciences
Hii ni fani inayomuandaa mwanafunzi kuwa msaidizi wa mfamasia
"C" katika Chemistry na Biology; na "D" katika Basic Mathematics, Physics/Engineering Sciences na English
5.Clinical medicine
Hii ni fani ambayo mwanafunzi hupewa mafunzo ya kuwa daktari msaidizi,wenye taaluma hii mara nyingi utawakuta katika level ya zahanati mpaka vituo vya afya

6.Dentistry
Fani hii humuandaa mwanafunzi kuwa daktari msaidizi wa meno

7.Physiotherapy
Fani inayomuandaa mwanafunzi kuwa mtaalamu msaidizi wa mazoezi ya kitaalamu ya viuongo
"C" katika Chemistry na Biology; na "D" katika Basic Mathematics na Physics
8.Nursing midwfery
Hii ni fani inayomuandaa mwanafunzi kuegemea kwenye tawi moja la nursing la ukunga yani afya ya mama na mtoto
"C" katika Chemistry na Biology; na "D" Physics na English,wenye mswaki wa hesabu hii wanaweza kuingia
9.Medical laboratory
Hii ni fani inayomuandaa mwanafunzi kuwa mtaalamu msaidizi wa maabara za afya
"C" katika Chemistry na Biology; na "D" katika Basic Mathematics, Physics na English
10.Orthopaedic technology
Fani humuandaa mwanafunzi kuwa mtaalamu msaidizi wa teknolojia za viuongo bandia
"C" katika Chemistry,Physics na Biology au Basic Mathematics
Fani hii hutolewa na chou cha Muhimbili tu kupitia teaching centre ya KCMC
11.Environmental health sciences
Fani hii humuandaa mwanafunzi kuwa mtaalamu msaidizi wa uzuiaji wa magonjwa kwa kutunza mazingira mara nyingi huwajiriwa kama mabwana afya

12.Community health
Fani hii ambayo ni tawi la Nursing humuandaa mwanafunzi kuwa mshauri na muangalizi wa afya ya jamii
“D” 4 ambapo moja ya D hizo iwe ya Biology
Kwa ambao vigezo havijakaa vizuri kidogo wanaweza kuanzia certificate miaka miwili ambapo kwa course nyingi huwa unatakiwa kuwa na D kwenye masomo yote ya sayansi pamoja na English