Mada maalum ya magari: Uzoefu, ushauri na maswali

Badili engine kuepuka gharama zaidi

Mkuu vp kuhusu 3sg E.

Aisee mi engine yangu ni YAMAHA 3SG E, beam nna muda nayo sasa lkn imekua inakata timing belt mara kwa mara na kupindisha valve, belt iliokuja na gari ilidumu sana. Nilipoanza kuweka hizi za madukani imekua shida. Kuna wakati nimefunga belt miez mitatu inakata fundi anashauri ule haukua mzuri wakati huu tununue aina flani ya japan ni nzuri sana tukiweka ni yale yale.

Naomba kuuliza tabia ya kukata belt kwa hii engine ni kawaida ama kuna shida pia kwa fundi namna ya ufungaji wa hio belt au head...
 
Umepima crane shaft?

Hapana mkuu:

Sina uhakika sana kama kuna kitu tumepima, uhakika ni kwamba tumekua tukihangaika na belt tuu bila kutafuta tatizo linasababishwa na nn, mara nyingi hisia imekua ni belt haikua original.

Labda unipe maelezo kidogo kuhusu hio crane shaft ni kitu gani na mahusiano yake na kukata timing belt.
 
Jaribu kwanza kufanya hivyo tafadhali
 
Wakuu Samahanini kidogo.

Nauza mashine za kuchanganya zege ( concrete mixer). Ni brand ya Honda , zina HP 8 kila moja na zinatumia Petrol. Ziko mbili na zimetumika nje( abroad) ziko in very good condition. Kwa mwenye uhitaji naomba ani PM.

Asanteni
 
Wakuu Samahanini kidogo..
Nauza mashine za kuchanganya zege ( concrete mixer). Ni brand ya Honda , zina HP 8 kila moja na zinatumia Petrol. Ziko mbili na zimetumika nje( abroad) ziko in very good condition. Kwa mwenye uhitaji naomba ani PM.
Asanteni
Nimekupm
 
Habari wakuu. Samahani naomba kujuzwa, et inawezekana kuchukua Engine ya Toyota Wish ukaweka kwenye Nissan X Trail?
Kama inawezekana, je Ulaji wa mafuta kitaalamu inabaki kuwa wa Wish au laah?
Febraethan kwanini unataka kuacha injini ya nissan extrail na kutaka kuweka ya Toyota wish kwenye hiyo Nissan, nini kimetokea? injini ya extral imekuletea maudhi/kero gani
 
Habari wakuu,
Nina harrier matako ya nyani, Naomba msaada kujua kwa nini mara nyingi nikisha-lock milango baada ya muda kidogo inaanza kupiga alarm. Kwa kweli huwa inanikera sana na inapiga kelele kweli kweli. Sijafunga system mpya ya alarm iliyopo ni ya humo humo kwenye gari.
 
Nenda Karume kwa nyuma kuna garage pale wanaweza kukusaidia mie niliwahi peleka ya kwangu Ila zamani kidogo
 
Wakuu naomba mwenye uzoefu na gari za JEEP hasa hizi model za karibuni za bodi ya mayaimayai. Je zinapaatikana show rooms? vipi kuhusu uimara wake, usumbufu nk.
 
Back
Top Bottom