Mada maalum ya magari: Uzoefu, ushauri na maswali

Habari wakuu. Samahani naomba kujuzwa, et inawezekana kuchukua Engine ya Toyota Wish ukaweka kwenye Nissan X Trail?
Kama inawezekana, je Ulaji wa mafuta kitaalamu inabaki kuwa wa Wish au laah?
 
Habari wakuu. Samahani naomba kujuzwa, et inawezekana kuchukua Engine ya Toyota Wish ukaweka kwenye Nissan X Trail?
Kama inawezekana, je Ulaji wa mafuta kitaalamu inabaki kuwa wa Wish au laah?
Mmh hizo ni brand mbili tofauti hapo itabidi ubadili mifumo kama mitatu hivi
Umeme
Control box
Gear box
Pamoja na hiyo engine
 
Naomba kufahamu hivi ukijaza gari full tank mpaka mafuta yakaribie kumwagika nje/ au kuinua gari ili mafuta yaingie zaidi ni kweli huu mtindo unaharibu fuel gauge au boya la tank au pump ya kwenye tank? Hasa gari ya petrol?
Sio kivile lakini pia haishauriwi ili kutoa nafasi ya kumupua
 
Naomba ushauri Mshana Jr au expert yeyote pia..Nina Raum old model nliinunua ikiwa imefungwa sport rim na nmeitumia kwa miezi Kama miwili bila kuwa na tatizo lolote upande wa wheels ila Cha kushangaza kwa takribani mwezi na kitu imekuwa na tatizo linalojirudia la kupoteza allignment kiasi kwamba kwa mwezi tu huo nmebadili tairi zote za mbele awamu tatu Hadi nmeamua kupaki gari, nmebadili mafundi watatu ila tatizo liko pale pale haichukui hata siku mbili inaanza Tena Kula tairi excessively.
Kuna fundi alishauri tufunge tie rod end mpya tumefanya hivyo ahida ipo palepale. Nmempelekea pia fundi anaetumia vifaa kufanya allignment ila Bado hata yeye ilimshinda .. naomba ushauri kujua ikiwa hata rims zinachangia Hilo ama la!
 
Naomba nisitoe jibu la kubahatisha ..je uko wapi? Lakini je umejaribu kucheki stabilizer links ziko sawa?
 
Niko Mbamba bay Ruvuma...zaidi ya kubadili tie rod end hakuna kingine tulichoangalia na kukishughulikia
Stabilizer links zikichoka alignment husumbua.. Na je wheel balancing ulifanya? Unaweza kufanya alignment kumbe shida iko kwenye balance
 
Nimesoma huu uzi kuanzia mwanzo hadi mwisho,nilichojifunza ni kuwa mafundi wa Tanzania huwa wanaharibu magari badala ya kutengeneza magari.
Nakubaliana na wewe kwa asilimia 85%, gari yangu niliagiza nje ni aina ya harrier, ilikuwa fresh sana, ila kuna kakitu kamoja kaliaharibika, nikaenda kutengeneza gareji moja hapa mjini, yani tokea hapo nimekuwa ni mtu wa kuenda gereji kila siku yani...mala hiki mala kile... duh hata nashindwa nifanyeje yani
 
Mambo vp wakuu kina mshana na wengineo bila shaka pasaka imeenda vema. Niko dar nina shida na half cut ya toyota will cypher. Kama kuna mtu mwenye nayo au mwenye kufaham wap naweza pata kwa urahisi nipate contact itakua vema zaid. Natanguliza shukrani za dhati.
IMG-20210404-WA0001.jpg
 
Mambo vp wakuu kina mshana na wengineo bila shaka pasaka imeenda vema. Niko dar nina shida na half cut ya toyota will cypher. Kama kuna mtu mwenye nayo au mwenye kufaham wap naweza pata kwa urahisi nipate contact itakua vema zaid. Natanguliza shukrani za dhati.View attachment 1743284
Salama kabisa hebu tuwasiliane kesho tafadhali
 
Back
Top Bottom