Licha ya kushinda ndege hiyo, Armando sasa anakabiliwa na uwezekano wa kuiuza kutokana na gharama kubwa za matengenezo na kuhifadhi.
Armando, ambaye ni rubani wa kibiashara na mume, alishiriki shindano la Mr. Beast mwaka huu la kuishi siku 100 ndani ya ndege binafsi aina ya Hawker 800XP yenye thamani ya dola za kimarekani milioni $2.5 ili kuweza kumiliki ndege hiyo endapo angeweza.
"Survive 100 Days Trapped In A Private Jet, Keep It,"
MrBeast alimtambulisha mshiriki mpya, Armando, ambaye aliombwa kukaa ndani ya ndege kwa siku 100 mfululizo miezi michache iliyopita.
Armando alitumia zaidi ya miezi mitatu kwenye ndege ya kibinafsi ya MrBeast bila kuruhusiwa kukanyaga ardhini hadi changamoto hiyo ikamilike.
Ndege hiyo haikuwa ile kama jumba la kifahari watu wangeweza kutarajia, bali ilikuwa ndogo, na iliyojifinya ndani.
Armando alikataa ofa za starehe kama vile kitanda au kuoga, kwa vile zilikuja na masharti.
MrBeast alitoa matoleo ofa mpya kila wakati lakini tu ikiwa Armando atakubali kukatwa zawadi ya mwisho.
Armando alisema hapana, kila wakati.
Kila baada ya siku 10, MrBeast aliinua dau, na kumpa Armando dola $100,000 ili akatize shindano na kuondoka, na hadi kufikia dola $250,000.
Kufikia Siku ya 90, ofa ilifikia kilele cha dila $500,000, dola nusu milioni taslimu, papo hapo. Armando alikaa.
Siku ya 90, MrBeast alimpa Armando $500,000 ili kuongeza muda wa kuishi ndaani ya ndege hiyo kwa siku nyingine 100. Ingawa alijaribiwa, rubani aliamua kutoendelea, akitaja mkazo wa kihisia moyo wa kuwa mbali na familia yake na ugumu wa kuishi bila mawasiliano.
Siku ya 100, Armando alifungua milango ya ndege, akizuia machozi.
MrBeast alimpa chaguo moja la mwisho: kuchukua pesa taslimu $500,000 au ndege ya kibinafsi, Armando alichagua ndege ya kibinafsi, akisema ni kitu ambacho angeweza kurithisha kwa mtoto wake.